Talaka inavyoniaribia Binti yangu mapema💔

Talaka inavyoniaribia Binti yangu mapema💔

Mpaka hapo kakua ndo anakoelekea pia...mi mwanangu wa kiume ni miaka 9 pia lakini hathubutu kuniuliza maswali ambayo anajua yataniumiza japo najua anatamani kujua mengi ila anahuruma sana...huwa ananiangalia sana machoni kujua hali yangu au mood yangu.Ni mwema kwa kweli.

Hakuna MTOTO wa kiume ambae si MWEMA kwa mama yake
 
Nnaimani mnaendelea vizuri wanajamii forum,

Kama kawaida yangu kuwaleteeni Mikasa inayonitokea kwenye maisha yangu, sababu hapa ndio sehemu pekee nisiyojulikana uhalisia wangu, napata uhuru zaidi wa kufunguka ili kupata ushauri wa kunikosoa na kuniita moyo.

Ni hivi baada ya kutengana na aliyekua mke wangu, Sasa tunaelekea mwaka wa nne, na muda si mrefu tunakamilisha talaka.

Hapo awali mwanamke aling'ang'ania kukaa na watoto kitu ambacho kiliniumiza saana. lakini nikacheza na akili yake kiasi Cha yeye mwenyewe kutamka kuniachia watoto wangu niishi nao.

Hata hivyo nilishapata mwanamke kutoka nchi jirani ambaye niliamini ataishi vizuri na watoto wangu Hawa wadogo baada ya kua nae kwenye mahusiano kwa kipindi Cha mwaka kabla hajarudi kwao.

Nilimsafirisha kutoka nchini kwao Hadi hapa Tz na Sasa ananilelea watoto, na watoto wangu naona wakipendeza japo huyu Binti angu akibadilika badilika mood.

Mama Yao (mtalaka) aliumia saana kiskia kuna mwanamke naenda kuishi nae, kitu ambacho alitaka aje ampe masharti (kumtisha) huyu mwanamke wangu mpya (step mother) endapo hatoishi vizuri na watoto wake, kitu ambacho Mimi nilimkataza.

akasema anajua atakachofanya kwa watoto maana atawajaza sumu ili wajilinde dhidi ya huyo step mother wao hili nalo nilimuonya lakini nadhani alilifanya kwakua Kuna mambo napambana nayo Sasa nadhani ni matokeo ya hizo sumu.

Binti (9yrs) yangu amekua hamfurahii step mother wake bila sababu ya msingi hata nilipokaa nae kuzungumza nae aliniambia Hana tatizo nae zaidi aliniuliza kwann nimeachana na mama Yake?

Ni desturi yangu kufanya nao ibada pamoja na kuwasaidia masomo Yao hivo wamekua wakiniuliza maswali mbali mbali kwakua wanajua baba Yao hua sifichi.

Mara kadhaa nimekua nikiwasisitizia majukumu Yao ya baadae watakapokua wakubwa kwamba wakiume atakua baba na familia yake na wakike atakua mama wa familia yake.

kila ikifika hatua ya kusema Binti yangu ataolewa na kua na familia yeye anabadilika sura na kukataa kati kati kwamba hato olewa Wala kuzaa nikimuuliza kwann anasema hataki tuu...

Nawaza saana na kujiuliza yule mama yake ni kama mfeminist tuu anakauli za kusema hataki tena kuolewa na haamini katika ndoa na ndoa ni kama utumwa Sasa anaishia kuchapika tuu mjini naona kabisa hiki kilicho kichwani kwa Binti yangu ni matokeo ya kuachana na mama Yao na ndio sumu alizomtia Binti yangu...

Wataalamu nisaidieni nawezaje kumuokoa Binti yangu dhidi ya hili balaa maana Dunia ishaharibika..

Note: kataa ndoa ushauri wenu naujua MSIkomenti.
Kwanza pole hizo ni changamoto za maisha tatizo kubwa hapo ni hao watoto kulelewa na step mother , kimsingi hakuna naeweza kulea mtt asomzaa vzr kama mama mtu hata iweje ungetengenez mazingr tu wallet na mama yao kuliko ulichofanya hatar sna ogopa matapel
 
Athari za kuvunjika ndoa ni wazi huathiri pia malezi ya watoto.
Ninachokiona hapo ni kuwa binti yako anaamini wewe baba ndiye mkosaji na chanzo cha mama yao kuondoka. Na kama aliwahi kushuhudia ukimpiga, kumnyanyasa mama yao, ni vigumu kuondoa kinyongo hicho moyoni mwake; na hii hupelekea kuwachukia wanaume wote au kuchukia maisha ya ndoa.
Kama unaamini wewe upo sahihi, mueleze ukweli chanzo cha mama yao kuondoka. Akijua mama ndiye mkosaji, atakuwa upande wako.
 
