msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 863
- 1,534
Katika jitihada za kupunguza tatizo la upungufu wa watumishi wa afya, serikali kupitia wizara ya afya imezindua mpango maalum wa kuajiri kwa muda wahitimu wa kozi mbali mbali za afya ambao watakuwa wanafanya kazi kwa kujitolea katika hospitali na vituo vya kutolea huduma
Ni mpango mzuri kwani nje na kuwajengea uwezo na uzoefu kitaaluma, utasaidia pia kupunguza tatizo la uhaba wa watumishi wa afya lililopo nchini
Kwakuwa pia kuna tatizo la upungufu wa walimu hususani wa masomo ya sayansi na hesabu si vibaya wizara ya elimu na Tamisemi kuiga mpango huu mzuri ili kupunguza tatizo la uhaba wa walimu mashuleni
Mpango huu wa kuwapata walimu wa kujitolea unaweza kufikiwa kwa kuwashirikisha wadau mbali mbali wa elimu, wafanyabiashara na pia halmashauri kutenga kiasi cha asilimia ya mapato yake kwaajili ya kuwalipa walimu hao ili waweze kujikimu kwa mahitaji ya kila siku
Baada ya utaratibu huu kuwa rasmi ndipo serikali itumie kigezo cha kujitolea kama kipaumbele cha ajira kuliko hali ilivyosasa ambapo utaratibu haujawekwa bayana na shule hazina uwezo wa ku-accomodate hao walimu