TAKUKURU yaingilia kati sakata la Makonda na GSM. GSM aliripoti hati ya kiwanja kupotea

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Serikali imesema inalichunguza sakata la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed (GSM) la kugombea kiwanja Na.60 kilichopo Regent Estate Manispaa ya Kinondoni jijini hapa.

Akizungumza mwisho wa wiki iliyopita, Wakili wa GSM, Alex Mgongolwa alisema mteja wake ana vielelezo vyote, huku Makonda akimtaka mfanyabiashara huyo kumwachia mai yake.

Akizungumza jana na Mwananchi kwa simu, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Salum Hamduni alisema suala hilo wanalifanyia kazi.

"Uchunguzi upo wa namna nyingi. Na mimi taarifa nimezisikia kupitia vyombo vya habari lakini tunaona kuna kazi ya kufanya katika hilo. Kwa hiyo tumelichukua tunalifanyia kazi," alisema Hamduni.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu uhalali wa vielelezo vya wawili hao, Kamishna wa Ardhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Idrisa Kayera alisema vyombo vya Serikali vinavyochunguza suala hilo.

"Zinachunguzwa (hati) na mamlaka nyingine ili kujua uhalali wao. Sisi tukipata wakishatoa maelekezo tutaendelea na hatua nyingne.

"Kwa mujibu wa utaratibu ni kwamba mtu ukifanya uhamisho anatakiwa awasilishe ofisini, ili ijulikane, lakini hilo tumeziachia mamlaka zifanyie kazi ili kujua," alisema.

Alisisitiza kuwa hizo ni mamlaka za uchunguzi, bila kuzitaja, huku akizitaka pande mbili kwenda kushtaki kwenye vyombo vya Dola.

"Kwa sababu wao wenyewe ndio walihusika kwenye mkataba baina ya Makonda na GSM, wao wapeleke kule, majibu tutaletewa, wakisema hivi vitu havina uhalali tutachukua hatua," alisema.

Akifafanua zaidi, Kayera alisema GSM alishatoa taarifa idara ya ardhi kuhusu kupotea kwa hati ya kiwanja hicho, na alipewa nakala ya uthibitisho mwingine.

"Baada ya kutoa taarifa kuwa amepoteza na kwa mujibu wa sheria, ukipoteza hati unaleta taarifa, inatangazwa kwenye gazeti la kawaida, inatolewa certified, kwa mujibu wa kumbukumbu, hatua hizo zilifuatwa, lakini kwa sasa si rahisi kusema nani ni halali," alisema.

Chanzo: Mwananchi
 
Kwahiyo Takukuru siku zote hawaoni umuhimu wa kuchunguza tuhuma za Makonda za matumizi mabaya ya ofisi ila hili la kiwanja ndio kazi yao.

Wakishachunguza watueleze pia Makonda alipata wapi million 120 na kwa mshahara upi?
 
Serikali imesema inalichunguza sakata la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed (GSM) la kugombea kiwanja Na.60 kilichopo Regent Estate Manispaa ya Kinondoni jijini hapa.

Akizungumza mwisho wa wiki iliyopita, Wakili wa GSM, Alex Mgongolwa alisema mteja wake ana vielelezo vyote, huku Makonda akimtaka
Imekula kwa Makonda
 
Hii story ya hati ya kiwanja kupotea kuna mahali ililetwa nikaiona, kumbe ni kweli huu mchezo GSM atakuwa alitoa kiwanja kwa Makonda wakati Makonda akiwa mkubwa sasa wamemgeuka baada ya "godfather" wake kuondoka, huu mchezo naona umechezwa na "wajanja" huko wizarani.

Kweli kutesa kwa zamu, naona TAKUKURU wameiwahi hii issue mapema ili kuwatuliza walioshika mpini kwa sasa, TAKUKURU ni ofisi fulani inayotumiwa na watawala na marafiki zao kwa mapenzi yao binafsi, sio kwa manufaa ya umma kwani wizi unaotokea huko serikalini kwa viongozi kuhusika huwa hawasemi chochote.
 
Serikali imesema inalichunguza sakata la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed (GSM) la kugombea kiwanja Na.60 kilichopo Regent Estate Manispaa ya Kinondoni jijini hapa.

Akizungumza mwisho wa wiki iliyopita, Wakili wa GSM, Alex Mgongolwa alisema mteja wake ana vielelezo vyote, huku Makonda akimtaka =
Siku hii kesi itakapotinga Mahakamani ndiyo tutajua ukweli kama Makonda na Bashite ni kitu kimoja.....!!
 
Hii story ya hatibya kiwanja kupotea kuna mahali ililetwa nikaiona, kunbe ni kweli huu mchezo GSM atakuwa aliucheza na wajanja huko wizarani.

Kweli kutesa kwa zamu, naona TAKUKURU wameiwahi hii issue mapema ili kuwatuliza walioshika mpini kwa sasa, TAKUKURU ni ofisi fulani inayotumiwa na watawala na marafiki zao kwa mapenzi yao binafsi, sio kwa manufaa ya umma kwani wizi unaotokea huko serikalini kwa viongozi kuhusika huwa hawasemi chochote.
Hapa inaonekana Kuna makubaliano halali yalifanyika kati ya GSM na Makonda kuhusu ununuzi wa kiwanja.Na yalifanyika wakati Makonda Ni mkuu wa mkoa.Sasa GSM amegeuka hayo makubaliano.Anaanza uongo.GSM anashirikiana na Ridhiwani Kikwete kudanganya umma.GSM inaonekana hana elimu .
 
