5523
JF-Expert Member
- Nov 13, 2014
- 2,275
- 2,410
Sasa kama wewe si muislam na huna mfumo wowote wa maisha unaoamini itakuwa ni vigumu sana kuendelea kujadiliana hapa, wewe si mtu unayeamini chochote hivyo unaishi labda kwa matamanio yako tu na pengine unahusudu mavazi ya kizungu.Kwanza fahamu kwamba mtu asiye muislam sio lazima awe mkristo. Pili fahamu kwamba hizo nguo ndizo zilizokuwa zinavaliwa enzi hizo kwa sababu hakukuwepo na suruali wala gauni sasa kusema kwamba ni mavazi ya kiarabu ni kukosa uelewa tu na kukariri mambo.
Na ndio maana unafikiria kwamba nguo zilizovaliwa muda huo ni kutokana na wakati, akili yako inakupa hivyo kwa sababu ww huamini katika uislamu na pengine huna dini kabisa kwa maelezo yako, lakini nikufahamishe vazi la muislamu limetajwa katika kitabu kitukufu Quran na ndivyo waislam wa kweli wanavyo vaa sasa na hata kwa hao waliopita zama hizo, dini ya kiislam ina apply muda wote haipitwi na wakati ata watakaokuja baada ya 200 years.