DOKEZO TAKUKURU Wakamateni Sheikh, Alhad Mussa Salum, RITA, Mkurugenzi, Ardhi na Polisi kwa kuvunja Msikiti wa Mwenge kwa Mabavu

DOKEZO TAKUKURU Wakamateni Sheikh, Alhad Mussa Salum, RITA, Mkurugenzi, Ardhi na Polisi kwa kuvunja Msikiti wa Mwenge kwa Mabavu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mleta mada ni mnufaika wa msikiti kiuchumi na katengeneza document fake. Nenda mahakamani kama ww Kidume. Na hakimu anaifahamu issue yote hii na document zako fake
 
Hebu wewe tuambie ukweli. Tuoneshe picha ya huo Msikiti unaojengwa kwa ndani.
Jamaa kaingia mkataba na hao watu wa miaka 15 kujenga maduka kuzunguka msikiti then ndan atajenga msikiti mkubwa wa gorofa. na unajengwa muda huu sambamba na maduka. Atamiliki miaka 15 then anawaachia. Mbona ni kawaida kila mahali inafanyika hivyo.
 
Endeleeni na Gwajima na Mwamposya kumbe yenu yanawafika puani
 
Salaam Wakuu,

Jamani tunaomba msaada, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum atatutoa roho.

Baada ya rais Samia kuingia Madarakani, wale watu wa pesa inaongea Wamerudi kwa kasi ya ajabu. Mtu mwenye pesa sasa anaweza kufanya chochote na usimfanye kitu.

Katika Mkoa wa Dar Es Salaam kuna Taajiri amewaweka mfukoni Watendaji wote wa Wilaya ya Kinondoni hawa Wakina Gondwe.

Kipindi cha nyumba, kuna Tajiri alitaka kununua Msikiti ili ajenge maduka, Bodi ya Wadhamini ya Msikiti Wakamkatalia. Ikabidi Tajiri huyo amtumie Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ambaye alitetengeneza Bodi mpya ya wadhamni wasio hata waumin wa Msikiti ili Waweze kumuuza Tajiri na Wakafanikiwa. Kumbuka Msikiti unamilikiwa na Taasisi ya Mwenge Mosque & Islamic Centre. Hakuna aliyeshirikishwa kwenye Uteuzi wa Bodi Mpya.

Waumini Walilalamika RITA, Ardhi na kwa Mkurugenzi wa Kinondoni bila mafanikio.
View attachment 2359556
Wakashangaa Hati ya jengo wanayo wao lakini wakashangaa Msikiti unavunjwa na kuanza kujengwa Maduka. Walipojaribu kuzuia, Wakaitwa Polisi wa Oysterbay wakawakamata wote walioonekana kulalamika na kuwekwa ndani bila dhamana. Walikaa sana Polisi kwa kosa la kifanya fujo Msikitini. Aliyekua Msimamizi Mkuu wa Msikiti akafa kifo cha gafla kwani aliteswa sana na Polisi wakitaka aoneshe hati ya kiwanja ilipo kwani aliwanyima.

Je, Tajiri aliwezaje kununua sehemu na kujenga bila ya kuwa na hati?

Je, Kwanini Bodi ya Wadhamni iliundwa haraka bila kufuata kanuni?

Kwanini Polisi Wawashikile watu na kuwanyima dhamana hadi uzio uwekwe?

RITA WALIFIKA KUKAGUA MALI ZETU LAKINI HADI LEO HAWATUPI MREJESHO
View attachment 2359599
Kwanini RITA pamoja na kuja sehemu ya tukio, mbona hawajasitisha ujenzi?

Je kwanini Mkurugenzi alisimamisha ujenzi, lakini baada ya mhusika mkuu kufariki akaruhusu ujenzi uendelee?

Hawa waumini wanatishiwa kubambikizwa kesi ya Ugaidi.

