Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
ukipanda boda halafu tangu mwanzo wa safari dereva boda wako ni mwendo wa honi tu pwiiip pwiipwiip hadi mwisho wa safari anataka apite kila gari, kila kizuizi wala Subra, ujue soon mnapukutika nae....Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, kati ya Januari hadi Septemba 2023, kulikuwa na matukio ya Ajali za Pikipiki 339 zilizosababisha Vifo vya watu 263
Mkuu wa Dawati la Elimu Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Michael Deleli amesema Majeruhi walioripoti taarifa za Ajali kwenye Vituo katika kipindi hicho ni 252
Waathirika wakuu katika ajali nyingi za Vyombo vya Moto ni Abiria ambao ni 60% tofauti na makundi mengine yanayoathiriwa na Ajali hizo
Soma Takwimu zinaonesha kila sekunde 24 kuna mtu anafariki kwa ajali ya barabarani
maana semi trela imewasha indicator kabisa kwamba inakunja kulia au kushoto yeye analazimisha kupita huko huko na mihoni kibao kwa speed ya 100 kwenye kona shaaaa ...
Taa za barabarani nyekundu zimewaka kabisa na gari zimesima, anakuja boda na abiria wake pwiipwiip piiii piiii anazitime eti zilizoruhusiwa zipungue halafu eti kwa speed ajatize awahi kulikwepa lililoruhusiwa,
My friend wewe abiria na uyo boda wako soon mnapukutika kuongeza hiyo idadi ya waliopukutika kwa ajali ya boda bila wasi wasi wowote ....