Talaka inavyoniaribia Binti yangu mapema💔

Talaka inavyoniaribia Binti yangu mapema💔

Shkamoo babu wa busara,

unajua mda mwingine sisi wanawake, mwanaume anaeza kua tayar kusamehe yaishe lakini mwanamke nkakomalia talaka na kufanya vituko juu tena vya ajabu,kwahiyo kuliko kufa presha heri ukubali tu.

kuoa haraka labda aliona hatoweza kulea na kusimamia watoto ye mwenyewe kulingana na maisha yake yalivyo🥲coz ukisoma hapo sababu kuu ya yeye kuoa tena ni watoto.

(ulinde sana moyo wako kuliko vyote ulindavyo,mana ndiko zitokako chemchemi za uzima).

Ni kweli, mara nyingi Wazazi huwafikiria zaidi watoto.

Kwahiyo maamuzi mengi tunayafanya Kwa kuwaangalia zaidi wao

Shukrani Mjukuu, I real appreciate 🙏
 
Watoto umewaingizia mawazo ambayo hayalingani na umri wao
Mtoto wa 9yrs unamwambia ishu za ndoa ili iweje?
Mkuu umefail parefu
 
Nnaimani mnaendelea vizuri wanajamii forum,

Kama kawaida yangu kuwaleteeni Mikasa inayonitokea kwenye maisha yangu, sababu hapa ndio sehemu pekee nisiyojulikana uhalisia wangu, napata uhuru zaidi wa kufunguka ili kupata ushauri wa kunikosoa na kuniita moyo.

Ni hivi baada ya kutengana na aliyekua mke wangu, Sasa tunaelekea mwaka wa nne, na muda si mrefu tunakamilisha talaka.

Hapo awali mwanamke aling'ang'ania kukaa na watoto kitu ambacho kiliniumiza saana. lakini nikacheza na akili yake kiasi Cha yeye mwenyewe kutamka kuniachia watoto wangu niishi nao.

Hata hivyo nilishapata mwanamke kutoka nchi jirani ambaye niliamini ataishi vizuri na watoto wangu Hawa wadogo baada ya kua nae kwenye mahusiano kwa kipindi Cha mwaka kabla hajarudi kwao.

Nilimsafirisha kutoka nchini kwao Hadi hapa Tz na Sasa ananilelea watoto, na watoto wangu naona wakipendeza japo huyu Binti angu akibadilika badilika mood.

Mama Yao (mtalaka) aliumia saana kiskia kuna mwanamke naenda kuishi nae, kitu ambacho alitaka aje ampe masharti (kumtisha) huyu mwanamke wangu mpya (step mother) endapo hatoishi vizuri na watoto wake, kitu ambacho Mimi nilimkataza.

akasema anajua atakachofanya kwa watoto maana atawajaza sumu ili wajilinde dhidi ya huyo step mother wao hili nalo nilimuonya lakini nadhani alilifanya kwakua Kuna mambo napambana nayo Sasa nadhani ni matokeo ya hizo sumu.

Binti (9yrs) yangu amekua hamfurahii step mother wake bila sababu ya msingi hata nilipokaa nae kuzungumza nae aliniambia Hana tatizo nae zaidi aliniuliza kwann nimeachana na mama Yake?

Ni desturi yangu kufanya nao ibada pamoja na kuwasaidia masomo Yao hivo wamekua wakiniuliza maswali mbali mbali kwakua wanajua baba Yao hua sifichi.

Mara kadhaa nimekua nikiwasisitizia majukumu Yao ya baadae watakapokua wakubwa kwamba wakiume atakua baba na familia yake na wakike atakua mama wa familia yake.

kila ikifika hatua ya kusema Binti yangu ataolewa na kua na familia yeye anabadilika sura na kukataa kati kati kwamba hato olewa Wala kuzaa nikimuuliza kwann anasema hataki tuu...

Nawaza saana na kujiuliza yule mama yake ni kama mfeminist tuu anakauli za kusema hataki tena kuolewa na haamini katika ndoa na ndoa ni kama utumwa Sasa anaishia kuchapika tuu mjini naona kabisa hiki kilicho kichwani kwa Binti yangu ni matokeo ya kuachana na mama Yao na ndio sumu alizomtia Binti yangu...

