TAMISEMI/UTUMISHI saidieni watumishi walipwe haki zao pindi wanapohamishwa vituo vya kazi

TAMISEMI/UTUMISHI saidieni watumishi walipwe haki zao pindi wanapohamishwa vituo vya kazi

Majwahis

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
575
Reaction score
545
Ni kawaida sana kwa Mtumishi anapohamishwa kituo Cha Kazi uchelewa/kutolipwa kabisa gharama za kujikimu na kubeba Mizigo kwenye halmshauri nyingi.

Mtumishi anakaa miezi 6, mwaka au zaidi bila kulipwa! Kuna mwingine alilipwa kidogo kidogo kwa miaka 5, kweli hii ni aibu na kumdumaza Mtumishi. Ndiyo maana wanatembeza bodaboda kuitafuta hela! Ndiyo, mmempeleka ugenini atamudu vipi maisha na familia?

Nashauri Serikali, kuweka bajeti ya uhamisho Tamisemi mtu anapohamishwa mnamtumia na hela yake ya kujikimu.

Halmshauri hizi makandokando ni mengi hadi kero; wako kilocal zaidi.
 
Walimu mna laana ambayo hata shetani amewalaani pia, subiri mpate joto la jiwe shenzi zenu
 
Sheria ni usiondoke mpk ulipwe stahiki zako otherwise ulihama kwa hiari au makubaliano ukayaridhia!
 
Fahamu haki na wajibu wako kama mtumishi na wa mwajiri wako,usihame bila kulipwa,ukiwachekea hao watakuumiza hela wanazo sema priority.
 
Back
Top Bottom