TAMISEMI wametangaza ajira za afya leo kupitia Sekretarieti ya Ajira, sasa ni mwendo wa Interview

Sasa kuna kada hazina watu kabisa.

Mfano EN(nurse certificate)
Karibia wengi waliajiriwa miaka ya hivi karibuni.

Halfu utaratibu wao wa tamisemi zamani ulikuwa unazingatia First in first Out.

Hauoni kama hii itapelekea waliomaloza hivi karibuni wengi kuwa kwenye utumishi wa umma ilhali walimuda mrefu wameshindwa kupata chance ya kufaulu usaili.
 
PSRS wana vigezo wa kuchagua watu na kuwapa nafasi za kazi.

Mojawapo ya kigezo ni umri.

Kivipi umri utazingatiwa: Endapo marks za ufaulu wa oral zikafanana, umri utaangaliwa halafu mwenye umri mkubwa atapatiwa nafasi.

Hivyo hivyo kuna vigezo vya jinsia, ulemavu. Kwenye jinsia Ke atapata nafasi endapo amelingana marks na Me ila hapa nafikiri(sina uhakika) umri lazima uwe/karibia sawa.
 
Halfu mambo yako ovyo sana mkuu mm mwaka jana nimepambana oral mwaka jana afya tulikuwa written 1000+ oral 120 mpaka leo mwezi wa kumi hata watu 50 hawajachukua na database ina expire mwezi ujao.
 
Halfu mambo yako ovyo sana mkuu mm mwaka jana nimepambana oral mwaka jana afya tulikuwa written 1000+ oral 120 mpaka leo mwezi wa kumi hata watu 50 hawajachukua na database ina expire mwezi ujao.
 
Hapo kuna wengine tuna umri mdogo ila tumemaliza muda mrefu na tushapambana sana na ma interview hayo.

Kiuhalisia mimi ni mtu ambaye nina imani sana na utumishi.

Ila mara baada ya kufanya written kadhaa na oral Pasi na mafanikio hali iliyopelekea kuchukua sana hii michakato.

Kiukweli mimi sio kwamba naogopa interview ila Mfumo wa kuajiri utumishi umeniondolea imani.
 
Asante sana mkuu kwa majibu yako nashukuru baada ya kurudi kuangalia tena nimekuta tayari document nilizopakia zikiwa verified zikionekana

Swali langu la mwisho hivi hawa mareferee watatu ni kweli huwa wanapigiwa simu?

Maana kuna mareferee unaweza waweka kwa nia nzuri tu wakaamua kukukanda wakipigiwa simu badala ya kukupa maua yako.

Natanguliza shukrani
 
Umri bado mdogo hata kama ushamaliza chuo muda mrefu, hauwezi kufanana na mwenye umri mkubwa katika kipindi cha Utumishi wa Umma.

Huyo mwenye umri mkubwa atawahi kustaafu kabla yako, hivyo anatakaiwa kuingia kwenye Utumishi wa Umma kabla ya wewe.

Kitu pekee kitakachokuokoa ni kufaulu Oral kwa Alama za Juu. Wapo waliopita kwa namna hii wengi tu
 
Naskia hua hawapigiwi simu ila wape taarifa tuu hao referee wako kabla ya kuwaweka.
 
Sijawahi kusikia PSRS wawapigie referee
 
kuna rafiki yangu kasahau password za ajira portal na alikuw ashajisajili mwanzo na akibonyez forgrt password hapokei respond yeyote huyu anasaidikaje??
 
 
Habari za muda huu ,nimejaribu kurepost passport size niliyo attach kwenye profile yangu. Shinda ni kwamba kuna background inaonekana nyuma yenye rangi ya karatasi ya kaki mbali hii hii imekaaje? Iko sawa au hiyo background ya nyuma zaidi iyo ya kaki haikutakiwa hapo na nimefanya juu chini kubadilisha picha imegoma
 
Hiyo background sio sahihi kaka
 
Em jaribu kama una-crop hy picha
 
Tafuta picha ambayo ni nzuri kabisa, backgrou ya blue/blue bahari.

Usikubali kuja kutokuwa shortlisted kwa mambo madogo madogo kama hayo
 
Tafuta picha ambayo ni nzuri kabisa, backgrou ya blue/blue bahari.

Usikubali kuja kutokuwa shortlisted kwa mambo madogo madogo kama hayo
Hapa naongezea ikibidi atumie ila app ya kutengenezea passport mimi niliitumia

Nilipiga picha nyuma ya shuka la blue ile app ikanisaidia kupata passport makini sana tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…