Wataalamu nisaidieni nawezaje kumuokoa Binti yangu dhidi ya hili balaa maana Dunia ishaharibika..

Note: kataa ndoa ushauri wenu naujua MSIkomenti.
Mfanye rafiki yako wa karibu na vizawad vya hapa na pale lakini pia waombee sana watoto hasa watolee sadaka. Watoto wanaombewa mzee na kuwatolea sadaka na ukipata muda uwe unaenda nao kuwatembelea watoto yatima unawapa hela za kuwapa na vizawad. Kisha ombea watoto wapate wenza wema maishan. Mungu ni muaminifu atajibu. Mi mpaka kesho ninaamin nimefika hapa kwa maombezi ya wazazi wangu hasa maza. Ukitaka usalama wa watoto usidhulumu, usiibe wala kumfanyia yeyote baya coz sheria ya asili ina tabia ya kudai.
 
Binti wa miaka 9 ashakuwa na mawazo ya kuolewa au kutoolewa... Mimi binti yangu naye ana miaka 9 nadhani hata wazo hilo hana kabisa na wala hajaelewa ndoa hata ni kitu gani.
Mimi mwenyewe single father
Huenda wewe ndo hujaelewa kama anaelewa hayo mambo. Muhimu sana kua na personal/friend talks na watoto utayajua mengi
 
Kulikuwa na sababu ipi kubwa ambayo mlishindwa kukaa chini na Mkeo mtalikiwa hadi mfikie kutalikiana?

Wake zetu Kuna wakati Wana kera na kutuudhi, lakini kwani hukujua umemwoa binadamu mwenzio nasio Malaika?

Kwani wewe hukuwahi kumkosea Mkeo na akakusamehe mara kadhaa?

Anyways, Kwa maoni yangu ulifanya haraka Kuoa tena mara baada ya kutalikiana na aliyekuwa Mkeo.
Bora kuachana mapema kuliko kuja kuuana huko ndoani jamaa yuko sahihi
 
Ndugu hata ufanyaje mtoto niwamama we kula maisha nambususu mpya mpe huduma bint yako kama kawaida mambo yabadae huko achana nayo mana huna unaweza kubadili
 
ishi vizuriii kwa upendo mkuu na huyo mwanamke uliyenae sasa,ili ajionee uzuri wa familia,amini atabadilika.

Acha kuongea nae hayo maswala,wacha ajionee wewe na huyo mkeo mwingine mkiishi kwa amani, furaha na upendo.


Huyu jamaa amekushauri vizuri Sana hata Mimi na mke Wangu Ndio MAISHA ambayo tutaishi DHIDI ya watoto WETU, weka distance na Watoto wako then kuwa karibu na huyo mke wako mkishauriana pamoja, mkila pamoja, mkifurahi pamoja, mkitoka pamoja na kufanya Mambo mengine kwa pamoja huku mkiwaacha watoto wakiwa watazamaji, wakiwaangalia mnavyopendana na kuwa na umoja....


Amini Mkuu hutotumia Nguvu tena ya maneno kuweka Maono dhabiti na SAHIHI NDANI yake B'se picha husafilisha Mawazo kwa kasi sana kuliko Sauti, usiweke ukalibu na hao Watoto watakusumbua sana na kukutia stress na utakufa mapema, weka distance kidogo na wao ili uwape nafasi ya kukuona vyema na kwa usahihi wewe na mkeo mnavyoishi amini hayo Mawazo ya kishetani ya kutotaka kuolewa na kuzaa yatamtoka B'se atashuhudia raha na furaha na Amani katika NDOA kitu ambacho kitaprove wrong ile sumu aliyopandwa na mama yake kuhusu kusudi la MUNGU 👉 NDOA


Wewe ni baba na kiongozi Usijengee ukaribu na Watoto Mkuu B'se watakuzoea na mazoea huleta KIBURI na jeuri, jenga ukaribu na mke wako Harafu acha Watoto wawatazame wewe na mke wako mkiwa pamoja na mkifurahia NDOA YENU fanya hivyo utakuja Kushukuru hapa
 
Back
Top Bottom