Hii story ya hatibya kiwanja kupotea kuna mahali ililetwa nikaiona, kunbe ni kweli huu mchezo GSM atakuwa aliucheza na wajanja huko wizarani.

Kweli kutesa kwa zamu, naona TAKUKURU wameiwahi hii issue mapema ili kuwatuliza walioshika mpini kwa sasa, TAKUKURU ni ofisi fulani inayotumiwa na watawala na marafiki zao kwa mapenzi yao binafsi, sio kwa manufaa ya umma kwani wizi unaotokea huko serikalini kwa viongozi kuhusika huwa hawasemi chochote.
Nilipoona GSM aliooteza hati ya hiko kiwanja, nimeshajua ni kweli walimpa bashite. GSM anapotezaje hati ya kiwanja? [emoji23][emoji23]
 
Ukiwasoma watu walioko mamlakani pamoja na kwamba wanasema habari ya UCHUNGUZI kuendelea but kuna key words kadhaa hapo kwa hizo pande zilizo hojiwa is like Makonda kuna sehemu kadhaa kakosea so sitapata TABU kusikia baada ya Uchunguzi kwamba bwana Makonda alivamia kiwanja cha watu, just soma tena, kuna key words kadhaa hapo zinazo ashiria kwamba sheria IPO upande wa mfadhiri wa Yanga zaidi kuliko Makonda
 
Nilipoona GSM aliooteza hati ya hiko kiwanja, nimeshajua ni kweli walimpa bashite. GSM anapotezaje hati ya kiwanja? [emoji23][emoji23]
GSM ni mwanadamu pia ana udhaifu wake ila kwa historia yao ya ujanja janja kwa hili nakubaliana nawe, huu ni mchezo, na kile kiwanda chao Mwenge wakatia kiberiti kuzidi kuwadanganya wajinga.
 
Serikali imesema inalichunguza sakata la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed (GSM) la kugombea kiwanja Na.60 kilichopo Regent Estate Manispaa ya Kinondoni jijini hapa.

Akizungumza mwisho wa wiki iliyopita, Wakili wa GSM, Alex Mgongolwa alisema mteja wake ana vielelezo vyote, huku Makonda akimtaka mfanyabiashara huyo kumwachia mai yake.

Akizungumza jana na Mwananchi kwa simu, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Salum Hamduni alisema suala hilo wanalifanyia kazi.

"Uchunguzi upo wa namna nyingi. Na mimi taarifa nimezisikia kupitia vyombo vya habari lakini tunaona kuna kazi ya kufanya katika hilo. Kwa hiyo tumelichukua tunalifanyia kazi," alisema Hamduni.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu uhalali wa vielelezo vya wawili hao, Kamishna wa Ardhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Idrisa Kayera alisema vyombo vya Serikali vinavyochunguza suala hilo.

"Zinachunguzwa (hati) na mamlaka nyingine ili kujua uhalali wao. Sisi tukipata wakishatoa maelekezo tutaendelea na hatua nyingne.

"Kwa mujibu wa utaratibu ni kwamba mtu ukifanya uhamisho anatakiwa awasilishe ofisini, ili ijulikane, lakini hilo tumeziachia mamlaka zifanyie kazi ili kujua," alisema.

Alisisitiza kuwa hizo ni mamlaka za uchunguzi, bila kuzitaja, huku akizitaka pande mbili kwenda kushtaki kwenye vyombo vya Dola.

"Kwa sababu wao wenyewe ndio walihusika kwenye mkataba baina ya Makonda na GSM, wao wapeleke kule, majibu tutaletewa, wakisema hivi vitu havina uhalali tutachukua hatua," alisema.

Akifafanua zaidi, Kayera alisema GSM alishatoa taarifa idara ya ardhi kuhusu kupotea kwa hati ya kiwanja hicho, na alipewa nakala ya uthibitisho mwingine.

"Baada ya kutoa taarifa kuwa amepoteza na kwa mujibu wa sheria, ukipoteza hati unaleta taarifa, inatangazwa kwenye gazeti la kawaida, inatolewa certified, kwa mujibu wa kumbukumbu, hatua hizo zilifuatwa, lakini kwa sasa si rahisi kusema nani ni halali," alisema.

Chanzo: Mwananchi
Ridhiwani Kikwete yuko wizarani
 
Nilipoona GSM aliooteza hati ya hiko kiwanja, nimeshajua ni kweli walimpa bashite. GSM anapotezaje hati ya kiwanja? [emoji23][emoji23]
Hapo sasa,yani GSM na watalaam wake kweli waipoteze Hati?

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] huu ni mchezo anachezewa Bashite,kuna siku Rzwani alienda pale wizarani ki kazi,kumbe ni kummaliza Bashite,hati ipotee kisha ikutwe kwa mkuu wa mkoa??acha inyeshe tuone panapo vuja
 
Back
Top Bottom