TAKUKURU yaingilia kati sakata la Makonda na GSM. GSM aliripoti hati ya kiwanja kupotea

Hapa inaonekana Kuna makubaliano halali yalifanyika kati ya GSM na Makonda kuhusu ununuzi wa kiwanja.Na yalifanyika wakati Makonda Ni mkuu wa mkoa.Sasa GSM amegeuka hayo makubaliano.Anaanza uongo.GSM anashirikiana na Ridhiwani Kikwete kudanganya umma.GSM inaonekana hana elimu .
Mwaka 2013 Makonda alikua hohehai hana hela ya kununua kiwanja mikocheni kwa 120M

Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
 
Makonda atuonyeshe bank transfer aliyomlipa GSM, aonyeshe pia malipo ya serikali kwa ajili ya transfer na pia atuonyeshe baada ya kununua kiwanja aliingiza kwemye daftari za mali za watumishi wa umma.

Kama vyote hana basi alitaka kupora eneo la watu, pili kesi ya uhujumu uchumi kwa kuinyima serikali mapato inamhusu na pia kesi ya utakatishaji pia inamhusu.

Hili jambo sio dogo kama tunavyoona kwemye kesi ya maimuna na Ngoswe wakigombea kiwanja.
 
Baba alifariki watoto ni yatima wanateseka Sana hawa ila mama yao hana mpango nao maana walivimba endi za uhai wa baba
 
GSM anadai kafanya mkataba wa ujenzi wa milioni 640 na kampuni ya Group 6 International mnamo mwaka 2016, hapohapo Makonda anadai yeye ndiyo anafanya ujenzi pale unaosimamiwa na mdogo wake tokea 2018 na kanunua kila kitu kwenye eneo hadi AC na vifaa vingine vya ujenzi na risiti anazo. Hapo nani anadanganya?
 
Baba alifariki watoto ni yatima wanateseka Sana hawa ila mama yao hana mpango nao maana walivimba endi za uhai wa baba
Nyie baba yenu akiwa na nguvu mlikuwa mnatuonea Sana na kutudharau.
Maisha ama binadamu na Mali na pesa ujue kuvitenganisha ili uishi vizuri. Ukianguka na gari lako no watu watakaokusaidia na sio mipesa yako ndnai ya gari lako..sio upate pesa uwe limbukeni ujione kuwa waweza kuiendesha dunia Kama familia yako.
 
Hii story ya hati ya kiwanja kupotea kuna mahali ililetwa nikaiona, kumbe ni kweli huu mchezo GSM atakuwa alitoa kiwanja kwa Makonda wakati Makonda akiwa mkubwa sasa wamemgeuka baada ya "godfather" wake kuondoka, huu mchezo naona umechezwa na "wajanja" huko wizarani.

Kweli kutesa kwa zamu, naona TAKUKURU wameiwahi hii issue mapema ili kuwatuliza walioshika mpini kwa sasa, TAKUKURU ni ofisi fulani inayotumiwa na watawala na marafiki zao kwa mapenzi yao binafsi, sio kwa manufaa ya umma kwani wizi unaotokea huko serikalini kwa viongozi kuhusika huwa hawasemi chochote.
umeongea ukweli
 
Ni kweli ukifuatilia mazingira ya maelezo haya inaonekana Makonda alipewa kiwanja enzi zile za utawala ulee ambao mtoto kipenzi akikufanyia dhuruma yoyote mahali pakukimbila hapakuwepo zaidi ya kukubaliana na mtoto kipenzi wa baba mwenye nyumba.

Na watakuwa walifanya hivyo kwa usalama wao, tofauti na hivyo habari za kuhusika na madawa ya kulevya zingewahusu, kuvamiwa na watu wasiojulikana pengine na hata kuvamiwa na mtoto kipenzi wa baba mwenye nyumba kungewahusu.
 
Serikali imesema inalichunguza sakata la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed (GSM) la kugombea kiwanja Na.60 kilichopo Regent Estate Manispaa ya Kinondoni jijini hapa.

Akizungumza mwisho wa wiki iliyopita, Wakili wa GSM, Alex Mgongolwa alisema mteja wake ana vielelezo vyote, huku Makonda akimtaka mfanyabiashara huyo kumwachia mai yake.

Akizungumza jana na Mwananchi kwa simu, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Salum Hamduni alisema suala hilo wanalifanyia kazi.

"Uchunguzi upo wa namna nyingi. Na mimi taarifa nimezisikia kupitia vyombo vya habari lakini tunaona kuna kazi ya kufanya katika hilo. Kwa hiyo tumelichukua tunalifanyia kazi," alisema Hamduni.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu uhalali wa vielelezo vya wawili hao, Kamishna wa Ardhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Idrisa Kayera alisema vyombo vya Serikali vinavyochunguza suala hilo.

"Zinachunguzwa (hati) na mamlaka nyingine ili kujua uhalali wao. Sisi tukipata wakishatoa maelekezo tutaendelea na hatua nyingne.

"Kwa mujibu wa utaratibu ni kwamba mtu ukifanya uhamisho anatakiwa awasilishe ofisini, ili ijulikane, lakini hilo tumeziachia mamlaka zifanyie kazi ili kujua," alisema.

Alisisitiza kuwa hizo ni mamlaka za uchunguzi, bila kuzitaja, huku akizitaka pande mbili kwenda kushtaki kwenye vyombo vya Dola.

"Kwa sababu wao wenyewe ndio walihusika kwenye mkataba baina ya Makonda na GSM, wao wapeleke kule, majibu tutaletewa, wakisema hivi vitu havina uhalali tutachukua hatua," alisema.

Akifafanua zaidi, Kayera alisema GSM alishatoa taarifa idara ya ardhi kuhusu kupotea kwa hati ya kiwanja hicho, na alipewa nakala ya uthibitisho mwingine.

"Baada ya kutoa taarifa kuwa amepoteza na kwa mujibu wa sheria, ukipoteza hati unaleta taarifa, inatangazwa kwenye gazeti la kawaida, inatolewa certified, kwa mujibu wa kumbukumbu, hatua hizo zilifuatwa, lakini kwa sasa si rahisi kusema nani ni halali," alisema.

Chanzo: Mwananchi
Patamu hapo
 
Hamduni ananyatia kichwa cha Makonda
 
Back
Top Bottom