Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
TAKUKURU GEITA YAWAFIKISHA MAHAKAMANI WABUNGE NA MADIWANI MAJIMBO YA CHATO KASKAZINI NA CHATO KUSINI
Ndugu Wanahabari,
Kati ya tarehe 28.11.2025 na tarehe 30.11.2025 TAKUKURU (M) Geita ilipokea taarifa za uwepo wa vitendo vilivyoshukiwa kuwa ni vya rushwa vilivyofanywa na Mhe. Cornel Lucas Magembe Mbunge wa Jimbo la Chato Kaskazini kwa kushirikiana na Mhe. Frank Leonard Francis aliyekuwa Diwani mteule Kata ya Mganza.
Uchunguzi ulithibitisha kuwa viongozi hawa waliwakusanya madiwani wateule 20 wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato katika Hoteli ya Lakezone iliyopo Jijini Mwanza na baadaye Serengeti Palace Hoteli iliyoko Mji Mdogo wa Katoro-Geita, kwa lengo la kuwashawishi kwa hongo ya fedha, chakula na malazi madiwani hao ili kupiga kura za upendeleo kwa mgombea waliyemtaka katika nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Chato.
Ndugu Wanahabari,
Katika taarifa nyingine ilidaiwa kwamba, Mhe. Pascal Lucas Lutandula Mbunge wa Jimbo la Chato Kusini kwa kushirikiana na Ndg. Bartholomeo Christian Manunga aliyekuwa Diwani mteule wa Kata ya Bwongera, na Mhe. Josephat Elias Manyenye aliyekuwa Diwani mteule Kata ya Bwera katika kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, walituhumiwa kujenga ushawishi wenye vitendo vya rushwa kwa Diwani mteule wa Kata ya Muungano Mhe. Njile Charles Mboligo kwa kumpa hongo ili kujiondoa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi ili kumpatia ushindi wa wazi Ndg. Bartholomeo Christian Manunga katika uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Chato.
Kufuatia matukio hayo Ofisi ilianzisha uchunguzi na kubaini uwepo wa vitendo vya rushwa katika mchakato wa uchaguzi huo wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kulazimika kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waliobainika kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 329 Marejeo ya Mwaka 2023 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 11/2024 ambapo watuhumiwa tajwa wamefikishwa Mahakamani leo tarehe 09/03/2026. Kesi hizi zimesajiliwa kwa nambari CC Na. 5100/2026 pamoja na CC Na. 5099/2026 mtawalia.
'Kuzuia Rushwa ni Jukumu Lako na Langu; Tutimize Wajibu Wetu'
Imetolewa na:
Juge
James G. Ruge
MKUU WA TAKUKURU (M) GEITA.
SIMU: 0738 150078