TAMISEMI: Mfumo wa kusoma madeni ya parking ulipata hitilafu ukashindwa kutuma ujumbe kwa wenye magari

TAMISEMI: Mfumo wa kusoma madeni ya parking ulipata hitilafu ukashindwa kutuma ujumbe kwa wenye magari

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kulalamika kuwa kuna utaratibu mbovu unaendeshwa na watu wanaohusika kukusanya madeni ya maegesho ya magari, mamlaka zimetolea ufafanuzi malalamiko hayo.

Mdau huyo alidai wahusika wanatega njiani, wanasimamisha gari na kumfuata Dereva wakiwa wengi katika hali ya kumtisha, wanamtaka alipe deni papohapo, hata kama sio deni halisi wao hawajali na kuwa wanasababisha foleni katika maeneo ya oparesheni zao.

Kumsoma Mdau bonyeza hapa ~ Wanaohusika kudai fedha za ‘parking’ kwa kusimamisha magari barabarani, wamekuwa kero kwa Wananchi!

UFAFANUZI WA SERIKALI
Mwalimu Kibasa kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, ndiye Mratibu na Msimamizi wa Zoezi la Kukusanya Madeni ya Maegesho ya Magari Mkoa wa Dar es Salaam.

MADENI YA PARKING DAR NI ZAIDI YA TSH. BILIONI 12
Kibasa anasema madeni yaliyopo kwa sasa Mkoa wa Dar es Salaam ni makubwa na lazima zifanyike njia za kuweza kukusanya. Anaeleza:

Mfano Ilala madeni ni Tsh. Bilioni 7.5, Kinondoni ni Tsh. Bilioni 2.6, Temeke Tsh. Bilioni 1.2, Ubungo Tsh. Milioni 604 na Kigamboni ni Tsh. Milioni 371.

Zoezi hili la kukusanya madeni limeanza Juni 19, 2024, hadi kufikia Juni 28, 2024 tumekusanya zaidi ya Tsh. Bilioni 1.1 kwa Dar es Salaam.

Mchakato ni kuwa tunatakiwa kukusanya kwa wingi inavyowezekana na bila kuwakera watu tunaokusanya madeni kwao.

Magari ambayo yataruhusiwa kuendelea na safari wakati wa ukaguzi ikitokea tumewakmata wahusika na wana madeni ni kama gari lina mgonjwa ambaye anatoka au anaenda Hospitali, pili ni kama mhusika ana mtoto mdogo, sio mtoto ambaye yupo darasa la pili au kuendelea, tatu ni walio katika msafara wa msiba.

Pamoja na hivyo, kuwaachia haitamaanisha watasamehewa madeni, wataachiwa lakini wataambiwa wanatakiwa kulipa.

SABABU ZA KUWA NA WATUMISHI WENGI WAKATI WA KUDAI
Mchakato unahusisha magari mengi na hivyo lazima Watendaji wawe wengi pia, kuna wakati tunaweza kusimamisha magari zaidi ya 20, hivyo, kukwepa kusababisha foleni tunakuwa na Watumishi wengi.

Ukilipa utaondoka, kama hautalipa tutabaki na wewe ili tuendelee na mchakato hadi jioni ambapo tutakuwa tunakamilisha kazi.

Hatuwezi kubeba gari la mtu, tutamruhusu aondoke muda wa kazi ukiisha hadi kufikia mtu aweze kubebewa gari lake ni anapokuwa mbishi na hataki kuelewa.

Tunaambatana na Auxiliary Police pamoja na Mgambo katika zoezi letu.

MAGARI YA SERIKALI HAYADAIWI ISIPOKUWA IKIWEKWA NAMBA BINAFSI
Ukiwa na gari la Serikali ambalo umebadilisha namba ukaweka ya binafsi ambayo inadawa, sisi tutakusimamisha na kukutaka ulipe, tunachoangalia ni namba ambayo inadaiwa.

Wapo ambao tunawasimamisha (wakiwa na magari ya Serikali) wanagoma kulipa kwa kuwa yale ni magari ya Serikali, sisi tunakomaa nao na kuwataka walipe hata kama wao hawahusiki na deni la hiyo namba.

Maelekezo tuliyopewa kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI kuwa tukakusanye madeni, hakutoa maelekezo kuwa ikija gari fulani inayodaiwa tuiache.

Magari yenye namba za Serikali yenyewe hatuyadai kwa kuwa ni muongozo wa Sheria ilivyotungwa Bungeni.

Hivi karibuni wakati mchakato ukiendelea tulipata shida kidogo na gari ya Wizara ya Afya, tuliikamata, wahusika wakaanza kupigapiga simu huku na kule, wakataka kuanza kutupa maelekezo, mimi nipo ‘site’ kwenye kazi kisha unataka kunifundisha kazi, hapo ndipo walipokosea.

