Elections 2010 TAKUKURU yamkamata Magreth Sitta Tabora; Aachiwa kwa dhamana

Elections 2010 TAKUKURU yamkamata Magreth Sitta Tabora; Aachiwa kwa dhamana

CCM internal cleansing....kama ile ya Jugoslavija ya early 1990s....ili wabaki RA and tribe.....sijui hawa wapiganaji hawaoni...tokeni humo mje CHADEMA
 
Hizo ni cheche za Rostam na Lowasa dhidi ya chuki ya Richmond! kwani kuwa na mil.1 nikosa? mi nilidhani amekamatwa akigawa!
TAKUKURU waache chuki binafsi. Mbona walishindwa kukamata walio kwapua pesa BOT? mpaka leo ni usanii mtupi! Hivi hizo kesi ziliishia wapi? Kazi kutufanyia usanii.
 
so habari ndiyo hiyo

Huyu mama hana kesi hapo, hawa TAKUKURU wanajifanyia kazi kama amateurs.
Profiling yao haifiki katika tendo la kutaka kutenda kosa. Kumkamata mtuhumiwa
na vifaa vya kwake mwenyewe au pesza zake bado hakumfanyi kuwa ametenda kosa.
Wangeendelea kumfuatilia nyendo zake na kuona kama anagawa pesa au simu kwa
wapiga kura lakini wao wamekurupuka kabla mtuhumiwa kutenda hilo kosa la rushwa.
Mahakama yoyote ile itamwachia huru kwa kukosekana ushahidi wa kutosha.
 
eti kukutwa na nokia 7 (1616)= angalia picha chini, milioni moja na bahasha za kaki 100....Takukuru hao hewani!! Wakati wa Richmond hatukuwasikia!!!... USHAURI "Spika Sitta, Magret Sitta, Mwakyembe na wengineo tokeni CCM......................
1616_black_front_604x604.png
 
PCCB wanacheza mchezo wa kisiasa kuonyesha kuwa kweli wako kazini na wananchi waone kuwa serikali ilikuwa serious iliposema inakataa rushwa kwenye uchaguzi kuanzia mwaka huu. Hii itaisaidia sana CCM kuvuna kura kwa watu watakaoamini kuwa kweli kuna seriousness.

Itakapofika kwenye kampeni kubwa za vyama vingi, CCM itatumia ahadi ya kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa kama mtaji wao na kuonyesha kuwa ilianza kufanya hivyo kwenye chaguzi za ndani za kupata wagombea. Watasema, "Si mmeona tulikamata hata vigogo?" Wananchi watakubali na kuipa kura nyingi kama wataachiwa kuendelea na sanaa hii.

Kama kweli PCCB wako serious kukamata na kushitaki wagombea wanaotoa rushwa, ni dhahiri wangetumia njia zinazokubalika na ambazo zinaweza kutumika kufungulia mashitaka. Huwezi kumkamata mtu na kumtuhumu kwa hisia tu. Kuna watu wengi tu wanatembea na pesa nyingi kwenye magari yao mwaka mzima bila kuwa na nia ya kutoa rushwa kwa yeyote. Kuna watu wengi tu wanamiliki simu na mali nyingine nyingi tu kwasababu mbalimbali na wala sio rushwa. Iweje kwa kipindi hiki, mtu (mgombea) akiwa na mali au pesa awe na nia ya kutoa rushwa hata kabla hajaonekana akisogelea kuchukua hatua ya kufanya hivyo?

Mimi naona PCCB wanafanya hivyo ili baadae kusiwe na kesi ya wagombea hao kujibu na wakati huo huo CCM iwe imeshafaidika na mtaji huo wa kudhihirisha kuwa wanachukia rushwa. Itakuwa kosa kudhani kuwa CCM hawajui kuwa kero kubwa kwa wananchi kipindi hiki cha uchaguzi ni rushwa.
 