Hapa chini naweka Ushahidi
View attachment 2359543
Hii hapa ni OB ya Polisi waliokamatwa kisa wanazuia Msikiti wao Usibomolewe. Huruma za Polisi ACP Ramadhan Kingai ndo zilifanywa Waachiliwe baada ya kuhoji sababu ya kuwashikilia bila dhamana wala kupelekwa mahakamani. Ni baada ya kuelezwa kilicho nyuma ya pazia.
View attachment 2359556
Hii ni barua iliyowataka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA) na BARAZA Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) kufika mbele ya Mkuu wa Wilaya ili atatue mzozo huu lakini hawajatokea kila Walipoitwa.
View attachment 2359570
View attachment 2359571
Hii ni kibali cha kusimamisha Ujenzi, wiki mbili baada ya alokuwa anatetea Msikiti usibomolewe kufariki, Wakakihuisha
View attachment 2359582View attachment 2359583View attachment 2359581
Na hiii ni hati halali waliyopewaTaasisi ya Mwenge Mosque & Islamic Centre ambayo hadi sasa bado wanayo, ila mtu mwingine kaja kabomoa Msikiti na Kujenga Maduka chini ya Usimamizi wa Polisi. Hawana hata Umiliki.
View attachment 2359584View attachment 2359585
Na huu ni Uthibitisho wa Serikali za Mtaa kutoelewa kunachoendelea mtaani kwake
View attachment 2359588View attachment 2359587
Na haya ndo Maduka yanayojengwa sehemu ulipokuwa Msikiti Mwenge mbele ya Magorofa ya Jeshi barabara ya TRA

Tunaomba Serikali Sikivu ya Mama Samia iingilie Kati swala hili. Bado naamini Godwin Gondwe anao uwezo wa kutatua mgogoro huu japo haoneshi jitihada zozote kuhakikisha hili swala linaisha.

Mkuu wa Mkoa Makalla sababu ni rafiki yake na Sheikh Salum, kila siku anasema yupo busy.
dubu Bodi of trusrees kwanini wasiende mahakamani? Wanaogopa nini kenda Mahakamani? Utapata hai zako bila shda ingawa itachelewa
 
AAh, sheria itafata mkondo wako, si jambo la kustusha sana, Bakwata mbona wameuza viwanja vya wakf kwa Manji siku nyingi sana.

Silioni tatizo, Waislam kama wana hasira wajenge mwengine mzuri zaidi na mkubwa kuliko uliovunjwa.
Sa ingine unakuaga na akili 👏👏
 
Jamaa kaingia mkataba na hao watu wa miaka 15 kujenga maduka kuzunguka msikiti then ndan atajenga msikiti mkubwa wa gorofa. na unajengwa muda huu sambamba na maduka. Atamiliki miaka 15 then anawaachia. Mbona ni kawaida kila mahali inafanyika hivyo.
Bora wangetoa miaka 90.
Sasa kobazi watakua wamekula advance imeisha ndo wanaanza kokoro.
 
Alafu nasikia huyo tajiri kaingia mkataba wa miaka 30 ndio awaachie eneo lenu,dah kweli wajinga ndio waliwao,hivi umeshawahi kusikia kanisa linaingia ubia na muwekezaji kweli?

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Adui wa muislamu ni muislam mwenyewe
Kazi ya bakwata ni kutangaza mwezi muandamo tu ila wamefilisi mali nyingi sana za waislamu
Amkeni mpambane
 
NASHAURI ACHANENI HAO HUO MSIKITI... TAFUTENI MSIKITINI MWINGINE MSWALI... RUDINI CHINI MUMUOMBE ALLAAH MAGHFIRAH... ALAFU WA KUMUOMBA MSAADA NI ALLAAH SIO KIUMBE... HAO VIUMBE MNAOWAOMBA MSAADA HAWANA MSAADA WOWOTE...

ALAFU SIKU NYINGINE... MSIKITI SIO MALI YA WAUMINI... LAZIMA UWE CHINI YA MMILIKI MMOJA... HAKUNA MALI YA WOTE...HIVI HAMJIFUNZI KWA MTU KAMA GWAJIMA AU KAKOBE NA WACHUNGAJI WENGINE WA MAKANISA MBALIMBALI YANAIBUKA... MBONA WAO HAWANA MIGOGORO... ILE NI MALI YAKE MCHUNGAJI... HAO BAKWATA... PALE HAMNA DINI PALE... WALE WALISHAJIKATIA TAMAA NA AKHERA...HUYO ALHAD NI SHEIKH WA KIYAHUDI AMBAYE ALLAAH ALIMTAJA KATIKA SUURAT TAWBA AYA YA 34...Msimwangalie kama mwenzenu huyo.

