Mkuu na wewe unaonekana huifahamu vizuri Mara, ni mkoa wa kipinzani kwa miaka yote tangu chaguzi za vyama vingi zianze. Ebu niambie ni jimbo gani la mkoa wa Mara halijawahi kuwa chini ya upinzani.
Hesabu mnazopiga ndio zinakuwa ngumu kutokea kivitendo. Majimbo yote hayo JPM mwaka 2015 alikuwa anashinda kwa tofauti ndogo sana, sio kwamba majimbo wanayoshinda wabunge wa CCM basi wapiga kura wote ni CCM na yale ya CHADEMA si wapiga kura wote ni CHADEMA.
Nina uvivu wa kuandika lakini ningekupa historia ya mkoa huo tangu siasa za 1995 ambako baba wa taifa (RIP) mwenyewe alikuwa chini ya mbunge wa upinzani, huku Rorya ikienda kwa Mabere Nyaucho Marando, Mwibara ikienda kwa kijana wa upinzani na tangu hapo Musoma mjini imeshakuwa chini ya upinzani, Bunda ndio usiseme kabisa bila kusahau Serengeti na Tarime ambayo inatupa taabu sana na hata figisu za kuligawa jimbo hilo lilipelekea majimbo yote mawili kuwa upinzani. Kiufupi Mara na Kagera upinzani hupo na inabidi tuchange karata zetu vizuri sana na tuache blabla.