SoC02 Takwimu ziwaongoze wananchi katika kujenga uchumi

SoC02 Takwimu ziwaongoze wananchi katika kujenga uchumi

Stories of Change - 2022 Competition

ismaelmkay

New Member
Joined
Aug 25, 2022
Posts
4
Reaction score
2
Uchumi ni utafiti wa uhaba na athari zake kwa matumizi ya rasilimali. Masomo ya uchumi huwa yanalenga kuelewa namna gani watu hu badili tabia ili kukumbana na hali inayoendelea. Uchumi hauna mipaka wala haujaeleweka kikamilifu. Bado kuna mambo mengi ambayo hupatikana kwa kushtukiza au yapo katika majaribio. Mengi sasa ni ya kutabiri tu kwa kutizama yale yanayofanana au kuelekeana.

Mipango yetu ya kiuchumi na maendeleo tumewaachia sana viongozi. Viongozi ambao tunaimani wanajua kile kilicho bora kwetu sisi na namna gani ya kukitekeleza. Hao viongozi wanapata fursa ya kututumikia kwa kupigiwa kura. Katika kutafuta kura huwa wana-ahidi kutimiza mambo mengi mazuri na yenye kutupa matumaini makubwa kuhusu baadaye. Lakini hata kama uchumi ni mpana sana, uwezo wa kiuchumi unakikomo na icho kikomo sio adhabu bali ni ukweli unaonesha uwezo na fursa zinazopatikana kwa muda huo.

Hizi ahadi za mara kwa mara zinatengeneza mazingira kwa wananchi ya kuamini kwamba kiongozi mzuri ni yule mwenye kuhaidi mengi. Na ndiyo chanzo cha mambo kama deni la taifa na tozo tunazoamrishwa kuzilipa. Tupo kwenye nafasi hii kwa sababu ya presha za voingozi kukubalika kwa haraka na kwa kuzooesha wananchi kwamba maendeleo ni yale tu wanayoyaona kwa macho na kwa haraka. Huu ni mfano wa mapungufu ya mfumo wa uongozi tunaotumia.

Hakuna jambo hapa duniani ambalo watu wachahe tu ndo wanalifaamu na wananchi wao hawawezi kueleweshwa. Hilo halipo katika kazi za utumishi wa umma. Kama wananchi tungependa tueleweshwe kwasababu kasi ya ubunifu unaotumika kubuni mbinu mpya za kuwatoza wananchi unatisha.

Kila mwaka serikali inatanganza bajeti inayonesha mapato inayotegemea kupata na matumizi inayotegemea kufanya. Bajeti hii inapitishwa na wabunge ambawo ni sauti ya wananchi kwasababu wanatumwa na wananchi. Huu ni mfumo unaokubalika leo lakini mapungufu hupatikana pale ambapo mwananchi sauti yake inaishia kwenye kumtuma muakilishi. Baada ya hapo ni juu yake huyu mbunge kupendekeza kama anavyojua yeye na mara nyingi kipaumbele ni kufanya mengi bila kujali mzigo anaombebesha mpiga kura wake. Mwananchi binafsi anaweza kujaribu kufanya lolote kupata wepesi lakini mbunge anafanya lolote kukubalika.

Pia, inafahamika kwamba ili mtu yoyote aweze kujadili au kuchangia kwenye jambo lolote, ni muhimu awe na takwimu na pia uwelewa wa kuzifafanua na kuzitendea hipaswavyo. Leo, hoja za wananchi nyingi hushindwa kupiga hatua kwasababu hawana takwimu sahihi ndo maaana mara nyingi tunaishia kwenye kusikia watu wanauliza, kwanini? Na nikwasababu kwa uelewa wake hakiingi akilini.

Maswali yetu kama wananchi sio magumu wala si ya uzushi bali ni maonesho ya kutokuelewa kwetu wapi tumekosea kama nchi. Nchi imejengwa na wazee wetu toka zamani kwa mipango ya kodi iliyopendekezwa kipindi hicho. Kwanini leo serikali imejikita zaidi kwenye ubunifu wa kumtoza mwananchi?

Kwani kodi tulizokuja tunalipa hazikutosha? Labda nchi imekuwa na serikali inakuwa pia lakini sii hivyo vyanzo vya kodi vinakuwa pia? Wapi tulidanganywa hapo awali hadi tuwe naulazima wa kuongezewa mzigo leo? Unasema tuchangie mia kwa jili ya ujenzi flani, kwani apo awali uwo ujenzi tuliupotezea? Na ni hadi lini tutachangia?

