DOKEZO TAKUKURU Wakamateni Sheikh, Alhad Mussa Salum, RITA, Mkurugenzi, Ardhi na Polisi kwa kuvunja Msikiti wa Mwenge kwa Mabavu

DOKEZO TAKUKURU Wakamateni Sheikh, Alhad Mussa Salum, RITA, Mkurugenzi, Ardhi na Polisi kwa kuvunja Msikiti wa Mwenge kwa Mabavu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Uongozi ulioondolewa madarakani uligoma kukabidhi vitendea kazi ikiwamo hati, Viongozi waliochaguliwa wakaenda kuifuta hati na kuprocess hati mpya ipo na ndio imetumika kuombea vibali
Jee huo utaratibu umo katika sheria kuwa mtu akigoma kutoa hati yake unakwenda kutenngeneza nyengine.Na nani anayekupa hiyo nyingine kabla kufutwa ya mwanzo.Ingekuwa ni hivyo majambazi wakitaka nyumba eneo fulani ukigoma kuwapa wanakwenda kutengeneza nyengine halafu unahamishwa.Ikiwa hilo lipo basi kuna kasoro kubwa na sheria ya ardhi lazima ibadilishwe isitoe mwanya kwa utovu wa nidhamu namna hiyo.
 
Hivi waislamu kumbe tukionewa au mkionewa, wakionewa na wenzeo mambo ni simple kiasi hiki, yaani mnalia na kuandika Kwa huruma na kiasi hiki. Mtonyo umeingia huo mfumo ni wenu na wetu tuendelee kuyaishi machungu. Timiza wajibu kama raia mnaonewa na kuteswa hio mimi siwezi na haitatokea, wasiponiua basi nikitoka naondoka na kijiji chote, hata Hamza yumkini kalikuwepo kasababishi, Dhuluma mwiko mwiko mwiko. Yeye atakaye moto afanye Dhuluma
 
ninamaswali machache ,tafadhali njoo na majibu Ili tupate mwanga.

1:Mbona kwa mjibu wa Hilo Bango kinacho Jengwa ni Msikiti, na kituo kisicho julikana kitashughulika nanini.
Tajiri hapo Yuko wapi?

2:Mwenye kujenga (kujengewa)ni baraza la wadhamini wa Msikiti.
shida Ipo kwa kinacho Jengwa au wanao simamia ujenzi?

3:Imam wa Msikiti Yuko upande gani anaungana na wajenzi au upande wanao Pinga?
 
Pambaneni mpaka kieleweke! Uzuri nyie vita mnaiweza! Si mna ile kaulimbiu kwamba “hakuna kumuachia mungu ni jino kwa jino?!”...haya komaeni sasa
Kuna mambo matatu kwenye uonevu wapaswa kuchagua mojawapo.

1:Kudhuwia uonevu kwa mkono.
2:kukemea uonevu
3: kusikitika tu

Kati kahayo (3)wapaswa kuchagua mojawapo japo namba Tatu ni dhaifu lakini Kuna mda inachukua nafasi Kutokana na mazingira.
 
Salaam Wakuu,

Jamani tunaomba msaada, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum atatutoa roho.

Baada ya rais Samia kuingia Madarakani, wale watu wa pesa inaongea Wamerudi kwa kasi ya ajabu. Mtu mwenye pesa sasa anaweza kufanya chochote na usimfanye kitu.

Katika Mkoa wa Dar Es Salaam kuna Taajiri amewaweka mfukoni Watendaji wote wa Wilaya ya Kinondoni hawa Wakina Gondwe.

Kipindi cha nyumba, kuna Tajiri alitaka kununua Msikiti ili ajenge maduka, Bodi ya Wadhamini ya Msikiti Wakamkatalia. Ikabidi Tajiri huyo amtumie Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ambaye alitetengeneza Bodi mpya ya wadhamni wasio hata waumin wa Msikiti ili Waweze kumuuza Tajiri na Wakafanikiwa. Kumbuka Msikiti unamilikiwa na Taasisi ya Mwenge Mosque & Islamic Centre. Hakuna aliyeshirikishwa kwenye Uteuzi wa Bodi Mpya.

Waumini Walilalamika RITA, Ardhi na kwa Mkurugenzi wa Kinondoni bila mafanikio.
View attachment 2359556
Wakashangaa Hati ya jengo wanayo wao lakini wakashangaa Msikiti unavunjwa na kuanza kujengwa Maduka. Walipojaribu kuzuia, Wakaitwa Polisi wa Oysterbay wakawakamata wote walioonekana kulalamika na kuwekwa ndani bila dhamana. Walikaa sana Polisi kwa kosa la kifanya fujo Msikitini. Aliyekua Msimamizi Mkuu wa Msikiti akafa kifo cha gafla kwani aliteswa sana na Polisi wakitaka aoneshe hati ya kiwanja ilipo kwani aliwanyima.

