TAMISEMI wametangaza ajira za afya leo kupitia Sekretarieti ya Ajira, sasa ni mwendo wa Interview

TAMISEMI wametangaza ajira za afya leo kupitia Sekretarieti ya Ajira, sasa ni mwendo wa Interview

Ajira za afya zina interview?? 1.umefanya internship mwaka mzima 2. umefanya mthiani wa leseni alafu bado ufanyiwe interview???
Acha kukariri, Engineer hawana Leseni? Vip CPA za wahasibu,vip kuhusu Wanasheria wanapita Law school? Hao wote wanafanya interview kwenye ajira zao..hata Ajira za afya kipind cha nyuma ili ufanye kazi Muhimbili,mtu alitakiwa afanye Interview.
 
Address za kupokelea(receiver's address) ni zipi? Maana kila mkoa imetangaza ajira zake

Sent from my Pixel 3a using JamiiForums mobile app
.
Screenshot_20240707-173506.jpg
 
Hivi ndivyo watanzania tunavyotafutiana ulaji. Wakili/mwanasheria anaenda kupiga pesa mno. Kama huna elfu 5000/10000 katika Kila cheti, aise mtanzania mwenzangu jobless huombi hizi nafasi za kazi. Hivi hiki kipengele Cha kuwatafutia ulaji mwakili na wanasheria wetu hakiwezi kuondolewa?
 
Sio lazima kwenda kwa mwanasheria.. vyeti vyenyewe vimethibitishishwa hakuna haja ya mwanasheria
 
Habari.

Hatimaye Tamisemi wametoa ajira za afya kupitia sektreatarieti ya ajira na utumishi wa umma.

Kiuhalisia mambo yanaenda kuwa Magumu kadri miaka inavyoenda.
Itabidi watu wafanye Interview.

Karibuni kwa mjadala na kuwekeana sawa kwa tunaomba hizi ajira.

Zipo kada mbalimbali nazo ni.

1. TABIBU MSAIDIZI(CLINICAL ASSISTANT)-639
2. AFISA LISHE
3. MUUGUZI II -2282
4. AFISA MUUGUZI MSAIDIZI 1016
5. MFAMASIA DARAJA LA PILI (PHARMACIST)-128
6. TABIBU KINYWA NA MENO(DENTAL THERAPIST)-210
7. MSAIDIZI WA AFYA -1057
Jumla.
8. AFISA AFYA MAZINGIRA
DARAJA LA PILI(ENVIROMENTAL OFFICER II)-124
9. KATIBU WA AFYA-41
10. FIZIOTHERAPIA II -83
11. MTEKNOLOJIA MENO DARAJA LA II -3
12. AFISA PHYSIOTHERAPY II-11
13. AFISA MUUGUZI DARAJA LA PILI-301
14. AFISA MTEKNOLOJIA MAABARA DARAJA LA PILI-57
15. DAKTARI BIGWA WA MAGONJA YA NDANI -7
16. MTEKNOLOJIA MSAIDIZI RADIOLOJIA -15
17. AFISA AFYA MAZINGIRA DARAJA LA PILI -124

Karibuni kwa kujadili.

Kusaidiana jinsi ya kuomba.

Walimu mjiandae.
😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom