TAMISEMI yafafanua kasoro za majina ya walimu walioitwa kwenye ajira 13,000 za Magufuli

TAMISEMI yafafanua kasoro za majina ya walimu walioitwa kwenye ajira 13,000 za Magufuli

Tulipo piga kelele kuhusu walimu waliotumia index za kidato cha nne za mwaka jana(2019),katibu mkuu alijitokeza na kutoa utetezi dhaifu kwamba walikosea kuandika mwaka wa kumaliza kidato cha nne badala yake wakaandika mwaka wa kumaliza chuo na kwamba walimu hao wamemaliza form four kati ya 2010 - 2014.

Kutokana na utetezi huo dhaifu uliotolewa na katibu, leo namleta kwenu DAUDI MWITA WILLIAM.

Tamisemi imemwajiri mwalimu huyo kwa kutumia index namba ya kidato cha nne S0846-0089/2010 ambayo sio yake.

Katika uchunguzi mdogo niliofanya nimebaini kuwa DAUD WILLIAM ameajiriwa kwa kutumia namba ya mwanafunzi ZILPA FREDRICK ambaye hakubahatika kuendelea na masomo kutokana na kupata ufaulu hafifu kwenye matokeo yake ya kidato cha nne.

Ushahidi huu hapa

(i) Kiambatanisho kumwonyesha DAUDI WILLIAM mwl aliyeajiriwa na tamisemi

View attachment 1639959
(ii) kiambatanisho kumwonyesha ZILPA FREDRICK mmiliki halali mwenye index namba S0846-0089/2010
View attachment 1639968

Mbaya zaidi TAMISEMI ambao wana fanya kazi kwa kushirikiana wizara ya elimu ambayo ina mifumo ya kuhakiki uhalali wa vyeti wameshindwa kuhakiki vyeti vya waombaji badala yake wamewaachia wakurugenzi wa halmashauri ambao wana hakiki vyeti kwa macho.

Kwa mwendo huu watumishi hewa hawatokuja kuisha serikalini.
Mbona kiambatanisho Cha matokeo hakioneshi mwaka wa kumaliza shule acha kudokoa namba na kuja kuzuga hapa.
Tutaaminije Kama Zilpa alimaliza 2010.​
 
rais anajinasibu suala la vyeti feki kalidhibiti, ila kwa makosa haya ya TAMISEMI ni big NOOOO
Unaondoa wafanyakazi kazi feki then unawarudisha wafanyakazi feki.

Workdone=0
Inasikitisha sana. Pamoja na jitihada za Rais za kuondoa watumishi hewa, wanaondokea mlango wa mbele na kuingilia mlango wa nyuma. Rais bado ana kazi sana ya kutumbua majipu
 
Mbona kiambatanisho Cha matokeo hakioneshi mwaka wa kumaliza shule acha kudokoa namba na kuja kuzuga hapa.
Tutaaminije Kama Zilpa alimaliza 2010.​
Ukisema nipige screenshot ikionyesha hadi mwaka maana yake jina la mlengwa ambaye ni ZILPA halitaonekana. Kwahiyo kama unataka kuhakikisha kama hizi shutuma ni za kweli au uongo ingia kwenye tovuti ya necta uangalie matokeo ya kidato cha nne 2010 ya mtahiniwa mwenye namba S0846-0089/2010. Ukimaliza kuangalia uje ufute huu utetezi wako wa kijinga.
 
Mbona kiambatanisho Cha matokeo hakioneshi mwaka wa kumaliza shule acha kudokoa namba na kuja kuzuga hapa.
Tutaaminije Kama Zilpa alimaliza 2010.​
hata mimi nilikuwa najiuliza hilo swali ... huyu jamaa mwongo sana anaamnisha watu uongo namba ya juu inaonesha mwaka lkn namba ya chini haina mwaka...... uzushi wa kitoto sana huu ..
 
Mtamlaumu bure katibu mkuu tamisemi kifupi tu ni kuwa serikali haina hela za kuajiri walimu 13000 hivyo njia iliyotumika ni kuweka majina hewa ambayo ndio hayo mengi mnaona yana utata,mfano ni yule bwana aliyejirudia mara 195 hii ilikuwa ni mbinu mojawapo ya kupunguza idadi na walipoona raia wanapiga kelele katibu alijitokeza na kutoa utetezi dhaifu wa kiwango cha darasa la kwanza.KATIBU ANAKINGIWA KIFUA NA MTU ASIYEONEKANA la sivyo angekuwa hana kazi siku ya pili tu majina yalipotangazwa.Serikali imeajiri walimu halali wasiopungua 2000 hao wengine waliosalia ni changa la macho ndio maana mnaona madudu ni mengi!
 
hata mimi nilikuwa najiuliza hilo swali ... huyu jamaa mwongo sana anaamnisha watu uongo namba ya juu inaonesha mwaka lkn namba ya chini haina mwaka...... uzushi wa kitoto sana huu ..
Kumbe JF ina wajinga wengi kiasi hiki?

