TAMISEMI wametangaza ajira za afya leo kupitia Sekretarieti ya Ajira, sasa ni mwendo wa Interview

TAMISEMI wametangaza ajira za afya leo kupitia Sekretarieti ya Ajira, sasa ni mwendo wa Interview

Mimi ninatumia PC kumuombea, sasa jana nimejaribu kwa kumsajili kwa kutumia email nyingine, kumbe kwenye simu yake anatumia email nyingine, ndio maana nawaza huo ujumbe wa Ku activate akaunti yake ya ajira portal utatumwa wapi, au nianze upya tu mchakato wa kumsajilia akaunti mpya?
Email ya kwanza kuitumia kufungulia akaunti ndio itatumiwa hy link ya kuactive
 
Kuna kitu hapa kingine, akaunti niliyomfungulia ajira portal ina utofauti na anayotumia kwenye simu yake, yaani email mbili tofauti, je hapo kwenye huo ujumbe wa kufanya akaunti yake ya ajira portal iwe active utatumwa wapi, maana ni email mbili tofauti.
Kwanza mfumo una ruhusu account moja tuu! Kama unaongelea email basi email itayapokea ujumbe wa kuhuisha account yako ni ile email uliotumia kufungua account ajira portal!
 
Jamaa inaonyesha anaogopa knoma interview, na kama kutakuwa na interview sidhan kama ataenda huyu lazima alale home kuendelea kusubiri kazi zisizokuwa na Interview
Kwa taarifa yako nina oral mwaka jana nimepiga interview taasisi kubwa tu ya afya ba tulikuwa 700+ na nikapita sasa sijui kipi unadhani naogopa
 
Huyu jamaa inabidi atuonyeshe akaunti yake kuanzia mwanzo hadi mwisho ili kama kuna makosa tumsaidie kurekebisha kabla ya deadline

Utawala2025
Hiyo Hapo
Screenshot_20240714-163824~4.jpg
 
Bro, sijakuelewa.
Yn atulie mpaka atakapoitwa interview ndio abadili anuani kvp wakat wakiitwa maana ake tayari watakuwa wameshaandaliwa sehemu pa kufanyia usaili?

Au unamaanisha kuitwa usaili na kufanya usaili n vitu viwili tofauti?
Ebu soma vizuri hapo kweny boksi jekundu unisaidie na mimi kuelewa
Screenshot_20240714-151244.jpg
 
Mwaka jana wizara ya afya walitoa ajira post 289 na waliomba kupitia Utumishi waliitwa kazini na hawakufanya interview.
Ajira za mwaka jana za wizara hazikupitia utumishi kwa maana ya Psrs...ila zilipitia portal maalumu ya wizara ya afya wenyewe kama ambavyo ilivyokuw kwa portal ya tamisemi kwa ajira za mwaka jana.
 
Asante Kwa ufafanuzi ulionyooka. Swali Moja haujafafanua/kujibu ambalo ni kwamba: mfano Mimi musangaa nimeomba nafasi ya daktari bingwa mkoa wa katavi nimejaza anuani yangu mkoa wa Mtwara, je interview itanihitaji niende mkoani katavi au niabaki hapo hapo Mtwara? Kumbuka hii ni online interview kama ulivyodadafua. Kama itanihitaji nifanyie huko huko Mtwara, naweza kwenda kwenye vituo vyao pendekezwa kulingana na watakavyoelekeza, je ikitokea nipo mkoani Mara nitatakiwa kusafiri kwenda Mtwara kwenye anuani niliyojaza au mfumo utanikubalia kusailiwa hata kama nitakuwa Mara huko huko Kwa nafasi ya daktari bingwa niliyoomba mkoa wa katavi?
Kila mkoa una kituo chake. Utafanya mtihani katika kituo kilichopo mkoa husika.
 
Tupe mwanga maswali ya oral yanakuwaje mkuu, english or swahili or both? Na yanakuwa ya darasani au ni yale maswali trick kama utaifanyia nini kampuni tukikuajiri au utakuwa nani baada ya miaka 8[emoji28]
Ufahamu.

Scenario za hospital kama ethical dillema.

Maswali yake mengi ni ufahamu hayako direct anaweza akawa anahitaji management ya ugonjwa Fulani ila akakuzunguka.

Kiukweli majamaa inabidi usome upige shule kweli kweli uwe una uelewa kila mahali wa kada yako.

Ila maswali ni ya darasa ila wanayaleta mazingira ya kazini.

Japo kabla haujaenda kwa interview jus job discription zako.na Uzi some kila moja kama topics.

Mfano kama ww CO.

Moja ya jukumu lako ni Ku conduct minor cases zote basi hapo inabidi usome minor case na procedure zote.

Kama moja ni Ku provide health education to the clients lazima upige shule ya Health education and importance zake zote.

Kama muuguzi.

Utafanya Maternal and child care inatakiwa usome RCH uijue.

Ukisema To provide General nursing care basi hapo inatakiwa upige shule ya General nurse ,care zote na management zote.



Kikubwa na cha msingi jamani.

1.Tumwamini Mungu.

2.Tuanze sasa kusoma.

3.Interview inatisha ila tusiogope.

ORAL .

COMMON QN.

1.Introduce Yourself

2.Explain your job description according to your position unayotakiwa kuajiriwa...
 
Nyie mnajua hamjaomba kazi halfu wajuaji sana.

Mimi nimeaplai kazj iringa.

Ila current location Dar.

Haya niambie interview nitaitwa wapi?
Kijana interview utafanya kwenye kituo kilicho sehemu ulipo. Kumbuka kabla ya kufanya usaili, kama application zako ziko sawa, utapewa examination number. Hiyo examination number ni kwa ajili ya usaili wa nafasi uliyoomba. Hata kama utafanyia mtihani kwa kituo cha Dar es salaam na umeapply Iringa. Inaruhusiwa.

Kama hauelewi hizi kazi watafute psrs kwa maelekezo
 
Kuna mtu nina jaribu kumuombea nafasi za afya, nimesha sajili akaunti, tatizo nikianza tu ku apply hiyo nafasi inaandika Account Inactive, je nifanye nini hapo?
Ukifungua account kwa mara ya kwanza. Kuna email unatumiwa kuactivate account. Nenda inbox ya email uliyoombea , utakuta activation email.


NB: Muwe mnafata maelezo mnayopewa. Achen papara.Deadline bado mbali.
 
Kijana interview utafanya kwenye kituo kilicho sehemu ulipo. Kumbuka kabla ya kufanya usaili, kama application zako ziko sawa, utapewa examination number. Hiyo examination number ni kwa ajili ya usaili wa nafasi uliyoomba. Hata kama utafanyia mtihani kwa kituo cha Dar es salaam na umeapply Iringa. Inaruhusiwa.

Kama hauelewi hizi kazi watafute psrs kwa maelekezo
Achana na mm


Nitafanya popote pale na kazi nitapata.

Humu ndani maafisa utumishi mmekuwa wengi.
 
Back
Top Bottom