Paspii0
JF-Expert Member
- Apr 10, 2020
- 638
- 1,043
"Busara ni zawadi ya wale wanaojua thamani ya ukimya, na uzito wa maneno."
Katika maisha ya kila siku, tunakutana na watu wengi , familia, marafiki, majirani, au hata wageni. Mara nyingine tunadhani tunazungumza kwa upendo, lakini kwa bahati mbaya, maneno yetu huacha majeraha yasiyoonekana.
ZINGATIA KWA UMUHIMU; Kuna maswali ambayo ni vyema kuyaepuka kabisa, hata kama nia yako ni njema,
FIKIRIA KABLA YA KUULIZA ,TAMBUA KUSIKILIZA NI FUNGAO LA BUSARA.
Usikimbilie kutoa kauli kwa kutegemea mtazamo wako binafsi wa maisha.
Labda,
USIMHUKUMU MJA KWA KILE USICHOKIJUA.
"Siku moja, kuna kijana aliunganishwa na schoolmates kupitia group la WhatsApp. Wakati mazungumzo yanaendelea, bila kufikiri sana akauliza mwenzake, kuwa ana watoto wangapi?’ Alidhani ni swali la kawaida. Yule dada alinyamaza, kisha akaondoka kwenye group. Baadaye watu wakafahamu alikuwa akipitia changamoto kubwa sana ya uzazi. Nawalijisikia vibaya mno… hapo tunajifunza ,kuwa ukimya wa mtu si mara zote ni chuki ,mara nyingi ni kinga.
TUCHUKUANE KWA HURUMA.
Watu wengi hujitenga si kwa sababu hawapendi watu, bali hulinda amani ya mioyo yao dhidi ya maswali yenye kuumiza au kejeli zisizo na sababu.
Mtu anapokuja kukusalimia, mpokee kwa moyo wa upendo, si kwa mfululizo wa maswali kama mahojiano.
Kuwa mtu wa faraja, si wa mashindano.
Kuwa wa kutia moyo, si wa kuvunja moyo.
MAISHA SI MASHINDANO.
Kila mmoja wetu ana mzigo wake wa siri, wengine kiuchumi, wengine kihisia, wengine kimahusiano au kiafya.
TUSIONGEZE UZITO KWA NDUGU ZETU KWA MANENO YETU.
Mdomo wako unaweza kuwa baraka au sumu , chagua kuwa baraka.
~Chavalikungu.!

- "Mbona hujaolewa bado?"
- "Kwa nini huna watoto?"
- "Utazaa lini? Umri unaenda!"
- "Unafanya kazi gani?"
- "Mbona umenenepa? Mbona umekonda hivi?"
FIKIRIA KABLA YA KUULIZA ,TAMBUA KUSIKILIZA NI FUNGAO LA BUSARA.
Usikimbilie kutoa kauli kwa kutegemea mtazamo wako binafsi wa maisha.
Labda,
- Mtu huyo amevumilia miaka mingi ya maumivu ya ndoa au utafutaji wa mwenza.
- Labda amepoteza mimba au amekuwa kwenye safari ngumu ya kupata mtoto.
- Au pengine amepoteza kazi, au hana kabisa , lakini anapambana kwa kila njia.