Kwani hu ndo mwongozo mpya wa kuuzoea? Umesema kuna tozo mpya na ni ya muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu, kwani hapo awali haikuwa ya muhimu? Umetumia mbinu gani kupata hitimisho ya kwamba tozo hazituumizi? Kwani sisi kama wananchi tumekosea nini ili tusijivunie na kipato hicho kipya?

Mapendekezo yangu ni, kwa kiwango cha elimu tulichoweza kufikia kama wananchi, ni vyema serikali iweke mpango wa kutoa taarifa sahihi kuhusu uwezo wa serikali yao, mipango iliyonao na mategemezi ya serikali kutoka kwa wananchi. Ambapo baada ya hilo kwa kushirikiana na wataalam pia kuonesha vipaumbele.

Mfumo wa uongozi ambao unafanya sauti ya mwananchi kuishia kwenye kumchagua muakilishi wake bungeni umepitwa na wakati. Mwananchi anatakiwa awe na mamlaka ya kufikisha sauti yake hatua nyingine zaidi. Aweze kuchangia kwenye kukubali serikali ifanye matumizi flani haswa yale yatakayokuwa yanamlazisha kutozwa zaidi au kuipelekea serikali kukopa.

Wakati waliopo madarakani wakipendekeza malengo. Vyama vya siaisa viendelee kuelimisha na kumshawishi mwananchi apendekeze ayo malengo yapite au yasipite kwa kutoa elimu ya ufafanuzi na kuonesha faida na mapungufu ambayo yatatokea. Huu mfumo utakuwa kwa kweli ndo umemuhusisha kikamilifu mwananchi katika maswala ya maendeleo nchini.

Hii itasaidia wananchi kutokutegemea vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wa serikali yake na kushiriki kizalendo kwenye kuukuza uwo uwezo. Pia itapunguza mzigo kwa viongozi ili wasiwe na ulazima wa kutoa ahadi hewa au za uongo. Kwa mfumo huu kiongozi bora atakuwa yule anaetimiza malengo kwa mda bila kuwapa mzigo mkubwa wananchi wake na yule anayetumia cheo chake kutimiza malengo na matakwa ya wananchi kwa vyanzo vilivyo karibu yake kama walivyopendekeza wananchi. Huu mfumo wa kutumia takwimu utasaidia sana ata pale kwenye mazungumzo kuhusu matumizi yasio ya lazima kwa mda huo.

Kutangaza malengo makubwa ya kimaendeleo ni jambo la kufurahisha na kusisimua. Lakini utekelezaji wake uko vipi? Malengo makubwa na mazuri tunayapenda lakini tunafikaje? Lazima tuelewe kwamba kiongozi ni binadamu pia na mienendo ya kiuchumi haimpi mtu yeyote uwezo wa kuunda kitu chochote toka hewani. Na wewe kama kiongozi ni vyema hutambuwe hili. Ili usilazimike kujikita kwenye ubunifu wa kuutafuta uwezo wa utekelezaji kwa kumuumiza yule yule mwananchi unayetaka kumhudumia kisa umetoa ahadi.

Kwa kumalizia naomba nisistize kwamba viongozi hawajakosea wala si wananchi. Kwasababu makundi yote haya ni washiriki tu kwenye mfumo wa uongozi ambao tumeupokea. Mwingine anaweza kusema ni chama tawala ndiyo kimechochea huu mfumo lakini hata vyama pinzani vinashiriki kwenye huu mchezo wa kuaminika zaidi na kutoa ahadi hewa kwa wananchi. Kwahiyo ni bora mabadiliko yawepo kwenye mfumo mzima ambapo sasa wananchi watachugua kwa hoja, uwezo na matumaini yaliyo sahihi. Vyama vya siasa visijikite zaidi kwenye kufanya mtu fulani akubalike bali kwenye kusukuma hoja zilizonyooka kwa watu.

Kama mfumo wa uongozi unalenga kufanya sauti za wananchi zisikike basi huu ndo mfumo bora. Huu mfumo utaweka wazi utendaji mzima na mikakati yote ya serikali. Hii ni bora zaidi ya mfumo uliyopo ambao unaweka mbele siiri, unawaweka watu mbali na serikali yao na viongozi hawawajibiki hipaswavyo pale wananchi wasiporidhika.

5ABD7642-EB17-4CCB-83D3-18213843E5F7.jpeg
 
Upvote 0
Back
Top Bottom