Nnaimani mnaendelea vizuri wanajamii forum,
Kama kawaida yangu kuwaleteeni Mikasa inayonitokea kwenye maisha yangu, sababu hapa ndio sehemu pekee nisiyojulikana uhalisia wangu, napata uhuru zaidi wa kufunguka ili kupata ushauri wa kunikosoa na kuniita moyo.
Ni hivi baada ya kutengana na aliyekua mke wangu, Sasa tunaelekea mwaka wa nne, na muda si mrefu tunakamilisha talaka.
Hapo awali mwanamke aling'ang'ania kukaa na watoto kitu ambacho kiliniumiza saana. lakini nikacheza na akili yake kiasi Cha yeye mwenyewe kutamka kuniachia watoto wangu niishi nao.
Hata hivyo nilishapata mwanamke kutoka nchi jirani ambaye niliamini ataishi vizuri na watoto wangu Hawa wadogo baada ya kua nae kwenye mahusiano kwa kipindi Cha mwaka kabla hajarudi kwao.
Nilimsafirisha kutoka nchini kwao Hadi hapa Tz na Sasa ananilelea watoto, na watoto wangu naona wakipendeza japo huyu Binti angu akibadilika badilika mood.
Mama Yao (mtalaka) aliumia saana kiskia kuna mwanamke naenda kuishi nae, kitu ambacho alitaka aje ampe masharti (kumtisha) huyu mwanamke wangu mpya (step mother) endapo hatoishi vizuri na watoto wake, kitu ambacho Mimi nilimkataza.
akasema anajua atakachofanya kwa watoto maana atawajaza sumu ili wajilinde dhidi ya huyo step mother wao hili nalo nilimuonya lakini nadhani alilifanya kwakua Kuna mambo napambana nayo Sasa nadhani ni matokeo ya hizo sumu.
Binti (9yrs) yangu amekua hamfurahii step mother wake bila sababu ya msingi hata nilipokaa nae kuzungumza nae aliniambia Hana tatizo nae zaidi aliniuliza kwann nimeachana na mama Yake?
Ni desturi yangu kufanya nao ibada pamoja na kuwasaidia masomo Yao hivo wamekua wakiniuliza maswali mbali mbali kwakua wanajua baba Yao hua sifichi.
Mara kadhaa nimekua nikiwasisitizia majukumu Yao ya baadae watakapokua wakubwa kwamba wakiume atakua baba na familia yake na wakike atakua mama wa familia yake.
kila ikifika hatua ya kusema Binti yangu ataolewa na kua na familia yeye anabadilika sura na kukataa kati kati kwamba hato olewa Wala kuzaa nikimuuliza kwann anasema hataki tuu...
Nawaza saana na kujiuliza yule mama yake ni kama mfeminist tuu anakauli za kusema hataki tena kuolewa na haamini katika ndoa na ndoa ni kama utumwa Sasa anaishia kuchapika tuu mjini naona kabisa hiki kilicho kichwani kwa Binti yangu ni matokeo ya kuachana na mama Yao na ndio sumu alizomtia Binti yangu...
Wataalamu nisaidieni nawezaje kumuokoa Binti yangu dhidi ya hili balaa maana Dunia ishaharibika..
Note: kataa ndoa ushauri wenu naujua MSIkomenti.