Je, Tajiri aliwezaje kununua sehemu na kujenga bila ya kuwa na hati?

Je, Kwanini Bodi ya Wadhamni iliundwa haraka bila kufuata kanuni?

Kwanini Polisi Wawashikile watu na kuwanyima dhamana hadi uzio uwekwe?

RITA WALIFIKA KUKAGUA MALI ZETU LAKINI HADI LEO HAWATUPI MREJESHO
View attachment 2359599
Kwanini RITA pamoja na kuja sehemu ya tukio, mbona hawajasitisha ujenzi?

Je kwanini Mkurugenzi alisimamisha ujenzi, lakini baada ya mhusika mkuu kufariki akaruhusu ujenzi uendelee?

Hawa waumini wanatishiwa kubambikizwa kesi ya Ugaidi.

Hapa chini naweka Ushahidi
View attachment 2359543
Hii hapa ni OB ya Polisi waliokamatwa kisa wanazuia Msikiti wao Usibomolewe. Huruma za Polisi ACP Ramadhan Kingai ndo zilifanywa Waachiliwe baada ya kuhoji sababu ya kuwashikilia bila dhamana wala kupelekwa mahakamani. Ni baada ya kuelezwa kilicho nyuma ya pazia.
View attachment 2359556
Hii ni barua iliyowataka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA) na BARAZA Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) kufika mbele ya Mkuu wa Wilaya ili atatue mzozo huu lakini hawajatokea kila Walipoitwa.
View attachment 2359570
View attachment 2359571
Hii ni kibali cha kusimamisha Ujenzi, wiki mbili baada ya alokuwa anatetea Msikiti usibomolewe kufariki, Wakakihuisha
View attachment 2359582View attachment 2359583View attachment 2359581
Na hiii ni hati halali waliyopewaTaasisi ya Mwenge Mosque & Islamic Centre ambayo hadi sasa bado wanayo, ila mtu mwingine kaja kabomoa Msikiti na Kujenga Maduka chini ya Usimamizi wa Polisi. Hawana hata Umiliki.
View attachment 2359584View attachment 2359585
Na huu ni Uthibitisho wa Serikali za Mtaa kutoelewa kunachoendelea mtaani kwake
View attachment 2359588View attachment 2359587
Na haya ndo Maduka yanayojengwa sehemu ulipokuwa Msikiti Mwenge mbele ya Magorofa ya Jeshi barabara ya TRA

Tunaomba Serikali Sikivu ya Mama Samia iingilie Kati swala hili. Bado naamini Godwin Gondwe anao uwezo wa kutatua mgogoro huu japo haoneshi jitihada zozote kuhakikisha hili swala linaisha.

Mkuu wa Mkoa Makalla sababu ni rafiki yake na Sheikh Salum, kila siku anasema yupo busy.
Ile msikiti ni amali iliyo chini ya jumuiya ya Waislam wa Mwenge. Ninaufahamu. Sasa hili la kuubomoa wakati wenye msikiti hawajaridhia ndo tunarudi kule kule kwenye kudhulumu amali za waislam.

FaizaFoxy angalieni hizi mambo zisije kuleta mtafafuku zaidi
 
Tafuteni mawakili wasomi mwende mahakamani, wallah mtashinda kesi, shida yenu mu wabahili mnaficha hela na mnapenda mtelemko, wapeni hela mawakili wasomi muone moto wao
 
Habari hii haina ukweli wowote Serikali iko macho sana halafu mleta habari wala hakutakiwa kuileta huku JF alitakiwa aipeleke TAKUKURU moja kwa moja huku kaileta ham a msaada wowote anatafuta huruma ya watu tu
Hujaona faida za hii mada ,kuletwa hapa?
 
Waleta habari ni viongozi waliopigwa chini kwenye uongozi kwakuwa walikuwa hawaleti maendeleo Msikiti ulikuwa dhalili leo viongozi waliochaguliwa wamekuja na mawazo mapya ya kuuendeleza uislamu Mwenge wanapigwa maneno. Kama wana hoja za msingi wapeleke hili jambo TAKUKURU AU Mahakamani sio kulileta JF kutaka huruma ya watu wasiokuwa na taarifa za upande wa pili[/QUOTE]

Hayo maendeleo ni kwa faida yanani?

Nakubaliana na wewe " Msikiti ulikua dhalili" je mmekubaliana kuhusu hayo maendeleo?
Je baada ya hayo maduka kujengwa nafasi inayo Baki inaacha sehem ya Msikiti na uwanja kwa shughuli za mikusanyiko Mikubwa?
 
