DOKEZO TAKUKURU Wakamateni Sheikh, Alhad Mussa Salum, RITA, Mkurugenzi, Ardhi na Polisi kwa kuvunja Msikiti wa Mwenge kwa Mabavu

DOKEZO TAKUKURU Wakamateni Sheikh, Alhad Mussa Salum, RITA, Mkurugenzi, Ardhi na Polisi kwa kuvunja Msikiti wa Mwenge kwa Mabavu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mleta mada ni mnufaika wa msikiti kiuchumi na katengeneza document fake. Nenda mahakamani kama ww Kidume. Na hakimu anaifahamu issue yote hii na document zako fake
Anajaribu kuwaongopea watu wasioelewa hii issue , kiongozi usipochaguliwa unatakiwa ukubali matokeo na usapoti viongozi wapya hasa wanapoleta maendeleo ya kweli ambayo wew hukuweza kuleta
 
Jamaa kaingia mkataba na hao watu wa miaka 15 kujenga maduka kuzunguka msikiti then ndan atajenga msikiti mkubwa wa gorofa. na unajengwa muda huu sambamba na maduka. Atamiliki miaka 15 then anawaachia. Mbona ni kawaida kila mahali inafanyika hivyo.
Huyu mleta habari anaongopea uma kwa masilahi yake binafsi, Msikiti umetengewa eneo lake na utajengwa wa ghorofa 4 awamu ya kwanza ni ujenzi wa maduka yanayozunguka eneo la nje( rejea kibali alichopost mleta habari ni kwaajili ya ujenzi wa msikiti na maduka)
 
Salaam Wakuu,

Jamani tunaomba msaada, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum atatutoa roho.

Baada ya rais Samia kuingia Madarakani, wale watu wa pesa inaongea Wamerudi kwa kasi ya ajabu. Mtu mwenye pesa sasa anaweza kufanya chochote na usimfanye kitu.

Katika Mkoa wa Dar Es Salaam kuna Taajiri amewaweka mfukoni Watendaji wote wa Wilaya ya Kinondoni hawa Wakina Gondwe.

Kipindi cha nyumba, kuna Tajiri alitaka kununua Msikiti ili ajenge maduka, Bodi ya Wadhamini ya Msikiti Wakamkatalia. Ikabidi Tajiri huyo amtumie Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ambaye alitetengeneza Bodi mpya ya wadhamni wasio hata waumin wa Msikiti ili Waweze kumuuza Tajiri na Wakafanikiwa. Kumbuka Msikiti unamilikiwa na Taasisi ya Mwenge Mosque & Islamic Centre. Hakuna aliyeshirikishwa kwenye Uteuzi wa Bodi Mpya.

Waumini Walilalamika RITA, Ardhi na kwa Mkurugenzi wa Kinondoni bila mafanikio.
View attachment 2359556
Wakashangaa Hati ya jengo wanayo wao lakini wakashangaa Msikiti unavunjwa na kuanza kujengwa Maduka. Walipojaribu kuzuia, Wakaitwa Polisi wa Oysterbay wakawakamata wote walioonekana kulalamika na kuwekwa ndani bila dhamana. Walikaa sana Polisi kwa kosa la kifanya fujo Msikitini. Aliyekua Msimamizi Mkuu wa Msikiti akafa kifo cha gafla kwani aliteswa sana na Polisi wakitaka aoneshe hati ya kiwanja ilipo kwani aliwanyima.

Je, Tajiri aliwezaje kununua sehemu na kujenga bila ya kuwa na hati?

Je, Kwanini Bodi ya Wadhamni iliundwa haraka bila kufuata kanuni?

Kwanini Polisi Wawashikile watu na kuwanyima dhamana hadi uzio uwekwe?

RITA WALIFIKA KUKAGUA MALI ZETU LAKINI HADI LEO HAWATUPI MREJESHO
View attachment 2359599
Kwanini RITA pamoja na kuja sehemu ya tukio, mbona hawajasitisha ujenzi?

Je kwanini Mkurugenzi alisimamisha ujenzi, lakini baada ya mhusika mkuu kufariki akaruhusu ujenzi uendelee?

Hawa waumini wanatishiwa kubambikizwa kesi ya Ugaidi.

