TAKUKURU yaagiza milango 83 ya kituo kipya cha Afya kuondolewa kutokana na kukosa ubora uliohitajika

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa wilayani Hanang mkoa wa Manyara imemuamuru Mzabuni Ayubu Iyaka aliyepewa kazi ya kutengeneza na kupachika milango kwenye jengo la kituo cha Afya cha Hirbadaw, kuondoa milango yote 83 aliyoweka kwenye kituo hicho baada ya kubainika haina Ubora.

Takukuru imebaini hayo baada ya maafisa wake kufanya ukaguzi kwenye kituo hicho ambapo aliingia mkataba na Halmashauri hiyo kutengeneza na kupachika milango 83 yenye ubora iliyotengenezwa kwa kutumia mbao ngumu kwa gharama ya shilingi Milioni 28,000,000.

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Holle Makungu Septemba 24,2020, amesema wamejiridhisha kuwa kwa makusudi Mzabuni huyo aliamua kukiuka mkataba akatengeneza na kuweka kwenye jengo hilo la Kituo cha Afya milango hiyo isiyokuwa na ubora.

Pamoja na hayo amesema Halmashauri ilishamlipa shilingi Milioni 14,000,000 ambazo ni nusu ya fedha walizoingia mkataba.

Makungu amesema milango hiyo ambayo inadaiwa kuwa ni mipya, imeonekana ikiwa imepasuka,mingine imepinda na kuvunjika kabla ya kituo kuanza kutumika.

Amesema kufuatia hayo Takukuru wilayani Hanang, imemuamuru Mzabuni huyo kuondoa milango yote 83 na kutengeneza mingine yenye ubora unaokubalika katika majengo ya serikali na kwa mujibu wa mkataba alioingia na Halmashauri, na kwamba ataruhusiwa kuweka milango hiyo baada ya kukaguliwa na kujiridhisha kama ubora wake umekidhi vigezo.

Takukuru imewaasa Wazabuni wanaopenda kufanya kazi na serikali kuwa waadilifu na kuzingatia mikataba ya kazi, huku ikitoa rai kwa watumishi wa Umma waliopewa dhamana ya kusimamia miradi ya Umma kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha miradi inatekelezwa katika ubora unaokubalika.
 
Dah hii hatari yan mlango mmoja 337,000/=hakuna kazi apo na fremu je ukiskia mbuzi kala goat ndo uko.
 
Watu Wameteengeneza mlango mmoja kwa 450,000
Mbao mkongo

Ova
Kwa bei ya 337,000 sio sawa mninga, mkola na mkongo sijui kwa maana mbao ngumu ikizid sana 230, 000 kwa bei ya Serikali kwa watu binafsi inacheza 150,000 mpaka 200,000 so kwa mazingira hayo hapo kuna shida fulani
 
Kuna shida mahali
Mkuu
Ona bei ya Hawa jamaa mm Nishawahi kununuaga
Milango kwao maana si kutaka stress na mafundi
Jamaa wa mirango wako keko

Ova
View attachment 1580388
20200704_121740.jpg
 
Kwa bei ya 337,000 sio sawa mninga, mkola na mkongo sijui kwa maana mbao ngumu ikizid sana 230, 000 kwa bei ya Serikali kwa watu binafsi inacheza 150,000 mpaka 200,000 so kwa mazingira hayo hapo kuna shida fulani
Nishanunuaga mwenyewe mbao ngumu mkongo
Mbao moja waliniuzia kwa 87000 mkongo
Nlichukua pisi kadhaa ilitengeneze milango 5
Mlango mmoja ulinigarimu 450,000 hyo mpaka finishing yake mpaka polish etc
Chini ya hapo huwez kupata mbao ngumu utauziwa au kuwekewa mbao iliyopigwa rangi tu
Kwa waliyofanya ujenzi wanaelewa
Sasa hyo milango wanayosema wao Labda size zake ni vidogo