Kwanza pole hizo ni changamoto za maisha tatizo kubwa hapo ni hao watoto kulelewa na step mother , kimsingi hakuna naeweza kulea mtt asomzaa vzr kama mama mtu hata iweje ungetengenez mazingr tu wallet na mama yao kuliko ulichofanya hatar sna ogopa matapel

MKUU kuna tofauti kati ya malezi na kuwahudumia Watoto, mama yao wa kuwazaa atakuwa better katika kuwahudumia na kuwapendelea Watoto ila huyo Mama yao wa kambo atakuwa better katika kuwalea na kuwapenda watoto

Kuna dhana potofu DUNIA inatufundisha na kutuaminisha kuhusu UPENDO 👉 kuna tofauti Kati ya kupenda na kupendelea na kibaya Zaidi Dunia inatufundisha Kwamba, kupendelea Ndio kupenda kumbe tunatenda kinyume na UPENDO... Mama wa kambo atakua neutral kwa hao Watoto hatowapendelea kamwe na huko ndiko kutenda Upendo wa Kweli kwa Watoto

Unafikiri kwanini waswahili husema MTOTO kwa mama HAKUI? ✍️
 
9yrs Bado huyo nenda nae taratibu tu mtoto wa kike ukiwa nae karibu lazma akusikilize tu baba ake
 
Huu uzi ni mzito na ni rahis tu kukoment ila muhusika ndo anajua joto Lake, mama awe anapenda au anapendelea still huwez linganisha na huo upendo wa mama wa kambo ever. ndo mana watu hata biblia inakataa kuachana sab wanaoumia ni wengine. ila Inapolazimu bas watot waish na mama yao over.
 
Hujanibu swali nimekuuliza 👉 unafikiri kwanini waswahili husema MTOTO kwa mama HAKUI?
 
Binti wa miaka 9 ashakuwa na mawazo ya kuolewa au kutoolewa... Mimi binti yangu naye ana miaka 9 nadhani hata wazo hilo hana kabisa na wala hajaelewa ndoa hata ni kitu gani.
Mimi mwenyewe single father
Unajiona umepatiia mwenyewe. Anapswa ajue na aelezwe kama yapo madhara ya kuiingia mapema au faida iwapo zipo.
Na usipomwambia Wewe ataambiwa na wengine tena kwa namna wanayoijua na kuipenda wao
 
Unajiona umepatiia mwenyewe. Anapswa ajue na aelezwe kama yapo madhara ya kuiingia mapema au faida iwapo zipo.
Na usipomwambia Wewe ataambiwa na wengine tena kwa namna wanayoijua na kuipenda wao
Kwa hiyo wewe una binti wa miaka 9 anayejua masuala ya ndoa?
 
Ni bora ukosee maisha lakini usikosee kuoa. Ni hasara kubwa inayoondoa hata maana ya maisha yenyewe.

Alafu Oi! inakuwaje unamfundisha mtoto wa miaka 9 maswala ya ndoa na kuolewa? Sio kwamba bado ni mdogo tu. Bali hayo mambo hatakiwi kuyasikia kutoka kwako hata akifika 18. Kunormalize hayo mambo kwenye umri huo ni kosa kubwa sana, kwani ataona sex ni kitu cha kawaida na lazima awe malaya kupita viwango. Unatakiwa umfundishe kujitegemea, kujituma na kujimbua, sio kugegedana. Inavyoonekana wewe na mkeo wa kwanza wote hamjitambui. Mimi nimeanza kuongea kuhusu ndoa na wazazi juzijuzi baada ya kuanza kukaribia hiyo hatua.

Mzazi asiyejitambua ni hasara na maumivu kwa mtoto.
 
Kulikuwa na sababu ipi kubwa ambayo mlishindwa kukaa chini na Mkeo mtalikiwa hadi mfikie kutalikiana?

Wake zetu Kuna wakati Wana kera na kutuudhi, lakini kwani hukujua umemwoa binadamu mwenzio nasio Malaika?

Kwani wewe hukuwahi kumkosea Mkeo na akakusamehe mara kadhaa?

Anyways, Kwa maoni yangu ulifanya haraka Kuoa tena mara baada ya kutalikiana na aliyekuwa Mkeo.
Mke agongwe nje bado unaendelea kuwa nae kisa watoto?
 
Back
Top Bottom