Nyie siyo Waislamu nao wajua!! ....kwanza wakikuangaia tuu hivi unaufyata mwenyewe......wale walio zuia kufanya Biashara ya kuuza Mahiti palee Ilala! na kweli serikali ikaufayata leo hii wamekwenda wapi??...

Makaburi ya waislamu yapo hapo mpaka leo ya sasa hivi! barabara ile ilipindishwa kwa nguvu hai za waislamu, yaani wale usiwachezee wangeenda kumbeba Mama Samia mzima mzima na kumpeleka pale!

Eti imamu aliye na Hati kafariki mweee!! Waislamu nao wajua mie???? No Mleta Mada umekosea njia, sema ukweli wako!! Waislamu siyo kitu cha mchezo!mchezo wewe!!! wale wako tayari kufa! waende Mbinguni!

Lkn Msikiti ubaki salama ndivo walivyo!!......kristo ya vatican inawajua, sikia sasa nakupa ushauri huu......'''Ukome kudai Mali zenu za Kanisa kwa kutumia Jina la Waislamu watukufu'''!! unasikia???

siku nyingine utatumiwa majini kiuno saba!! ....UOne fire!.......Mzee yfusufu yuko wapi???
 
Ukweli ni kuwa eneo hilo linajengwa maduka ya kisasa upande wa mbele halafu Msikiti wa kisasa wa ghorofa 4 unajengwa katika eneo la ndani. Yameanza maduka kwakuwa isingekuwa vizuri uanze Msikiti kisha watu wakianza kufanya ibada huku ujenzi wa maduka ungesumbua wanaofanya ibada kwani ibada inahitaji mahala tulivu( rejea kibali alichopost mleta habari kuwa ni kwaajili ya kujenga Msikiti na maduka ya biashara)
Hilo suala la kufanya biashara misikitini ni jambo limekatazwa na sheria ya kiislaam... MSIKITI KAZI YAKE SI BIASHARA... NA NDIO MAANA ALLAAH ANANYIMA BARAKA KWENYE HIYO MISIKITI NDIO MWISHO WA SIKU MNAISHIA KWENYE MIGOGORO ISIYOISHA...
 
Waleta habari ni viongozi waliopigwa chini kwenye uongozi kwakuwa walikuwa hawaleti maendeleo Msikiti ulikuwa dhalili leo viongozi waliochaguliwa wamekuja na mawazo mapya ya kuuendeleza uislamu Mwenge wanapigwa maneno. Kama wana hoja za msingi wapeleke hili jambo TAKUKURU AU Mahakamani sio kulileta JF kutaka huruma ya watu wasiokuwa na taarifa za upande wa pili

Hayo maendeleo ni kwa faida yanani?

Nakubaliana na wewe " Msikiti ulikua dhalili" je mmekubaliana kuhusu hayo maendeleo?
Je baada ya hayo maduka kujengwa nafasi inayo Baki inaacha sehem ya Msikiti na uwanja kwa shughuli za mikusanyiko Mikubwa?
[/QUOTE]
Maendeleo ni kwa faida ya uislam na kwa faida ya wanachama wanaomiliki msikiti huo.

Wanachama wote wa chama cha ushirika Mwenge wamekubaliana kufanya maendeleo hayo katika vikao rasmi , hao wapingaji nikujuze tu sio wanachama ndio maana wanaogopa kulipeleka hili jambo kwenye mamlaka zinazohusika

Maduka yanajengwa, Msikiti unajengwa wa ghorofa wenye uwezo wa kuchukua watu kuanzia 700 kuendelea na sehemu ya wazi imetengwa kwaajili ya parking na shughuli za hadhara
 
Hilo suala la kufanya biashara misikitini ni jambo limekatazwa na sheria ya kiislaam... MSIKITI KAZI YAKE SI BIASHARA... NA NDIO MAANA ALLAAH ANANYIMA BARAKA KWENYE HIYO MISIKITI NDIO MWISHO WA SIKU MNAISHIA KWENYE MIGOGORO ISIYOISHA...
Misikiti imeanzisha utaratibu wa kutengeneza maduka katika uzio ili angalau zipatikane fedha za uendeshaji wa misikiti kwakuwa kiukweli tabia ya utoaji sadaka kwa Waislamu hairidhishi tofauti na wenzetu wa dini nyingine wamejengewa tabia ya kutoa sadaka na zaka ambazo sadaka zinatumika kufinance mambo ya dini kama kulipa mishahara na kununua vitendea kazi.

Wewe mara ya mwisho umetoa Zaka lini AbuuMaryam?
 
Inna liLlahi wainna Ilaihi Rrajiuun.. Mungu atawalipa InshaAllah
 
Hayo maendeleo ni kwa faida yanani?

