Paspii0
JF-Expert Member
- Apr 10, 2020
- 638
- 1,043
Oprah Winfrey aliwahi kusema,
"Hakuna kinachotutokea kwenye maisha yetu bila kuwa na faida. Hakuna kinachotupata, hata kiwe kibaya namna gani, kinachoishia kupotea bila faida."
Maisha huja na changamoto, huzuni, makosa na maumivu. Lakini katika kila tukio, hata lile la kusikitisha au la aibu, kuna somo kubwa la maisha linalofichwa ndani yake.
"Ulihitaji kuumia ili ukue. Ulihitaji kukosea ili ujifunze."
Makosa hayapaswi kuwa chanzo cha aibu ,bali chanzo cha hekima. Unapokubali kujifunza kutoka kwa makosa yako, hata yale ya kijinga, unakuwa mtu bora zaidi.
Kila kilichokupata ni sehemu ya mpango wa ukuaji wako. Umeandaliwa ili ukue, uelewe, ujue thamani yako, na ujenge misingi imara ya maisha yenye maana.
Wewe ni zaidi ya makosa yako. Wewe ni somo linalotembea. Kila hatua uliyoipiga, hata ilipokuwa ya kurudi nyuma, imekuwa daraja la kukupeleka mbele.
Hivyo, usikate tamaa. Usijilaumu tena. Usiendelee kulalamika. Badala yake, simama. Tazama ndani yako. Jiulize kwa ujasiri: “Ninajifunza nini hapa?” Na hapo ndipo mwanga wako utaanza kung’aa. Hapo ndipo mabadiliko ya kweli huanzia.
~Chavalikungu..!
"Hakuna kinachotutokea kwenye maisha yetu bila kuwa na faida. Hakuna kinachotupata, hata kiwe kibaya namna gani, kinachoishia kupotea bila faida."
Maisha huja na changamoto, huzuni, makosa na maumivu. Lakini katika kila tukio, hata lile la kusikitisha au la aibu, kuna somo kubwa la maisha linalofichwa ndani yake.
Kila Tukio Lina Somo lake kwa undani,….
- Hata machozi yanakuachia somo.
- Hata unapopoteza, kuna kitu muhimu unachojifunza.
- Hata kosa, linapokueleweka vizuri, linakuwa darasa la maisha.
- Jiulize: Kwa nini hili lilinitokea?
- Kwa nini nilifanya kosa hili?
- Ni nini ninachoweza kujifunza kutokana na hali hii?
"Ulihitaji kuumia ili ukue. Ulihitaji kukosea ili ujifunze."
Makosa hayapaswi kuwa chanzo cha aibu ,bali chanzo cha hekima. Unapokubali kujifunza kutoka kwa makosa yako, hata yale ya kijinga, unakuwa mtu bora zaidi.
- Usilalamike tu bali tafakari.
- Usijilaumu tu bali jiulize ulijifunza nini.
- Usikimbie makosa yako bali yakumbatie kama walimu.
Maisha hayaendi kwa bahati mbaya. Kila tukio,jema au baya, la furaha au la huzuni, tambua limebeba ujumbe wa kukupeleka mahali ulipokusudiwa kufika.Kila kilichokupata ni sehemu ya mpango wa ukuaji wako. Umeandaliwa ili ukue, uelewe, ujue thamani yako, na ujenge misingi imara ya maisha yenye maana.