Talaka inavyoniaribia Binti yangu mapemađź’”

Pole sana kwa changamoto hio.
Binti yako baada ya kujazwa hio sumu na mama yake. Basi nayeye kaanza kuona kilicho mtokea mama yake kinaweza kumtokea na yeye ndo maana hatamani kuzaa wala kuolewa. Mpe muda akikua ata Elewa
Kitu kingine mpige stop huyo Ex wako maana anakuaribia familia yako na hapendi furaha na maendeleo yake. Kata kabisa mazoea nae. Ishu ya feminism ina waharibu eti No marriage no Stress
 
Kaka hayo usemayo nilijitahid saana lla mama Yao amekaza mwenye mawazo ya ki feminist.
Yeye mwenyewe ametoa pesa yake kuhakikisha talaka inatoka.

Omba lisikyfike
 
Kuachana ni issue ila kuoa tena ni issue nyingine.
Kupata bahati ya kuwa single kihalali ni kitu kisicho cha kuchezea , hio ilikua ni golden chance bro umechezea.

Mpe muda huyo mtoto, endelea kumlisha positive hata kama ameshiba negative.

This is a statement, kuwa single again sio fursa ya kuchezea, jamaa kaenda oa nchi jirani, shida sana!
 
Umenena ukweli mtu na licha ya watoto pia ninaudhaifu kuishi mwenyewe hua naathirika Hadi kiafya
 
9years is too young to be discussing marriage. Huyo ni mtoto saizi awaze vitu vya umri wake. Friends, shule, masomo hata muwe mnaulizana akikua anataka kua nani, kama anataka kuwa pilot basi maramojamoja unamtreat flight moja kwenda mkoa wa tofauti kuchochea ndoto zake, kama ni kuwa doctor unamnunulia books ama vitu vinaendana na career anayotaka. Unamuelekeza kwenye vitu tofauti kabisa na mambo ya ndoa. Sasa miaka 9 mnadiscuss ndoa kweli 🙄🙄 Hebu kuwa serious baba nanii
 
Mtoto wa miaka 6-8 anauwezo wa kutumia asilimia 80 ya ubongo wake na ndiyo maana wachina huwa wanawaweka pamoja watoto wenye akili wenye umri huo, (incubate), and nurturing
 
Kitu ambacho nimejifunza wanaume inabidi tujijali sana wenyewe.

Maana mama hata awe muovu vipi bado watoto watamtetea na kumuonea huruma yeye kuliko wewe.

Na wewe baba hata uwajali vipi wanao, Bado watazidi kuzidisha mapenzi kwa mama.
 
Sure binafsi najitahidi kuhakikisha upendo na ndio umetawala kwangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…