Nakubaliana na wewe " Msikiti ulikua dhalili" je mmekubaliana kuhusu hayo maendeleo?
Je baada ya hayo maduka kujengwa nafasi inayo Baki inaacha sehem ya Msikiti na uwanja kwa shughuli za mikusanyiko Mikubwa?
Maendeleo ni kwa faida ya uislam na kwa faida ya wanachama wanaomiliki msikiti huo.

Wanachama wote wa chama cha ushirika Mwenge wamekubaliana kufanya maendeleo hayo katika vikao rasmi , hao wapingaji nikujuze tu sio wanachama ndio maana wanaogopa kulipeleka hili jambo kwenye mamlaka zinazohusika

Maduka yanajengwa, Msikiti unajengwa wa ghorofa wenye uwezo wa kuchukua watu kuanzia 700 kuendelea na sehemu ya wazi imetengwa kwaajili ya parking na shughuli za hadhara
[/QUOTE]

Kama usemavyo ndivyo, basi ni jambo la kheli, lakini napata mashaka kwanini ujenzi ,utangulie wa maduka kabla ya Msikiti wenyewe?

Mahitaji hapo ni Msikiti , frem ni kwa maendeleo ya Msikiti, Leo zinatangulizwa frem kabla ya Msikiti hili naro haliko sawa.

Swala lakusema kua walalamikali sio sehemu ya members wa ushirika wa Mwenge Bado linaitaji ufafanuzi.
 
tumuombe dk mwaka aachie zzile video alizosema, pengine shkh atarudi nyuma kdg
 
Miaka 20 iliyoingiwa mkataba ni upande wa uwekezaji wa Maduka upande wa Msikiti hakuna mkataba unajengwa bure na huyo Mwekezaji wa Maduka amejitolea sadaka ya kujenga Msikiti for free na utakuwa chini ya Wanachama wa Mwenge.
Ndio maana yule Mzee semtumbi aliekuwa kang'ang'ania hati kuna muda alikuwa anauliza nini bodi isikope yenyewe ikajenga hayo maduka,alafu yakawa yanalipa hilo deni?hivi unajua pale kwa yale maduka tu kwa mwaka tu sidhan kama walikuwa wanakosa mil 100.na wewe kama ndio kati ya wale wanabodi,hivi mnadhani mngeshindwa kukopa hela na mkajenga wenyewe hayo maduka,kuliko kumpa mtu mkataba wa miaka 30 kweli?

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Na haya ndo Maduka yanayojengwa sehemu ulipokuwa Msikiti Mwenge mbele ya Magorofa ya Jeshi barabara ya TRA

Inawezekana kuna sababu za kimazingira, yaani shughuli za kiimani zinaweza kuingilia usingizi wa mlinzi wa taifa ambaye anahitaji usingizi wa kutosha.

Kuna vitu vingine kabla ya kujenga inatakiwa kuangalia mazingira siyo kila sehemu tunaweza kujenga kitu chochote bila kuangalia kwanza masuala mtambuka. Je kiwanja hicho madhumuni yake yalikuwa fremu na maduka, hivyo kubadilisha iwe shule ya chekechea au nyumba ya ibada n.k kunahitajika mchakato mpya hata kama unamiliki kwa hati halali kiwanja husika.

Nchi zilizo na mipango miji, ujenzi wa aina yoyote mbali na kuomba vibali husika lakini inabidi ofisi hizo za serikali husika kuwapa barua wakaazi wa jirani kujua kuwa kuna ujenzi wa aina fulani unaombewa kibali na kama kuna pingamizi lolote lenye mashiko basi wawasilishe pingamizi kwa mamlaka husika.


Inawezekana mamlaka husika walipelekewa pingamizi au hoja zenye mashiko na kwa vile wanajua vitaleta maneno makubwa wakaamua kumtumia Sheikh wa Mkoa kumaliza mtafaruku huo kimya kimya.

WaTanzania tujifunze kwanza kuangalia mazingira na kuomba vibali ofisi husika zenye mamlaka pia kuwajali wale tuliowakuta wapo pale mwanzo kama wanapingamizi lolote liwe la kimazingira au kijamii kama vile eneo hili la Mwenge lililopo jirani na maghorofa ya jeshi ambao huwa usingizi na utulivu ni mojawapo wa jambo kubwa wanalolizingatia ila waweze kuamka wakiwa hawana uchovu kwenda ktk shughuli za ulinzi wa taifa.

Ontario, Canada



More Info:
In addition to the planning approvals and building permit which are required for a building project, other permits and approvals may be required in particular circumstances, for example, Ontario Heritage Act, Conservation Authority and Ministry of Transportation approvals. These approvals are considered applicable law. Generally, the applicable laws, which are set out in the Building Code, must be complied with prior to the building permit being issued. READ MORE : Building permits | Citizen’s guide to land use planning.
 
Back
Top Bottom