Ova
 
Apo bado wadau wa manispaa waliokupa tenda watataka uwape milion kadhaa dah mm siwezi mkuu kwa kazi iyo.
Tatizo Kuna watu wanataka hel hapo hapo
Kwenye Kazi na yule aliyepewa tenda kwa style hyo
Hawez weka kitu kinachotakiwa lazima ataweka mbao tofauti

Ova
 
Nishanunuaga mwenyewe mbao ngumu mkongo
Mbao moja waliniuzia kwa 87000 mkongo
Nlichukua pisi kadhaa ilitengeneze milango 5
Mlango mmoja ulinigarimu 450,000 hyo mpaka finishing yake mpaka polish etc
Chini ya hapo huwez kupata mbao ngumu utauziwa au kuwekewa mbao iliyopigwa rangi tu
Kwa waliyofanya ujenzi wanaelewa
Sasa hyo milango wanayosema wao Labda size zake ni vidogo

Ova
Apo sahihi mlango wa mninga au mkongo minimum ni 450,000/=na sometimes mpaka laki 5 hadi tano na nusu pure panel door sasa kwa milango ya hospital tena taaisisi ya afya huwezi weka size ndogo kumbuka kuna dharura na vile vile utumiaji mbovu wa baadhi ya wateja au watumishi.
 
sijui milioni 28 nyingine anaitoa wapi?!wizi haufai
 
Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa wilayani Hanang mkoa wa Manyara imemuamuru Mzabuni Ayubu Iyaka aliyepewa kazi ya kutengeneza na kupachika milango kwenye jengo la kituo cha Afya cha Hirbadaw, kuondoa milango yote 83 aliyoweka kwenye kituo hicho baada ya kubainika haina Ubora.

Takukuru imebaini hayo baada ya maafisa wake kufanya ukaguzi kwenye kituo hicho ambapo aliingia mkataba na Halmashauri hiyo kutengeneza na kupachika milango 83 yenye ubora iliyotengenezwa kwa kutumia mbao ngumu kwa gharama ya shilingi Milioni 28,000,000.

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Holle Makungu Septemba 24,2020, amesema wamejiridhisha kuwa kwa makusudi Mzabuni huyo aliamua kukiuka mkataba akatengeneza na kuweka kwenye jengo hilo la Kituo cha Afya milango hiyo isiyokuwa na ubora.

Pamoja na hayo amesema Halmashauri ilishamlipa shilingi Milioni 14,000,000 ambazo ni nusu ya fedha walizoingia mkataba.

Makungu amesema milango hiyo ambayo inadaiwa kuwa ni mipya, imeonekana ikiwa imepasuka,mingine imepinda na kuvunjika kabla ya kituo kuanza kutumika.

Amesema kufuatia hayo Takukuru wilayani Hanang, imemuamuru Mzabuni huyo kuondoa milango yote 83 na kutengeneza mingine yenye ubora unaokubalika katika majengo ya serikali na kwa mujibu wa mkataba alioingia na Halmashauri, na kwamba ataruhusiwa kuweka milango hiyo baada ya kukaguliwa na kujiridhisha kama ubora wake umekidhi vigezo.

Takukuru imewaasa Wazabuni wanaopenda kufanya kazi na serikali kuwa waadilifu na kuzingatia mikataba ya kazi, huku ikitoa rai kwa watumishi wa Umma waliopewa dhamana ya kusimamia miradi ya Umma kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha miradi inatekelezwa katika ubora unaokubalika.
Imewekwa na Wana ccm na wamekula 10%
 
Apo sahihi mlango wa mninga au mkongo minimum ni 450,000/=na sometimes mpaka laki 5 hadi tano na nusu pure panel door sasa kwa milango ya hospital tena taaisisi ya afya huwezi weka size ndogo kumbuka kuna dharura na vile vile utumiaji mbovu wa baadhi ya wateja au watumishi.
Si ndy hapo.... Hapo eidha jamaa kakatwa Hela za kazi Ndomana Labda kawawekea flash doors etc
Maana bajeti ishavamiwa na walafi

Ova
 
Back
Top Bottom