Takwimu: Mtu mmoja anakunywa pombe lita 10.4

Takwimu: Mtu mmoja anakunywa pombe lita 10.4

𝐇𝐚𝐭𝐚 𝐚𝐧𝐚𝐲𝐞𝐨𝐧𝐣𝐚 𝐚𝐧𝐚𝐨𝐧𝐣𝐚 𝐳𝐚𝐢𝐝𝐢 𝐲𝐚 𝐡𝐢𝐳𝐨 𝐥𝐢𝐭𝐚.
 
WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema takwimu zinaonesha kuwa wanywaji wa pombe wameongezeka nchini hali inayofanya kuanza uhamasishaji wa kupunguza unywaji wa pombe.

Takwimu alizotoa zinaonesha kuwa mtu mmoja anakunywa lita 10.4 kwa mwaka ambapo awali mtu mmoja alikuwa anakunywa lita 9.1.

Akizungumza katika Mkutano wa Kwanza wa Mipango Mikakati wa Kukabiliana na Magonjwa yasiyoambukiza Afrika (ICPPA) Ummy amesema takwimu za mwaka 2016 watu waliokuwa wanakunywa pombe walikuwa asilimia 26 na walipunguza hadi asilimia 20 lakini kiwango cha unywaji pombe kimeongezeka kwa sasa.

“Tunahamasisha kupunguza unywaji wa pombe ulipitiliza tumeongeza kiwango mtu mmoja anakunywa lita 10.4 kwa mwaka hii ni hatari kwa afya,”amesisitiza ummy

Ummy amesema kuwa Tanzania kama nchi zingine inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kudhibiti na wanaona ongezeko kubwa la watu wenye magonjwa yasiyoambukiza husani shinizo la juu la damu, kisukari, masuala ya afya ya akili, selimundu na mengine ikiwemo ajali.

“Tutaendelea kuwekeza katika mikakati ya kinga na kuhakikisha wananchi wanapata huduma na kwenye kinga tutajikita katika kutoa elimu ya afya kwa wananchi kujikinga na tumekuwa na wataalamu kama Prof Janabi wamekuwa wakihamasisha kuzingatia ulaji unaofaa.

Aidha amewasisitiza vijana kufanya mazeozi na wasisubiri wapate magonjwa hayo ndio waanze kufanya mazoezi.

Chanzo: Habari Leo
Lita 10 kwa mwaka?
mbona huyo anakunywa kistaarabu.
walevi wenyewe lita 10 hata wiki haimalizi
 
Lt. 10 kwa mwaka ni hatari!

Wakati dr. Janabi anashauri mtu mmoja kupata bia mbili kwa siku ambayo ni lt. 1 (Balimi na Safari .. 0.5 lt)

ie: 1x365 /10(crete) =lt 365.5 ama crete 36 na nusu kwa mwaka.

Tena huo ni unywaji kwa afya.

Sasa hizo crete 2 kwa mwaka halafu ni hatari kwa afya kwa nini wasiifute pombe?

Jamani au hizi ni takwimu za kupika Waziri kabambikwa?

Mi hainiingii akilini ati!
Hata Mimi nadhani Kuna makosa Kwa kizi takwimu🤣🤣🤣🤣
 
Lt. 10 kwa mwaka ni hatari!

Wakati dr. Janabi anashauri mtu mmoja kupata bia mbili kwa siku ambayo ni lt. 1 (Balimi na Safari .. 0.5 lt)

ie: 1x365 /10(crete) =lt 365.5 ama crete 36 na nusu kwa mwaka.

Tena huo ni unywaji kwa afya.

Sasa hizo crete 2 kwa mwaka halafu ni hatari kwa afya kwa nini wasiifute pombe?

Jamani au hizi ni takwimu za kupika Waziri kabambikwa?

Mi hainiingii akilini ati!
Watu wengi hamjaelewa kabambikwa kwa nini?
 
Watu wengi hamjaelewa kabambikwa kwa nini?
Ni hivi: bia za walala hoi kipimo cha chupa moja ni 0.5lt yaani nusu lita.

Na kiafya unashauriwa unywe bia2 kwa siku, maana yake lita 1 kwa siku.

Mwaka mmoja una siku 365, hapo maana yake ni bia crete36. 5.

Kwa ufafanuzi huo, mtu mmoja anatakiwa kunywa kwa afya Sim tank zima la bia lenye ujazo wa lt 350 na kidogo peke yake kwa mwaka.

Je kwa maelezo yangu na takwimu alizozitoa Waziri ni yapi sahihi?

Ndonikasema kuwa kama lita 10 za bia kwa mwaka mzima ni hatari kwa afya, basi bia zifutwe.

Au wewe umeelewaje?
 
Ok, nilidhani unabishia takwimu, kumbe unahoji usahihi wa madhara ya kiafya, hapo nimeelewa.
 
Yaan tunahangaika kupata vyanzo vya mapato anatokea wazir anapanga kampeni za kushusha mapato....mkitukasirisha tunahamia japan soon....Mtuache hii vita ni kali...KABURI NDILO LITAKALO FANYA MAAMUZI...over..
 
Back
Top Bottom