Hapa chini naweka Ushahidi
View attachment 2359543
Hii hapa ni OB ya Polisi waliokamatwa kisa wanazuia Msikiti wao Usibomolewe. Huruma za Polisi ACP Ramadhan Kingai ndo zilifanywa Waachiliwe baada ya kuhoji sababu ya kuwashikilia bila dhamana wala kupelekwa mahakamani. Ni baada ya kuelezwa kilicho nyuma ya pazia.
View attachment 2359556
Hii ni barua iliyowataka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA) na BARAZA Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) kufika mbele ya Mkuu wa Wilaya ili atatue mzozo huu lakini hawajatokea kila Walipoitwa.
View attachment 2359570
View attachment 2359571
Hii ni kibali cha kusimamisha Ujenzi, wiki mbili baada ya alokuwa anatetea Msikiti usibomolewe kufariki, Wakakihuisha
View attachment 2359582View attachment 2359583View attachment 2359581
Na hiii ni hati halali waliyopewaTaasisi ya Mwenge Mosque & Islamic Centre ambayo hadi sasa bado wanayo, ila mtu mwingine kaja kabomoa Msikiti na Kujenga Maduka chini ya Usimamizi wa Polisi. Hawana hata Umiliki.
View attachment 2359584View attachment 2359585
Na huu ni Uthibitisho wa Serikali za Mtaa kutoelewa kunachoendelea mtaani kwake
View attachment 2359588View attachment 2359587
Na haya ndo Maduka yanayojengwa sehemu ulipokuwa Msikiti Mwenge mbele ya Magorofa ya Jeshi barabara ya TRA

Tunaomba Serikali Sikivu ya Mama Samia iingilie Kati swala hili. Bado naamini Godwin Gondwe anao uwezo wa kutatua mgogoro huu japo haoneshi jitihada zozote kuhakikisha hili swala linaisha.

Mkuu wa Mkoa Makalla sababu ni rafiki yake na Sheikh Salum, kila siku anasema yupo busy.
mbona jambo ni simple tu watu wakae kwa week nzima aliliwe tu mungu kwa muda wa week nzima kwa kila aliyehusika iwe polis,rita,hao mashehe,na kila atakahechukua frem hapo limkute jambo then muone kama hawatokuja hapo kuwajengea kabisa msikiti na si kurudisha tena eneo
 
Huyu mleta habari anaongopea uma kwa masilahi yake binafsi, Msikiti umetengewa eneo lake na utajengwa wa ghorofa 4 awamu ya kwanza ni ujenzi wa maduka yanayozunguka eneo la nje( rejea kibali alichopost mleta habari ni kwaajili ya ujenzi wa msikiti na maduka)
Wewe unaona inamake sense kujenga maduka kwanza kabla ya msikiti?
 
Wewe unaona inamake sense kujenga maduka kwanza kabla ya msikiti?
Kuna sababu iliyosababisha yaazwe maduka, wakandarasi wanaojenga ni wawili tofauti Mkandarasi wa Maduka alikuwa yuko tayari wakati Mkandarasi wa Msikiti alikuwa anamalizia ujenzi wa Msikiti mwingine na hawa wote wanatakiwa wafanye kazi kwa kupishana. Ungekuwa wew ungefanyaje?
 
Kama ni kweli wanajenga madula katika kiwanja cha msikiti ni dhulma kubwa sana. Serikali iingilie kati itende haki
Habari hii haina ukweli wowote Serikali iko macho sana halafu mleta habari wala hakutakiwa kuileta huku JF alitakiwa aipeleke TAKUKURU moja kwa moja huku kaileta ham a msaada wowote anatafuta huruma ya watu tu
 
dubu Bodi of trusrees kwanini wasiende mahakamani? Wanaogopa nini kenda Mahakamani? Utapata hai zako bila shda ingawa itachelewa
Hawawezi kwenda mahakamani kwakuwa wanaongea vitu vya uongo kwa masilahi yao ya kidunia, kama ni kweli walitakiwa wapeleke malalamiko TAKUKURU sio kupost JF
 
Alafu nasikia huyo tajiri kaingia mkataba wa miaka 30 ndio awaachie eneo lenu,dah kweli wajinga ndio waliwao,hivi umeshawahi kusikia kanisa linaingia ubia na muwekezaji kweli?

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Miaka 20 iliyoingiwa mkataba ni upande wa uwekezaji wa Maduka upande wa Msikiti hakuna mkataba unajengwa bure na huyo Mwekezaji wa Maduka amejitolea sadaka ya kujenga Msikiti for free na utakuwa chini ya Wanachama wa Mwenge.
 
Alafu nasikia huyo tajiri kaingia mkataba wa miaka 30 ndio awaachie eneo lenu,dah kweli wajinga ndio waliwao,hivi umeshawahi kusikia kanisa linaingia ubia na muwekezaji kweli?

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Miaka 20 iliyoingiwa mkataba ni upande wa uwekezaji wa Maduka upande wa Msikiti hakuna mkataba unajengwa bure na huyo Mwekezaji wa Maduka amejitolea sadaka ya kujenga Msikiti for free na utakuwa chini ya Wanachama wa Mwenge
NASHAURI ACHANENI HAO HUO MSIKITI... TAFUTENI MSIKITINI MWINGINE MSWALI... RUDINI CHINI MUMUOMBE ALLAAH MAGHFIRAH... ALAFU WA KUMUOMBA MSAADA NI ALLAAH SIO KIUMBE... HAO VIUMBE MNAOWAOMBA MSAADA HAWANA MSAADA WOWOTE...

