KERO TAMISEMI Dodoma Kuna nini, naomba kujuzwa wadau

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Kindo Sila

Member
Joined
Jun 22, 2024
Posts
6
Reaction score
6
OR TAMISEMI, Dodoma kuna nini, naomba kujuzwa wadau. Mimi ni mmojawapo wa watumishi niliopata uhamisho toka kwa Katibu Mkuu TAMISEMI, nikihamia HALMASHAURI nyingine. Cha kushangaza, tangu kuripoti kituo kipya mwezi Oktoba 2023, bado CHEKI namba kwenye MFUMO wa UTUMISHI (ESS) inasoma kwa Mwajiri wa zamani.

Afisa Utumishi wa sasa, anapoingia kwenye MFUMO wa watumishi wake ESS, hanioni. Afisa Utumishi wa zamani yeye anasema wewe ulishahama nenda kwa kwa Mwajiri wako, taarifa za kuhama nilishatuma TAMISEMI.

Wadau naomba kujua, nini tatizo TAMISEMI

Pia soma
- Ofisi ya Rais – TAMISEMI Special Thread: Karibu tukuhudumie, tupe Maoni, Maswali, Mapendekezo na Malalamiko
 
OR TAMISEMI Ujumbe wenu huu
 
Umejaribu kwenda Ofisini kuulizia swali hili au unakimbilia mtandaoni kwanza..
 
Kwahio wamepiga pin kamshahara?? Vi pepmis? Pole sana
 
Naomba kufahamu, MSHAHARA KUTOHAMISHWA kwenda kwa Mwajiri mpya baada ya kuhamisha Mwaka 2023 kwenda HALMASHAURI nyingine.

Shida Nini, HR wa zamani ukimfuata anasema wewe siyo mtumishi wangu TAARIFA ZAKO ZA UHAMISHO nimeshatuma Dodoma TAMISEMI.
 
Watumishi wamehamishwa tangu mwaka jana November hadi leo taarifa zao na mishahara haijahamishwa hadi leo hivyo wanakosa haki zao za kiutumishi
 
Tatizo mifumo ni migeni kwa hao maafisa utumishi....Pole sana nchi iliharakia mambo, matokeo yake 😳😳😳.

Mfano.

Watumishi waliambiwa watumie mwaka wa fedha 2023-2024 imefika june 2024 majukumu yamefutika yote ya mwaka mzima.

Matokeo ni kuanza upya ujazaji majukumu...😂😂😂😋😂😂
 
Naomba kufahamu, MSHAHARA KUTOHAMISHWA kwenda kwa Mwajiri mpya baada ya kuhamisha Mwaka 2023 kwenda HALMASHAURI nyingine.

Shida Nini, HR wa zamani ukimfuata anasema wewe siyo mtumishi wangu TAARIFA ZAKO ZA UHAMISHO nimeshatuma Dodoma TAMISEMI.
Mshahara si unaendelea kupata kupitia mwajiri wa zamani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…