TAMISEMI imemwajiri Babu Lembrice Peter kwa kutumia namba ya kidato cha nne ya mtu mwingine

Wahusikaa watakua wameshafikiwa na hizi taarifa.....lakini wew mkuu hebu tuambie ulianza vp kuling'amua hili Jambo??? Au Kati ya hao wawili mmoja ni mtu mnae fahamiana nae!!?? Au ww ni mfanyakazi Tamisemi!!??


Yote kwa yote mkuu una chembechembe za wivu kwa msela.....!!
 
TAMISEMI ni watu kama wewe.
Wanafamilia na ndugu pia.
Kuwa ni wewe uko kitengo muhimu kama tamisemi na BABU ndo awe mpwao mtoto wa dada ako unamuachaje kwa mfano
Utakuwa huna akili kabisa kumpendelea mtu, mwache ashindane kwa sifa.
 
serikali hii unaifuatilia mambo yake utakufa kwa presha
 
Sijaona logic,mtu anaweza kupata F zote lakini akaamua ku reseat na akapiga fresh na kusonga mbele.Namba ambayo huwa inatambulika ni ile ya awali alopiga F, hizo namba za ku reseat huwa zinaambatanishwa tu wakati wa maombi
 
Acha roho mbaya, huo unaofanya ni zaidi ya ushetani, akipata ajira wewe unaumia nini? na kwa nini umfuatilie mtu mmoja tu?
Unatao majibu mepesi kwenye hoja nzito.
Hapa kuna watu watapoteza kazi.
Makosa ni mengi mno.
 
Hayo majina yakichunguzwa sana utakuta namba ya mtihani ya binti aliyehitimu kidato cha nne imetumika kwa Me.
 
WanaJF tumesahau kwamba TAMISEMI walipokea maombi ya ajira hizi kwa njia Mtandao, yaani hawakupokea bahasha bali Soft copy via Developed system, kwahiyo mifumo yetu ya Computer, Ukifanya Gabbage In itakupa Gabagge Out. Waombaji waliingiza Taarifa chafu/za Uongo na mfumo pia Umetoa taarifa chafu za Uongo. Ni haki yetu kuwahukumu lkn pia Upande wa pili inatoa picha ni kiasi gani hatuko makini tunapoombakazi.

Mind you, TAMISEMI haijawaajiri hao, BALI WAMEITWA KAZINI, huko Halmashauri walikoitwa kuna UKAGUZI WA VYETI NECTA, UHAKIKI WA MAJINA nk nk kama huna Sifa hupenyi ng'oooo
 
​
Hii ni kweli watu watapigwa chini wengi Sana.
 
Tamisemi walikuwa na msemo,wanasema kuwa "kama hujatoa pesa hulambi maji"
 
Mkuu naona unamchome mtu utambi hapo.
alitembea na mkeo nini?
 
Mkuu watu wapo kimaslahi zaidi kipindi hiki. Kama waliomaliza form Four 2019 wameajiliwa, watashindwa kufanya hilo?
 
Sijaona logic,mtu anaweza kupata F zote lakini akaamua ku reseat na akapiga fresh na kusonga mbele.Namba ambayo huwa inatambulika ni ile ya awali alopiga F, hizo namba za ku reseat huwa zinaambatanishwa tu wakati wa maombi
Kama ali reseat jina lisingebadilika, lingekuwa lilelile
 
Halmashauri nyingi, nafuu Tamisemi, uwezo wa uhakiki ni mdogo, Tamisemi Wana access na NECTA wakati halmashauri wanakagua kwa macho, kudanganywa ni rahisi, hata wafanyakazi waliotumbuliwa sio halmashauri, ni tume maalumu ilipita Kila halmashauri.
 
No kweli kabisa walipata wote wana watu was huko sisi tumekoma watu wa kuwasidia jamaa zetu tufanye?
 
Hao uliosema washirikishwe kwenye kuchunguza hili wao ndiyo walikua wapishi wa taarifa feki za majina ya wapiga kura kwenye orodha ya wapiga kura wa zanzibar.

Serikali ya CCM imefitinika kila idara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…