RUDINI CHINI NYUMA... MRUDIENI MOLA WENU... MUOMBENI MSAMAHA... ALAFU ATAWASAIDIENI...

HAINA HAJA YA VURUGU WALA NINI... WACHA WACHUKUE... MSIKITI KAMA NI WA ALLAAH... ALLAAH MWENYEWE ATAULINDA MSIKITI WAKE... KAMA SIO WA ALLAAH... BASI HILO MLILOPATA NDIO LINAWASTAHIKI...

Mkishindwa nendeni mahakamani... Ila bado nachelea kuamini kuwa mtapata hiyo iitwayo haki...

ALLAAH ATUONGOZE...
 
Adui wa muislamu ni muislam mwenyewe
Kazi ya bakwata ni kutangaza mwezi muandamo tu ila wamefilisi mali nyingi sana za waislamu
Amkeni mpambane
Hilo eneo japo ni la bakwata wale jamaa wa kaptula waliwapindua wazee na wameendesha hapo muda wanakula ela tu
 
NASHAURI ACHANENI HAO HUO MSIKITI... TAFUTENI MSIKITINI MWINGINE MSWALI... RUDINI CHINI MUMUOMBE ALLAAH MAGHFIRAH... ALAFU WA KUMUOMBA MSAADA NI ALLAAH SIO KIUMBE... HAO VIUMBE MNAOWAOMBA MSAADA HAWANA MSAADA WOWOTE...

ALAFU SIKU NYINGINE... MSIKITI SIO MALI YA WAUMINI... LAZIMA UWE CHINI YA MMILIKI MMOJA... HAKUNA MALI YA WOTE...HIVI HAMJIFUNZI KWA MTU KAMA GWAJIMA AU KAKOBE NA WACHUNGAJI WENGINE WA MAKANISA MBALIMBALI YANAIBUKA... MBONA WAO HAWANA MIGOGORO... ILE NI MALI YAKE MCHUNGAJI... HAO BAKWATA... PALE HAMNA DINI PALE... WALE WALISHAJIKATIA TAMAA NA AKHERA...HUYO ALHAD NI SHEIKH WA KIYAHUDI AMBAYE ALLAAH ALIMTAJA KATIKA SUURAT TAWBA AYA YA 34...Msimwangalie kama mwenzenu huyo.

RUDINI CHINI NYUMA... MRUDIENI MOLA WENU... MUOMBENI MSAMAHA... ALAFU ATAWASAIDIENI...

HAINA HAJA YA VURUGU WALA NINI... WACHA WACHUKUE... MSIKITI KAMA NI WA ALLAAH... ALLAAH MWENYEWE ATAULINDA MSIKITI WAKE... KAMA SIO WA ALLAAH... BASI HILO MLILOPATA NDIO LINAWASTAHIKI...

Mkishindwa nendeni mahakamani... Ila bado nachelea kuamini kuwa mtapata hiyo iitwayo haki...

ALLAAH ATUONGOZE...
Ukiona hivyo hakuna tasisi imara wengi wamejaa tamaa na njaa tupu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Salaam,hiyo ni habari ya upande mmoja mkiskia upande wa pili mtawaona hawa walioleta habari hii ni chuki na hasad tu Waislamu wengi hawapendi maendeleo yanayoletwa na watu wengine.
 
Ukweli ni kuwa eneo hilo linajengwa maduka ya kisasa upande wa mbele halafu Msikiti wa kisasa wa ghorofa 4 unajengwa katika eneo la ndani. Yameanza maduka kwakuwa isingekuwa vizuri uanze Msikiti kisha watu wakianza kufanya ibada huku ujenzi wa maduka ungesumbua wanaofanya ibada kwani ibada inahitaji mahala tulivu( rejea kibali alichopost mleta habari kuwa ni kwaajili ya kujenga Msikiti na maduka ya biashara)
 
Wataendaje mahakamani na ushahidi wa kutunga. Huyu kaja kutaka huruma za watu
Ni kweli kabisa, siku zote ukweli utabaki kuwa ukweli ndio maana ameenda ofisi zote wamepuuzwa kwakuwa viongozi waliopo madarakani ni halali na wanafanya maendeleo kubadilisha mambo ya ovyo yaliyokuwa yanarudisha maendeleo nyuma
 
Back
Top Bottom