TAKUKURU yaagiza milango 83 ya kituo kipya cha Afya kuondolewa kutokana na kukosa ubora uliohitajika

Acha akipate.Ni nani aliyemwambia ku tender bei ndogo ili tu ashinde zabuni!
Nishanunuaga mwenyewe mbao ngumu mkongo
Mbao moja waliniuzia kwa 87000 mkongo
Nlichukua pisi kadhaa ilitengeneze milango 5
Mlango mmoja ulinigarimu 450,000 hyo mpaka finishing yake mpaka polish etc
Chini ya hapo huwez kupata mbao ngumu utauziwa au kuwekewa mbao iliyopigwa rangi tu
Kwa waliyofanya ujenzi wanaelewa
Sasa hyo milango wanayosema wao Labda size zake ni vidogo

Ova
 
Hii bei waliyoweka hapo (Tshs 28,000,000/) ni ya milango ya mbao za mti wa Mtundu kwa Mninga milango 83 ingegharimu Tshs 40,000,000/ almost
 
Kwa bei ya 337,000 sio sawa mninga, mkola na mkongo sijui kwa maana mbao ngumu ikizid sana 230, 000 kwa bei ya Serikali kwa watu binafsi inacheza 150,000 mpaka 200,000 so kwa mazingira hayo hapo kuna shida fulani
Wapi naweza pata kwa bei hiyo Boss?
 
Nakazia hapa!!
Usiangalie rushwa katika small circle, iangalie katika mapana yake. Value for money inahusika na rushwa. Pale unapotengeneza kitu kisichoendana na thamani au ubora uliokusudiwa inategemea ni nini kama sio mazingira yabrushwa na ubadhilifu. Kuna mtandao hapo unakuwa umejipanga
 
Nakubaliana na wewe 100%.Nilitarajia wafatilie kama kuna mgawo ulitembea hadi mzabuni kuweza kuweka miliango isiyo ubora,bila kizuizi chochote.
 
Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa wilayani Hanang mkoa wa Manyara imemuamuru Mzabuni Ayubu Iyaka aliyepewa kazi ya kutengeneza na kupachika milango kwenye jengo la kituo cha Afya cha Hirbadaw, kuondoa milango yote 83 aliyoweka kwenye kituo hicho baada ya kubainika haina Ubora.

Takukuru imebaini hayo baada ya maafisa wake kufanya ukaguzi kwenye kituo hicho ambapo aliingia mkataba na Halmashauri hiyo kutengeneza na kupachika milango 83 yenye ubora iliyotengenezwa kwa kutumia mbao ngumu kwa gharama ya shilingi Milioni 28,000,000.

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Holle Makungu Septemba 24,2020, amesema wamejiridhisha kuwa kwa makusudi Mzabuni huyo aliamua kukiuka mkataba akatengeneza na kuweka kwenye jengo hilo la Kituo cha Afya milango hiyo isiyokuwa na ubora.

Pamoja na hayo amesema Halmashauri ilishamlipa shilingi Milioni 14,000,000 ambazo ni nusu ya fedha walizoingia mkataba.

Makungu amesema milango hiyo ambayo inadaiwa kuwa ni mipya, imeonekana ikiwa imepasuka,mingine imepinda na kuvunjika kabla ya kituo kuanza kutumika.

Amesema kufuatia hayo Takukuru wilayani Hanang, imemuamuru Mzabuni huyo kuondoa milango yote 83 na kutengeneza mingine yenye ubora unaokubalika katika majengo ya serikali na kwa mujibu wa mkataba alioingia na Halmashauri, na kwamba ataruhusiwa kuweka milango hiyo baada ya kukaguliwa na kujiridhisha kama ubora wake umekidhi vigezo.

Takukuru imewaasa Wazabuni wanaopenda kufanya kazi na serikali kuwa waadilifu na kuzingatia mikataba ya kazi, huku ikitoa rai kwa watumishi wa Umma waliopewa dhamana ya kusimamia miradi ya Umma kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha miradi inatekelezwa katika ubora unaokubalika.
Duh TAKUKURU wanafanya kazi za uhandisi siku hizi! Wanaweza kunijengea nyumba yangu niwape tenda?
 
Aiyetakiwa kuwajibishwa ni Afisa manunuzi na "Inspection Team" yake. Wote hao wamekula rushwa. Pia "Advance Payment" huwa ni "discouraged" sana katika manunuzi ya Serikalini. Walitumia kigezo gani, yeye, Bosi wake, na Mhasibu?
 
T
Nishanunuaga mwenyewe mbao ngumu mkongo
Mbao moja waliniuzia kwa 87000 mkongo
Nlichukua pisi kadhaa ilitengeneze milango 5
Mlango mmoja ulinigarimu 450,000 hyo mpaka finishing yake mpaka polish etc
Chini ya hapo huwez kupata mbao ngumu utauziwa au kuwekewa mbao iliyopigwa rangi tu
Kwa waliyofanya ujenzi wanaelewa
Sasa hyo milango wanayosema wao Labda size zake ni vidogo

Ova
Tender huwa ni hiari, ila usidanganye bei na material, matokeo yake ndiyo hayo
 
Kufanya hizi kazi mnaita za force acc ni ujinga mtupu maana tenda bei chini kila mtu msimamizi anataka akutoe hela yaani Kuna lundo la maafisa wasimamizi kuanzia wanakamati Hadi wauguzi
 
Back
Top Bottom