Ikiwa ni kiongozi aliwahi kuongoza inji hii.. na ukimwona anahangaika na vijibahasha vya khaki ili kuwarubuni wapiga kura kama inavyotuhumiwa kwa mama Maggie Sitta, ni dhairi kuwa hata katika vinyang'anyiro vilivyopita huyu mtu hakushinda kihalali bali kwa rushwa tu, huyu mtu si msafi tena wale wanaompigia kura wamwangalie mara mbili mbili!!!. Haiingii akilini kiongozi safi na aliyeshindwa kihalali akawa ana dhamira mbaya ya kutoa rushwa ili apate kuwashinda wengine. Hata kama ni tuhuma tu, mazingira ya tuhuma husika yanaleta hoja nyingi zisizo na majibu upande wa mhusika..kama wewe si mtumishi wa DHL, wala Shirika la posta, bahasha 140 tena za khaki ni za kazi gani katika kipindi cha kampeni?.

Hii inadhirisha pia jinsi gani hao mawaziri wa JK (Serikali) walivyotuhadaaa kuhusu usafi wao wa kupambana na rushwa.

Rai yangu ni kuwa TAKUKURU wakiendelea na Kamatakamata hii hata kama hakuna atakaefikishwa mahakamani, mbiu itakuwa imesikika kwa wale wengine ambao wameoza kwa kupitisha vibahasha na wanataka kuingia madarakani kwa mfumo wa "vibahasha". Wataogopa kufanya mchezo huu mchafu!!!


.................................................................................................................................

From DAILY NEWS Reporter in Tabora, 28th July 2010 @ 12:00

THE Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) here is interrogating 10 people, including the Minister for Community Development, Gender, and Children, Ms Margaret Sitta, on suspicion of bribing party members with cash and mobile phones to solicit votes.

Ms Sitta, who is the wife of the Speaker of Parliament and Urambo East MP, Mr Samuel Sitta, is among the aspirants for the parliamentary special seats in Tabora Region through the party's women's wing.

Briefing reporters here on Wednesday, the Acting Regional PCCB Commander, Mr Bruno Rwenyagira, said that the suspects were arrested on Tuesday at around 1:55am at a guest house known as Camise situated in Cheyo A area, 100 meters from the regional PCCB office.

He named other suspects nabbed alongside the minister as the Uyui District Youth Secretary, Julius Kilimanjaro, Ipuri Ward CCM Secretary, Lucas Simwanza, Lutende Ward UWT Secretary party's Elizabeth Kondora and the ward's UWT Chairperson, Catherine Sepetu.

Other persons held are a CCM guard, Michael Manyanda, a teacher at Majengo Primary School, Mary Joseph, Uyui CCM District Publicity Secretary, Rashid Abdalla, a guard with CCM, Abdul Kayamba and the minister's driver, Cosmas Urio.

The PCCB official further said that the minister was caught in possession of seven mobile phone handsets, 1,015,000/- cash and 145 empty envelopes.

Mr Bruno said that the PCCB had been tracking the minister from 10pm on Tuesday in the guest houses that were used to accommodate delegates to the regional women's congress that was to pick the MPs on Wednesday.

He added that all the suspects have been interrogated and that they would be sent to court once investigations are complete.

Other aspirants were the outgoing MP Aziza Sleyum Ally, Munde Tambwe, Mwalimu Roda Sangwa, Juliana Changarawe, Ria Mruma and Lesu Kasila.

SUMBAWANGA

Meanwhile, From PETI SIYAME reports from Sumbawanga that the PCCB in Rukwa region has arrested two aspirants who are aspiring for parliamentary seats through the women's wing (UWT) of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM).

The women allegedly bribed some members of the UWT General Congress. Sumbawanga CCM District Secretary Silafu Maufi confirmed that the arrests of Ms Esta Mikoama Wafwilikwiza and Ms Odina Lujaji took place.

She said that the two are accused of providing General Congress members with accommodation and breakfast at one of the guest houses in the municipality of Sumbawanga, in the quest to win favours in the ongoing election primaries process.

She further said that one of the suspects was arrested in a guest house popularly known here as Jangwani Inn. She was allegedly chatting merrily with several would-be voters who are members of UWT General Meeting.