Tuliikamata gari hiyo na kuizuia kwa siku tatu lakini mengine yote yanakwenda kwa uzuri.

MFUMO ULIKUWA NA CHANGAMOTO
Sisi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Fedha na GePG ndio tuliotengeneza hii mifumo ya kukusanya fedha na ndio wamiliki, Kuna kipindi ilikuwa na changamoto ikawa haitumi meseji, Watu wakawa hawatumiwi meseji, huo ndio ukweli.

Mifumo ilianza kutotuma meseji tangu Juni 2023, hivyo kuanzia hapo Watu wakawa hawapati meseji.

Kipindi cha nyuma Mwaka 2022 hadi 2023 Watu walikuwa wanapata meseji. Madeni tunayokusanya yanaanza Julai 1, 2022 kuja huku.

KUHUSU KUWABAMBIKIA MADENI
Sio kweli, tunaokutana nao kwenye ‘site’ tunazungumza na tunaelewana, mfumu huu unakuonesha uliegesha gari sehemu gani, muda na hata picha kama utahitaji.

Tunao uwezo wa kuangalia picha iliyowekwa pale ni picha halisi au ilikuwa ‘screenshot’, tunao uwezo wa kuangalia kifaa kilipo.

WAPO WANAOCHEZEA MIFUMO
Hii kazi ya kukusanya madeni imekabidhiwa kwa makampuni, tunao vijana ambao sio waadilifu, kwa kuwa kuna malengo, ikitokea hawajatimiza lengo la makusanyo, anaingia kwenye stoo ya picha zake anajaza kuwa gari fulani liliegesha hapo ila sio ukweli.

Kupitia vifaa vyetu tunaweza kubaini tarehe ya kupiga picha na tarehe ya deni husika, hivyo tukibaini hakuna uhusiano wowote hapo tunatambua kuwa deni sio halisi.

Hatutaki kurudia makosa ya aina hiyo, ndio maana tunakuja na mfumo mpya kuanzia Julai Mosi, 2024 katika Mwaka huu wa fedha (2024/25).

Kwa hiyo kwa hizo changamoto zilizotokea mtu anatakiwa kulipa kisha kwenda Manispaa na kueleza changamoto hiyo.

GARI ILIBAMBIKIWA DENI LA MILIONI MOJA
Kuna Daladala ipo Kigamboni, ilibainika kuwa na deni la zaidi ya Tsh. Milioni moja na maegesho yake yakasoma yapo Mabibo Sokoni.

Nilipozungumza na mwenye gari akasema gari yake haijawahi kufika Mabibo Sokoni, tukawaambia watu wa mfumo waangalie, ikaonekana kuwa kule Mabibo sokoni namba ya gari inasoma ni yenyewe lakini gari linaloonekana ni Lori na sio Daladala husika.

Hivyo, inavyoonekana kuna wahuni ‘walio-crop’ namba ya gari na kuiweka kwenye picha ili gari isomeke ni hiyo lakini kilichosaidia kubaini hilo ni picha za magari kuwa tofauti.

Hivyo, wapo vijana ambao sio waadilifu kweli na kuna mahali hawajafanya kwa usawa, tunawtafuta hao ili hatua zichukuliwe.

MASHINE ZINATAKIWA ZISOMANE
Changamoto nyingine ni kuwa kuna mashine ambazo zikifanya kazi mfano Ubungo kiwango cha gharama ya kuegesha kinatakiwa kusoma hapohapo Ubungo, kifaa hicho kikienda sehemu nyingine ambapo gharama ya kuegesha ni tofauti kinaweza kushindwa kutambua mabadiliko hayo, hivyo kusababisha usumbufu na kuendelea kuingiza gharama za Ubungo.

Tunachokifanya kuelekea Mwaka Mpya wa Fedha tunatakiwa kuweka maboresho ya vifaa hivyo visomane, yaani kama kifaa kinatumika Ubungo kiendelee kubaki hapohapo siku zote, kama kikihamishwa kiwe na uwezo kuwa kusoma gharama kulingana na mazingira husika.
 
Okay, na issue ya gari namba Z au namba F kuonekana na deni? Nimejaribu kucheki semi-trailer nimekuta nayo inadeni inaonekana ilipark town mjini. Nimesearch gari moja lilipata ajali nimekuta lina deni la mwezi wa sita. Sijui mnatuonaje.
 
Okay, na issue ya gari namba Z au namba F kuonekana na deni? Nimejaribu kucheki semi-trailer nimekuta nayo inadeni inaonekana ilipark town mjini. Nimesearch gari moja lilipata ajali nimekuta lina deni la mwezi wa sita. Sijui mnatuonaje.
Hawa jamaa wameweka madeni automatically?
 
Huo mfumo kuanzia juu kuja chini ni wa kihuni tu

Ova
 
Back
Top Bottom