Labda tuseme hilo tangazo limeandikwa vibaya, linasema "kwa wale walioitwa kwenye usahili wa u update anwani zao ili wapangiwe vituo vya usahili vilivyo karibu nao"
Hapo wamezingatia kuwa, watu wanafanya movements za kila mara kwenye utafutaji ambapo anaweza kukutwa na muda wa usahili akiwa sehemu nyingine mbali na makazi yake.
Ebu tuchukulie wewe upo Dar kwa sasa ila wakati ukiendelea kusubiri call for Interview ukapata dharura ukaenda Mwanza, ukiwa Mwanza call for Interview zikatoka na inabidi ukafanyie usahili Dar. Sasa kwa kurahisisha wakasema "Wale walioitwa wabadili anwani zao ili waweze kufanya walipo kwa muda huo"
Hadi hapa unaonaje huu mtindo?