ALAFU SIKU NYINGINE... MSIKITI SIO MALI YA WAUMINI... LAZIMA UWE CHINI YA MMILIKI MMOJA... HAKUNA MALI YA WOTE...HIVI HAMJIFUNZI KWA MTU KAMA GWAJIMA AU KAKOBE NA WACHUNGAJI WENGINE WA MAKANISA MBALIMBALI YANAIBUKA... MBONA WAO HAWANA MIGOGORO... ILE NI MALI YAKE MCHUNGAJI... HAO BAKWATA... PALE HAMNA DINI PALE... WALE WALISHAJIKATIA TAMAA NA AKHERA...HUYO ALHAD NI SHEIKH WA KIYAHUDI AMBAYE ALLAAH ALIMTAJA KATIKA SUURAT TAWBA AYA YA 34...Msimwangalie kama mwenzenu huyo.

RUDINI CHINI NYUMA... MRUDIENI MOLA WENU... MUOMBENI MSAMAHA... ALAFU ATAWASAIDIENI...

HAINA HAJA YA VURUGU WALA NINI... WACHA WACHUKUE... MSIKITI KAMA NI WA ALLAAH... ALLAAH MWENYEWE ATAULINDA MSIKITI WAKE... KAMA SIO WA ALLAAH... BASI HILO MLILOPATA NDIO LINAWASTAHIKI...

Mkishindwa nendeni mahakamani... Ila bado nachelea kuamini kuwa mtapata hiyo iitwayo haki...

ALLAAH ATUONGOZE...
Waleta habari ni viongozi waliopigwa chini kwenye uongozi kwakuwa walikuwa hawaleti maendeleo Msikiti ulikuwa dhalili leo viongozi waliochaguliwa wamekuja na mawazo mapya ya kuuendeleza uislamu Mwenge wanapigwa maneno. Kama wana hoja za msingi wapeleke hili jambo TAKUKURU AU Mahakamani sio kulileta JF kutaka huruma ya watu wasiokuwa na taarifa za upande wa pili
 
Kuna sababu iliyosababisha yaazwe maduka, wakandarasi wanaojenga ni wawili tofauti Mkandarasi wa Maduka alikuwa yuko tayari wakati Mkandarasi wa Msikiti alikuwa anamalizia ujenzi wa Msikiti mwingine na hawa wote wanatakiwa wafanye kazi kwa kupishana. Ungekuwa wew ungefanyaje?
Lakin pia kutoka hapo ujenz ulipo mita 200 kuna msikiti mwingine so kama ni ibada kama kawaida.
 
Kuweni wakakamavu mpaka hilo jengo livunjwe au mupewe nyinyi.Huu utakuwa ni uhuni kwamba mtu asiye na hatia anaweza kufanya jambo kama hilo.Itaondoa dhana ya utawala wa kisheria.
 
Miaka 20 iliyoingiwa mkataba ni upande wa uwekezaji wa Maduka upande wa Msikiti hakuna mkataba unajengwa bure na huyo Mwekezaji wa Maduka amejitolea sadaka ya kujenga Msikiti for free na utakuwa chini ya Wanachama wa Mwenge

Waleta habari ni viongozi waliopigwa chini kwenye uongozi kwakuwa walikuwa hawaleti maendeleo Msikiti ulikuwa dhalili leo viongozi waliochaguliwa wamekuja na mawazo mapya ya kuuendeleza uislamu Mwenge wanapigwa maneno. Kama wana hoja za msingi wapeleke hili jambo TAKUKURU AU Mahakamani sio kulileta JF kutaka huruma ya watu wasiokuwa na taarifa za upande wa pili
Tusizunumzie maendeleo kabla kupata ufatanuzi wa hati.ikiwa wanaotaka maendeleo hawana hati maendeleo yao ni feki na hayatakuwa kwa maslahi ya uislamu.
 
HV kwanin huyu shehe azingolewe ktk nafsi hyo kwani kuwa shek mkuu wa mkoa Ni mkataba wa muda gani mnk naoan analalmikiwa sna na muft mkuu ataki kumngoaa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Tusizunumzie maendeleo kabla kupata ufatanuzi wa hati.ikiwa wanaotaka maendeleo hawana hati maendeleo yao ni feki na hayatakuwa kwa maslahi ya uislamu.
Uongozi ulioondolewa madarakani uligoma kukabidhi vitendea kazi ikiwamo hati, Viongozi waliochaguliwa wakaenda kuifuta hati na kuprocess hati mpya ipo na ndio imetumika kuombea vibali
 
Hawa waleta taarifa ni waongo, kwanini wanaogopa kulipeleka hili jambo TAKUKURU wawasaidie wanalileta huku????
Sasa wewe umeshaambiwa kuna watu wana mkono mrefu hadi kufikia hatua ya kusingizia kuwabambikizia watu kesi ya Ugaidi. Unafikiri kitu cha mchezo hicho?

Ndiyo maana wamelileta hilo suala kwa wananchi ili nguvu ya umma iweke shinikizo na Haki itendeke kwa pande zote mbili!
 
Back
Top Bottom