TAMISEMI kupangia watoto waliomaliza kidato cha nne kujiunga na vyuo

Unawazungumzia kwani ktk familia zao unawalisha wewe?? Kwanini hukutoa elimu kwa hao unaowafamu kuwa kwa uwezo wenu msiombe vyuo? Wewe uliyesikia tangazo kutoka TAMISEMI kuwa walitoa taarifa kwanini hukuwafikishia mzee? Nikafikiri ni google jina lake, ada unaweza kukuta anasomeshwa na kanisa kisa wewe hujiwezi. Mwisho kabisa kama waliomba f5 wakapangiwa vyuo basi tahasusi huenda hazikubali au USIMUAMINI mtoto kwa kukuambia kuwa sikuomba. Uzushi hatutaki nenda tamisemi kajihakikishie alichoomba
 
Shida za course za tourism ni connection na ukimalza lazma usome lugha hata 2 ten na usome driving licence C.
Baadhi ya kozi ambazo zimewekwa na serikali ni kupoteza mda zikiwemo Kozi zote Za CBE za diploma na certificate za NIT Tourism za ualimu nk. hazina ajira kabisa mtu kasomea CPA wa degree anazunguka mitaani kusaka ajira sembuse we wa certificate, kibaya zaidi kwanini aserikali emedhoifisha shule za advance private wakati wenyewe hawana uwezo wa accommodate wanafunzi wote walio maliza O'level, hapo nikama kuua future ya watoto wa Tanzania, ili waweze kutawaliwa bila pingamizi.
 
Wasingewapangia angelalamika. Wamepangiwa amelalamika. Always, the opposite is better!
Hata bila kupagia unaenda tu pale unapewa nafasi ili mradi una ada yao ya 700k au 1m af ungaike na hostel chakula na stationery, saerikali inakwepa majukumu yake tu.
 
Hata bila kupagia unaenda tu pale unapewa nafasi ili mradi una ada yao ya 700k au 1m af ungaike na hostel chakula na stationery, saerikali inakwepa majukumu yake tu.
Kwenye suala la elimu ya watoto wangu napambana kivyangu. Sina muda wa kuangalia sijui Serikali hivi Wala Serikali vile. Ndio maana mimi na watoto wangu hatushobokei mikopo ya HLSB. Napambana kivyangu hata wakilala njaa wanajua!
Wewe endelea kuzaa na kuilaumu Serikali!
 
Hongera mkuu naona uko vizuri kabisa.
 
Unataka aende advance akapoteze mda si kila kitu kulalamika
 
Hongera mkuu naona uko vizuri kabisa.
Hapana. Nimesema napambana. Pia mimi sio muumini wa kuombaomba. Nafurahia maisha niliyonayo na watoto wangu. Pambana achana na mikopo, sijui ada kubwa. Kwani LAZIMA wasome kama huna hela?
 
Yaani mtu ana division3 yake nzuri unampangia kigoma kasome Meteorology, Ada 1m..... Lo!
 
NENDA WEBSITE YAO ANGALIA VYUO VYA VETA VYENYE BAORDING VIKO KIBAO
Wewe kazi ilikuwa ndogo tu,sema VETA CHANG'OMBE, boarding.
Ada na michango yote jumla 260000/- kwa mwaka.
Lkn badala yake unakuja na website.
Acha uzembe mkuu,somesha mtoto wako huo ni wajibu wako.
 
Taaluma ni gharama, hata kama angeendelea na A level, mwisho wa siku angekumbana na chuo kwa gharama hizohizo,
Muhimu ni serikali ingewapa mikopo ili kuwawezesha wapate elimu. Lakini kusema vyuoni walipe 80k kwa mwaka si rahisi kulingana na level ya elimu inayotolewa, unless kama unataka elimu ya juu iharibike kwa wakufunzi kulipwa mshahara mdogo.

Mimi hii case ilinikuta mwaka jana kwa dogo, imebd nikubaliane na mazingira dogo aendelee na skuli.

Ila kiukweli, wazazi wengi huko vijijini wana uwezo kabisa wa kulipa hizo gharama, shida yao moja hawataki kuwekeza kwenye elimu, ila matukio mengine ya kijamii wamo sana.

Chuo saa hii unapewa control number, unalipa mdogomdogo.

Familia zetu zamani hawakuwa na ajira rasmi ila walisomesha watoto mpaka vyuo vikuu kwa kuuza ndizi na kahawa.

Mtu kalima tumbaku, anapata hela nyingi ila hawezi somesha mtoto, na kujifanya masikini, haya mambo nayashuhudia sana.

Kwahiyo shida ipo kwa wazazi, mtu akiamua anaweza. Tusipende sana mteremko kwa vitu vya msingi.

Suala la elimu nio hulka ya mtu tu, kuna watu wana mang'ombe mengi ila watoto wanaishia kuchunga.
 
Naomba link kuona majina ya waliopangiwa
 
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2026-06-10 at 12.50.46 AM.jpeg
    78.1 KB · Views: 11
CC: Professor Ridhiki Shemdoe

Jambo Nyeti Na Muhimu
October Siyo Mbali Fuateni Ushauri Uliotolewa
Vinginevyo Baadhi Ya Wazazi Watashindwa
VYUO Vitakosa Wanafunzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…