Jephta2003
JF-Expert Member
- Feb 27, 2008
- 6,590
- 6,355
Mwaka 2013 Makonda alikua hohehai hana hela ya kununua kiwanja mikocheni kwa 120MHapa inaonekana Kuna makubaliano halali yalifanyika kati ya GSM na Makonda kuhusu ununuzi wa kiwanja.Na yalifanyika wakati Makonda Ni mkuu wa mkoa.Sasa GSM amegeuka hayo makubaliano.Anaanza uongo.GSM anashirikiana na Ridhiwani Kikwete kudanganya umma.GSM inaonekana hana elimu .
NakaziaSawa
You can't be serious aisee 🙆♂️🙆♂️🙆♂️🙆♂️mama funga jela huyu X wako
umewaza kama mimi huu ni mtego kwa makonda. Takukuru wata muingiza pabaya apotezee hicho kiwanja.Kesi ya sabaya ilianzia hukohuko takukuru ....makonda kuwa makini
X Wake tena?Bashite afungwe tupunzike, mama funga jela huyu X wako, amekua DALALI TAPELI waviwanja.
Nyie baba yenu akiwa na nguvu mlikuwa mnatuonea Sana na kutudharau.Baba alifariki watoto ni yatima wanateseka Sana hawa ila mama yao hana mpango nao maana walivimba endi za uhai wa baba
Albert tunduni mwa sindao....... ameyataka mwenyewe....
umeongea ukweliHii story ya hati ya kiwanja kupotea kuna mahali ililetwa nikaiona, kumbe ni kweli huu mchezo GSM atakuwa alitoa kiwanja kwa Makonda wakati Makonda akiwa mkubwa sasa wamemgeuka baada ya "godfather" wake kuondoka, huu mchezo naona umechezwa na "wajanja" huko wizarani.
Kweli kutesa kwa zamu, naona TAKUKURU wameiwahi hii issue mapema ili kuwatuliza walioshika mpini kwa sasa, TAKUKURU ni ofisi fulani inayotumiwa na watawala na marafiki zao kwa mapenzi yao binafsi, sio kwa manufaa ya umma kwani wizi unaotokea huko serikalini kwa viongozi kuhusika huwa hawasemi chochote.
Yaani inawezekana walimpa hati halafu wakaripoti kupoteaKwa hiyo Mr. Makonda hakuona tangazo la kupotea kwa hati?
Ni kweli ukifuatilia mazingira ya maelezo haya inaonekana Makonda alipewa kiwanja enzi zile za utawala ulee ambao mtoto kipenzi akikufanyia dhuruma yoyote mahali pakukimbila hapakuwepo zaidi ya kukubaliana na mtoto kipenzi wa baba mwenye nyumba.Hii story ya hati ya kiwanja kupotea kuna mahali ililetwa nikaiona, kumbe ni kweli huu mchezo GSM atakuwa alitoa kiwanja kwa Makonda wakati Makonda akiwa mkubwa sasa wamemgeuka baada ya "godfather" wake kuondoka, huu mchezo naona umechezwa na "wajanja" huko wizarani.
Kweli kutesa kwa zamu, naona TAKUKURU wameiwahi hii issue mapema ili kuwatuliza walioshika mpini kwa sasa, TAKUKURU ni ofisi fulani inayotumiwa na watawala na marafiki zao kwa mapenzi yao binafsi, sio kwa manufaa ya umma kwani wizi unaotokea huko serikalini kwa viongozi kuhusika huwa hawasemi chochote.
Patamu hapoSerikali imesema inalichunguza sakata la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed (GSM) la kugombea kiwanja Na.60 kilichopo Regent Estate Manispaa ya Kinondoni jijini hapa.
Akizungumza mwisho wa wiki iliyopita, Wakili wa GSM, Alex Mgongolwa alisema mteja wake ana vielelezo vyote, huku Makonda akimtaka mfanyabiashara huyo kumwachia mai yake.
Akizungumza jana na Mwananchi kwa simu, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Salum Hamduni alisema suala hilo wanalifanyia kazi.
"Uchunguzi upo wa namna nyingi. Na mimi taarifa nimezisikia kupitia vyombo vya habari lakini tunaona kuna kazi ya kufanya katika hilo. Kwa hiyo tumelichukua tunalifanyia kazi," alisema Hamduni.
Akizungumza na gazeti hili kuhusu uhalali wa vielelezo vya wawili hao, Kamishna wa Ardhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Idrisa Kayera alisema vyombo vya Serikali vinavyochunguza suala hilo.
"Zinachunguzwa (hati) na mamlaka nyingine ili kujua uhalali wao. Sisi tukipata wakishatoa maelekezo tutaendelea na hatua nyingne.
"Kwa mujibu wa utaratibu ni kwamba mtu ukifanya uhamisho anatakiwa awasilishe ofisini, ili ijulikane, lakini hilo tumeziachia mamlaka zifanyie kazi ili kujua," alisema.
Alisisitiza kuwa hizo ni mamlaka za uchunguzi, bila kuzitaja, huku akizitaka pande mbili kwenda kushtaki kwenye vyombo vya Dola.
"Kwa sababu wao wenyewe ndio walihusika kwenye mkataba baina ya Makonda na GSM, wao wapeleke kule, majibu tutaletewa, wakisema hivi vitu havina uhalali tutachukua hatua," alisema.
Akifafanua zaidi, Kayera alisema GSM alishatoa taarifa idara ya ardhi kuhusu kupotea kwa hati ya kiwanja hicho, na alipewa nakala ya uthibitisho mwingine.
"Baada ya kutoa taarifa kuwa amepoteza na kwa mujibu wa sheria, ukipoteza hati unaleta taarifa, inatangazwa kwenye gazeti la kawaida, inatolewa certified, kwa mujibu wa kumbukumbu, hatua hizo zilifuatwa, lakini kwa sasa si rahisi kusema nani ni halali," alisema.
Chanzo: Mwananchi
Serikali imesema inalichunguza sakata la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed (GSM) la kugombea kiwanja Na.60 kilichopo Regent Estate Manispaa ya Kinondoni jijini hapa.