Tamaa za pesa zimetuponza Simba, tumesajili kimhemko. Sijasikitika sana

Tamaa za pesa zimetuponza Simba, tumesajili kimhemko. Sijasikitika sana

Joined
Aug 24, 2021
Posts
72
Reaction score
65
Wakuu hii Simba ukiangalia ni mbovu sana hairidhishi hata kuiangalia. Hata tuliposhinda kule Botswana wala sikufurahia jinsi timu ilivyocheza. Hii timu haionekani hata ikitafuta ushindi.

Tulicheza vibaya sana na timu ilionekana kuelemewa basi tu bahati ilikuwa kwetu. Kocha ameshindwa hata kutengeneza combination inayoeleweka.

Nakiri tumesajili kwa muhemko wa kuuza baadae baada ya kuuza Miquissone na Chama, kuna mdau aliniambia bodi inataka iuze wachezaji tena inufaike baadae kwa hiyo imesajili wchezaji kwa kigezo cha umri. Hili nakubali, je kwa Wachezaji gani?

Huyu Sadio Kanoute hamna kitu mule, yuko slow na hana kasi, kumbuka aliachwa kule Libya.

Huyu Peter Banda si mchezaji wa kukupa matokeo bado sana kwa umri na stamina yake.

Huyu Duncan Nyoni yuko na Stamina ila hatumpi nafasi.

Pappe osman Sakho ni mchezaji wa level za kawaida.

Tumeuza wachezaji wawili Quality tumesajili rundo lisilo na Quality.
 
Watanzania mkiacha lawama lawama tutafika mbali sana
 
Mkuu jana man u kala 5 na wachezaji wake wote bora mpira sometimes una dunda kuuza wachezaji simba sio issue messi kaondoka barca na kiwango chake chote kile ile ni timu wacha waje wengine wakina chama
 
Kwamba mkuu hujawahi kuona mtu anauza pikipiki, halafu ananunua helment
 
Mkuu jana man u kala 5 na wachezaji wake wote bora mpira sometimes una dunda kuuza wachezaji simba sio issue messi kaondoka barca na kiwango chake chote kile ile ni timu wacha waje wengine wakina chama
Liver ndio angelifungwa izo 5 ndio ingekua habari sio Manchester kufungwa 5 liwe jambo la kushangaza,ata kwa simba kufungwa imekua habari kwa sababu wengi walishaona mapungufu ya simba walishauli waliongea ila viongoz wakaweka masikio pamba matokea yake ndo aya
 
Wachezaji wote waliosajiliwa no waziri, tatizo makocha wamekariru Bocco, Wawa pia mbinu zao mbovu
 
Pengo la Chikwende linaonekana simba. Ili timu irudi kwenye form, inabidi tuuze Bwalya tumrudishe Kichuya.
 
Wakuu hii Simba ukiangalia ni mbovu sana hairidhishi hata kuiangalia. Hata tuliposhinda kule Botswana wala sikufurahia jinsi timu ilivyocheza. Hii timu haionekani hata ikitafuta ushindi.

Tulicheza vibaya sana na timu ilionekana kuelemewa basi tu bahati ilikuwa kwetu. Kocha ameshindwa hata kutengeneza combination inayoeleweka.

Nakiri tumesajili kwa muhemko wa kuuza baadae baada ya kuuza Miquissone na Chama, kuna mdau aliniambia bodi inataka iuze wachezaji tena inufaike baadae kwa hiyo imesajili wchezaji kwa kigezo cha umri. Hili nakubali, je kwa Wachezaji gani?

Huyu Sadio Kanoute hamna kitu mule, yuko slow na hana kasi, kumbuka aliachwa kule Libya.

Huyu Peter Banda si mchezaji wa kukupa matokeo bado sana kwa umri na stamina yake.

Huyu Duncan Nyoni yuko na Stamina ila hatumpi nafasi.

Pappe osman Sakho ni mchezaji wa level za kawaida.

Tumeuza wachezaji wawili Quality tumesajili rundo lisilo na Quality.
Tuliwaambia mwanzoni kabisa! Lakini mliishia tu kutukejeli. Sasa ni wakati wenu wa kulinywa. Na msiombee mkutane na Prisons au Polisi Tanzania kwenye ligi!

Aisee mtachezeshwa kwata mpaka mkome! Only Wananchi can handle them.
 
Kweli unauza mchezaji bilion nne unarudi kununua mchezaji wa milioni miatatu na bado mnamawazo ya kufika nusu fainali. Banda bado sana kwenye kuforce game, huyo Bwalya mpaka leo sijamuelewa japo huwa anawapumbaza kwenye game za wapinzani wazembe lakini ikija mechi tafu huwa hafurukuti. Huyo morisoni ndio kabisaaa, akipasiwa mipira 15 lazima nane atatafuta kufanyiwa faulo na mitano atafanya faulo na mpira wa dizaini hiyo unapoozesha mashambulizi. Huyo. Tusisahau huo mkanganyiko wa makocha unaweza pia ukachangia kipigo tulichopigwa
 
Kuna agent solution ambayo Kocha wa Simba anaweza kutumia ikamsaidia ...nakubali kuwa chama na miqueson waliibeba Simba lakini hawakucheza wenyewe uwanjani kulikuwa na wachezaji wengine name...wameondoka wawili na wengine wamebaki...so kwanza Hawa wachezaji wageni lazima tukubali quality zao ni za chini labda Duncan nyoni kidogo Hawa wengine hawana stamina na pia kanoute hastahili kabisa kuanza coz Hana stamina na pia Yuko slow so kujenga Simba mpya kupitia Hawa wachezaji ni sawa na kuota ndoto za alinacha...shida ya Simba ni kwenye kupanga timu Kocha akitulia kupanga timu vizuri Simba inaweza kurudi vilevile...Kuna option Kocha akaitumia ya kuwajenga kisaikolojia Morrison na dilunga Hama hata Duncan nyoni kuwa mbadala wa chama na miqueson...wakaungana na rally bwalya...halafu akamtumia mkude ama mzamiru badala ya kanoute na Wawa hakampumzisha alafu acheze inonga na onyango ama Kennedy ...so kikosi kikawa Kama ifuatavyo...mabeki kapombe,zimbwe ,pembeni..inonga na onyango Kati,lwanga na mkude wacheze double pivot..then mbele yao wacheze bwalya...miqueson na ..ama dilunga au Duncan nyoni na mshambuliaji akawa ni kagere...ambapo utakuwa ni 4,,2,3,1...Nina uhakika hundred percent Simba itarudi Kama mwanzoni...kosa tulilofanya ni kusajiri watoto Kama Banda na sakho ambao hawana stamina ..yaani tumepigwa mchana kweupe..
 
Back
Top Bottom