It has been alleged that the accommodation and breakfast for the would-be voters has been paid for fully by the suspect.

However, Ms Maufi further said that the Sumbawanga CCM District Office has not yet received a report of the incident officially.

"I heard this morning (Wednesday) people saying that Esta has been arrested by PCCB officials, but I do not know yet where they found her.

However, it was alleged that the suspect was nabbed at Jangwani Inn in the municipality, in the company of several members of the UWT General Meeting.

She is suspected of providing them accommodation and breakfast in exchange of favours in their votes.

The Regional PCCB Commander, Mr Charles Nakambetwa, confirmed the incident, saying that the suspects were released on bail after interrogation.

However, Ms Maufi further said that the suspect was still a genuine candidate.

MARA

From Tarime in Mara Region, Mugini Jacob reports that PCCB officials on Wednesday were forced to chase one of the CCM members seeking nomination to contest the Tarime parliamentary seat from his home to the District CCM offices.

The drama took place after the aspirant, Nyambari Nyangwine, was cornered by the PCCB officials in his house on Sirari Road after a tipoff that he was about to bribe some party members.

"We got information this morning that he (Nyangwine) had hidden some UWT-CCM members in his house. We went to find out what was happening but he refused to talk to us," Tarime District PCCB chief Bathoromeo Semhunge told the 'Daily News.'

Mr Semhunge explained that when PCCB operatives arrived at the house of the aspirant, one of his supporters tried to cheat them that he (Nyangwine) was absent. He abused them in the process.

After few minutes later Nyangwine got out of the house along with unknown CCM members and fled in his motor vehicle to the District CCM offices, about five kilometres away.

The anti-corruption official said that when they reached the CCM offices, they approached Nyangwine but he refused to speak to them.

At the same time, Tarime Regional Special Police Zone Commander (RPC), Constantine Masawe was forced to deploy security personnel at the district CCM office to maintain law and order.

But still the anti-corruption officials failed to apprehend the aspirant on reasons that were not made clear by Mr Semhunge. He, however, said investigation is underway but gave no details. Mr Nyangwine was not immediately available for comment on the fracas.

Other CCM members vying for the post are Mr Ryoba Kangoye, Col Gichonge Mahende (retired), Professor Ainory Gesase, Mr Nyamhenga Borago, Mr Modekae Moseti and Mr Paul Matongo.

http://dailynews.co.tz/home/?n=12077&cat=home
 
hizi ni njama za ROSTAM NA HOSEA za kumpunguza nguvu SPIKA tu kwasababu aliwashugulikia bungeni mbona wabunge,wadiwani wengi tu wanakamatwa lakini haitangazwi???yaani MAGRET ndo wa kwanza kutoa rushwa????SPIKA hili lisikuvunje moyo tena ukirudi mjengoni washugulikie ipasavyo
Mheshimiwa ni kweli uyasemayo?
Mie naona ni mtego wa panya na paka, mpaka sasa naona picha inazidi kunoga na kujionea jinsi vionngozi wa Sisiem wasivyojiamini kwa kuwa hawana uwezo wa kuatatua shida za nji hii. Sasa we mke wa mtu unaenda wapi muda wote huu? Tena nyumba ya kulala wageni huoni aibu? Wewe si mlokole? nahisi ungekuwepo wakati wa Yesu angemuuza kwa bei mbaya sana
 
eti kukutwa na nokia 7 (1616)= angalia picha chini, milioni moja na bahasha za kaki 100....Takukuru hao hewani!! Wakati wa Richmond hatukuwasikia!!!... USHAURI "Spika Sitta, Magret Sitta, Mwakyembe na wengineo tokeni CCM......................
1616_black_front_604x604.png
Ulitaka waogopwe na waachwe waendelee kutoa mlungula? Kama wao ni wasafi wana wasiwasi gani? watulie makwao, wasipitepite usiku wa manane kwenye nyumba za kulala wageni. Hizo simu na bahasha si angeziacha nyumbani, au anataka kufungua biashara ya stationery
 
huyu mama alikuwa anataka kutoa rushwa, sema hao takukuru wamekukuruka ovyo,
mahakamani huyo mama hana kosa maana atashinda kiurahisi sana.
 
