BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Geita imekamilisha uchunguzi safari ya China aliyokwenda aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Zahara Michuzi.
Uchunguzi huo ulioanza mwanzoni mwa Novemba 2023, ulitokana na agizo la aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita, Cornel Magembe la kuitaka Taasisi hiyo kuchunguza safari ya mkurugenzi huyo kama ilikuwa na masilahi ya halmashauri au ni maslahi binafsi.
Pia, aliitaka taasisi hiyo kubainisha kama matumizi ya safari hiyo yalitokana na fedha za halmashauri au ni za binafsi na endapo watabaini alitumia fedha za halmashauri, zirejeshwe na zielekezwe kutekeleza miradi ya maendeleo.
Akizungumza leo Aprili 25, 2024 wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa miezi mitatu iliyopita, Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Geita, Azza Mtaita amesema uchunguzi umekamilika, kwa sasa jalada lipo kwenye hatua nyingine ya kupata maoni ya kisheria ili hatua nyingine ziweze kufikiwa.
Hata hivyo, Mtaita hakueleza kilichobainika katika uchunguzi huo.
Zahra aliyehudumu kama mkurugenzi wa mji wa Geita kwa zaidi ya miaka miwili na Desemba 2023 alihamishwa kwenda Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro wakati uchunguzi huo ukiendelea.