DOKEZO TAMISEMI tusaidieni, tunakufa njaa kwenye vituo vya kazi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

chriper

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
347
Reaction score
454
Habari zenu wadau.

Bila shaka mpo poa aisee, mimi sitochoka kuongea tafadhari ebu wizara husika kupitia vyombo kama PCCB piteni kwenye ma halmashauri ya wilaya mkague pesa za kujikimu.

Tunapitia mazingira magumu jamani toka tulivyoripoti makazini binafsi hata sh.100 sijapewa. Hata ule msaada kutoka tu kwa mkuu wangu wa kituo cha kazi nimeomba sijapata nimejarbu kupiga simu na kutuma sms kwa mkuu wa kazi ngazi ya wilaya na kupiga simu na kutuma sms kwa katibu sijibiwi lolote.

Naishi mazingira magumu nalala chini nipo kwenye wilaya yenye baridi 24 hrs hebu, fikiri halafu nalala kwenye sakafu ambayo natandika shuka moja jingine najifunika.

Dumu moja la maji ni sh.600 hapo sijazungumzia chakula n.k

Nimeshakula sana kwa staff wenzangu hadi naona aibu sasa.

Najua nitaonekana muongeaji sana lakini ngoja niongee huenda nikawasaidia wengine walioshindwa ongea.

Jamani tusaidieni tupate pesa ya kujikimu tena iwe yote kwa pamoja maana nimesikia hii wilaya wanatoaga mara 100,000/= mara sh. Kadhaa mwisho wa siku wanaishia njiani hawajakamilisha hiyo pesa.

Kwa ufupi upande wangu naishi maisha magumu sana hata nashindwa kuelezea yote kwa ujumla.

NAJUA HUMU MPO MPAKA VIONGOZI TUSAIDIENI JAMAN.... [emoji120]🥹
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Usicheke mkuu ILA CHEKA SANA KAMA AYAJAKUKUTA USIONBE YAKUKUTE LAZIMA UTASIMULIA..toka nilivyo kula usiku sijala tena naratiba ya kula usiku to usiku tu.🥹 Sio poa.

Sent from my TECNO KI7 using JamiiForums mobile app
 
Habari zenu wadau.

Bila shaka mpo poa aisee, mimi sitochoka kuongea tafadhari ebu wizara husika kupitia vyombo kama PCCB piteni kwenye ma halmashauri ya wilaya mkague pesa za kujikimu.

Tunapitia mazingira magumu jamani toka tulivyoripoti makazini binafsi hata sh.100 sijapewa. Hata ule msaada kutoka tu kwa mkuu wangu wa kituo cha kazi nimeomba sijapata nimejarbu kupiga simu na kutuma sms kwa mkuu wa kazi ngazi ya wilaya na kupiga simu na kutuma sms kwa katibu sijibiwi lolote.

Naishi mazingira magumu nalala chini nipo kwenye wilaya yenye baridi 24 hrs hebu, fikiri halafu nalala kwenye sakafu ambayo natandika shuka moja jingine najifunika.

Dumu moja la maji ni sh.600 hapo sijazungumzia chakula n.k

Nimeshakula sana kwa staff wenzangu hadi naona aibu sasa.

Najua nitaonekana muongeaji sana lakini ngoja niongee huenda nikawasaidia wengine walioshindwa ongea.

Jamani tusaidieni tupate pesa ya kujikimu tena iwe yote kwa pamoja maana nimesikia hii wilaya wanatoaga mara 100,000/= mara sh. Kadhaa mwisho wa siku wanaishia njiani hawajakamilisha hiyo pesa.

Kwa ufupi upande wangu naishi maisha magumu sana hata nashindwa kuelezea yote kwa ujumla.

NAJUA HUMU MPO MPAKA VIONGOZI TUSAIDIENI JAMAN.... [emoji120]🥹
Ushaanza kulia njaa mapema hivi.

Ulitakiwa ujiandae hela ya serikali sio ya kuipigia mahesabu.

Pambana ukope kwa ndugu jamaa na marafiki.
 
Taja jina la wilaya na kituo cha kazi mara moja.
Ni halmashauri gani hiyo yenye baridi 24hrs/week halafu maji ni sh 600/dumu? Njombe, Arusha, Ngara, Makete na kwingineko serikali ilishamaliza kero za maji na umeme siku nyingi. Wapi huko unakokulalamikia?
 
Back
Top Bottom