Nimesikia mdau mmoja anadai CCM kama hawakutaki kwenye chama lazima wakufanyie vimbwanga kama hivyo unasonteshewa tu.. ...Kuna mmoja yuko mitaa yeye anatoa Rushwa kwa style ya kipekee ..akipita hapa na Prado takukuru wakati wanasubiri hiyo Prado iondoke eneo la tukio yeye alishaondoka na Rav 4 da kweli Kidumu chama cha mapinduzi :doh:
 
Ni kosa kuwa katika nyumba ya kulala wageni?
Ni kosa kuwa na bahasha za kaki?
Ni kosa kuwa na simu mpya zaidi ya moja?
Ni kosa kutembea na shilingi milioni moja?

Hii yote sanaa tu..........!


kwenye hayo maswali yote sioni kosa...:nono:
 
Hosea na watu fanyeni kazi za maana ambazo bado hamjazimaliza shauri ya kukurupuka kama hivi, hivi hiki chombo toka kimeanzishwa mimi binafsi sioni kinafanya nini zaidi ya kukiona kama kama chama cha siasa, toeni kadi basi mpate wanachama
 
Kukamatwa kwa waziri Sitta ni kwa kawaida kama mtu yeyote mtoa rushwa ambavyo angeweza kukamatwa, suala kwamba kwa nini yeye ndiyo atangazwe sana na vyombo vya habari jibu ni jepesi, huyu ni waziri aliye maarufu, si maarufu kwa kuwa wazir tu bali kwa kuchanganya na kuwa kwake mke wa Spika anayejinadi mpiganiaji haki kwa kuwakataa mafisadi, lakini pia huyu mama ni maarufu kwa yeye mwenyewe kumuunga mkono mumewe na kambi yao ya wanaojiita wapinga ufisadi. Sasa basi, kwa sababu ya ukweli huu wote, wale wote wafanya ufisadi walikuwa makini sana sana kuwatafuta na kuwapunguza spidi zao.

Michakato yote iendelee ya kuwanasa wote wenye tabia hii. Hatuhitaji mchungaji au mhubiri asemaye tufuate maneno yake na si matendo yake, sisi tunataka vyote maneno na hata matendo yao.
 
Naenda kupiga kambi Igunga, na tutaleta ripoti humu...Team ni kubwa sana, inayoenda Igunga...Mark this post
 
Kukamatwa kwa waziri Sitta ni kwa kawaida kama mtu yeyote mtoa rushwa ambavyo angeweza kukamatwa, suala kwamba kwa nini yeye ndiyo atangazwe sana na vyombo vya habari jibu ni jepesi, huyu ni waziri aliye maarufu, si maarufu kwa kuwa wazir tu bali kwa kuchanganya na kuwa kwake mke wa Spika anayejinadi mpiganiaji haki kwa kuwakataa mafisadi, lakini pia huyu mama ni maarufu kwa yeye mwenyewe kumuunga mkono mumewe na kambi yao ya wanaojiita wapinga ufisadi. Sasa basi, kwa sababu ya ukweli huu wote, wale wote wafanya ufisadi walikuwa makini sana sana kuwatafuta na kuwapunguza spidi zao.

Michakato yote iendelee ya kuwanasa wote wenye tabia hii. Hatuhitaji mchungaji au mhubiri asemaye tufuate maneno yake na si matendo yake, sisi tunataka vyote maneno na hata matendo yao.

hapo nakubaliana na wewe mkuu ila hawakuwa smart enough walau kwa habari zilizopo kwenye media (maana huenda kuna ambayo TAKUKURU wanayajua na hawajayasema hadharani).

Ila kwa hili, mama Sitta anaweza kabisa kuwaburuza TAKUKURU mahakamani kwa kumchafulia jina......

wenye akili zetu tunajua, akili za kuambiwa na kon'gota tunachanganya na zetu
 
huyu mama alikuwa anataka kutoa rushwa, sema hao takukuru wamekukuruka ovyo,
mahakamani huyo mama hana kosa maana atashinda kiurahisi sana.

Wamechemka vibaya sana kwa kukimbilia kwa papala. Ni sawa na mpenzi wa mpira mwenye midadi mpira ukitoka sentimita chache anausindikizia kwa macho nyavuni.

Kukutwa na bahasha 140 kwani mgombea haruhusiwi kuwaalika baadhi ya watu kwa barua? Hii is ground less as far as intent was not vivid.

Kukutwa na simu siyo issue pia. Kule ni kwao na ukweni pia hivyo katika family level anaweza kununua gift yoyote na kupeleka regardless ya uchaguzi. kwani kwa sababu ya uchaguzi tu haruhusiwi kuwa na mapenzi mema kwa ndugu zake? This is groundless as no direct link to beneficiaries as it cant be concluded that they were for whoever was there.

Suala la kukutwa na 1,000,000 ni upuuzi mtupu kwani hatujui viongozi wetu wanalipwa kiasi gani kama mshahara na malupulupu? mbona hizi na senti ndogo tu. Mbona nimemwona Waziri akienda kutangaza nia kijijini kwao na gari la serikali siyo matumizi mabaya ya mali ya serikali? Mbona watu tayari wameanza kampeni dhidi ya vyama vya upinzani kabla ya muda?

Wake up Tanzanians! Simtetei kwa kutoa rushwa anaweza kuwa alitaka kufanya hivyo lakini upelelezi ni wa hovyo sana na unamweka huru au wameharibu maksudi ili kuonekana walifanya kitu baada ya kupewa lead iformation na raia wema
 
Hawa watu ,Mwakyembe,Sitta na wengine sijui kwa nini wanashindwa kusoma alma za nyakati.Hawatakiwa kabisa ccm na ndio maana wanawatengenezea zengwe.Ushauri wa bure ni wao kutoka na kutafuta chama kitakachowathamini.Subirini kampeni za kweli zianze kama mtasikia hii kamatakama ya kijinga.Naona na hao takukuru wamegeuka wale polisi wa Jerry Muro wasiokuwa na uthibitisho wanang'ang'ania alikuwa alikuwa.
 
Jamani tuweni wa kweli kwenye hili huyu mama si safi kama watu wanavyosema tunamjua ambavyo amekuwa akihonga walimu wenzie si leo tu! hizo simu zote na bahasha za nini kama sio kugawa mafungu! tena gest house! acheni mambo ya ajabu wapeni nafasi TAKURURU kufanya kazi zake!
 
Needs thinking... Ujio wa Slaa utasababisha baadhi ya watu wafikishwe mbele ya sheria haraka iwezekanavyo ili akose la kuongea kwenye kampeni maana JK atakuwa walau kawaonyesha watanzania kuwa 'anaweza kuthubutu'!

Lakini, hii kamatakamata isiishie hapo, hatua zichukuliwe, na wakimaliza kamatakamata yao tutakuja na video evidences za wale ambao hawakuwagusa kabisa na tutawaonyesha kwa kifupi tu via JF, wakibisha tutaleta FULL video clips ili kuwaonyesha kuwa wanaokamatwa ni vidagaa bado kwani kuna mapapa haswa!

Ndo maana tunaipigia chapuo JF as jukwaa sahihi la kusema ukweli bila uoga.
Thax Invisible.

Tanzania ya wajukuu zetu ipo mikononi mwa manyang'au na ni budi tuirejeshe na turudishe ile misingi yetu ya awali na kusonga mbele.
 
Nahisi niwakati muafaka Jk anaitaji kujua ni jeshi la mawaziri la aina gani alillokuwa nalo miaka 5 iliopita na kuwahadaa wananchi yuko na baraza lililo imara...nahisi vitendo vya rushwa vya kuwakamata watu ni mfano wa kujua ni wapi alipo na wapi anaelekea

kitendo cha kukamatwa mama magreth sitta ambae ni waziri kinatuonyesha nini kinaendelea na tutarajie baraza gani 2011

Kazi kwako mtanzania mpiga kura
 
Back
Top Bottom