Ebu wewe nenda kwenye matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2010 upige screenshot ikimuonyesha ZILPA na mwaka wa kumaliza kule juu tuone kama utaweza.

Yaani badala ya kuangalia matokeo ili kujiridhisha kama ni uongo au ukweli unakuja hapa kutetea upumbavu. Pathetic
 
Tulipo piga kelele kuhusu walimu waliotumia index za kidato cha nne za mwaka jana(2019),katibu mkuu alijitokeza na kutoa utetezi dhaifu kwamba walikosea kuandika mwaka wa kumaliza kidato cha nne badala yake wakaandika mwaka wa kumaliza chuo na kwamba walimu hao wamemaliza form four kati ya 2010 - 2014.

Kutokana na utetezi huo dhaifu uliotolewa na katibu, leo namleta kwenu DAUDI MWITA WILLIAM.

Tamisemi imemwajiri mwalimu huyo kwa kutumia index namba ya kidato cha nne S0846-0089/2010 ambayo sio yake.

Katika uchunguzi mdogo niliofanya nimebaini kuwa DAUD WILLIAM ameajiriwa kwa kutumia namba ya mwanafunzi ZILPA FREDRICK ambaye hakubahatika kuendelea na masomo kutokana na kupata ufaulu hafifu kwenye matokeo yake ya kidato cha nne.

Ushahidi huu hapa

(i) Kiambatanisho kumwonyesha DAUDI WILLIAM mwl aliyeajiriwa na tamisemi

View attachment 1639959
(ii) kiambatanisho kumwonyesha ZILPA FREDRICK mmiliki halali mwenye index namba S0846-0089/2010
View attachment 1639968

Mbaya zaidi TAMISEMI ambao wana fanya kazi kwa kushirikiana wizara ya elimu ambayo ina mifumo ya kuhakiki uhalali wa vyeti wameshindwa kuhakiki vyeti vya waombaji badala yake wamewaachia wakurugenzi wa halmashauri ambao wana hakiki vyeti kwa macho.

Kwa mwendo huu watumishi hewa hawatokuja kuisha serikalini.
Hivi wahusika Bado hawajiuzulu nyadhifa zao hadi Sasa? Hawa ni wahujumu uchumi wasakwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
 
Serikali yaanika sababu kasoro majina kwenye ajira za walimu

SERIKALI imeeleza sababu zilizochangia kuwapo kwa kasoro mbalimbali kwenye majina ya ajira za walimu 13,000 zilizowekwa kwenye tovuti hivi karibu.

Hali hiyo ilizua mjadala na maswali mengi katika mitandao ya kijamii, huku ikibainisha hatua zilizochukulia na zikazochukuliwa kuanzia jana.

Ufafanuzi huo ulitolewa jana na makatibu wakuu watatu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhandisi Joseph Nyamhanaga, Katibu Mkuu Utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo.

Mhandisi Nyamhanga alisema kuwa kutokana na kuwapo kwa maswali mengi katika mitandao ya kijamii kuhusu majina ya walimu waliopata ajira za ualimu, wameshazifanyika kazi baadhi ya dosari.

Alisema maswali ambayo yalikuwa yakihojiwa ni mwalimu mmoja jina lake kujitokeza zaidi ya mara 196, hivyo kuibua mjadala.

“Hili tayari tumeshalifanyia kazi na hii ilitokana na tulivyokuwa tukiandaa orodha hii ili kupandisha kwenye tovuti… kuna tatizo la kiufundi lilitokea, lakini hali hii siyo kama imeathiri lolote au mwalimu huyo kuchukua nafasi za wengine 195, tumeshalifanyika kazi tumeona leo tuwaite ili kuwaeleza suala hili namna ambavyo tumelitatua,” alisema Nyamhanga.
Aidha, alisema dosari nyingine mbayo ilikuwa ikilalamikiwa ni majina ya baadhi ya watu waliopata ajira kuonekana ni wahitimu wa kidato cha nne mwaka jana.

“Tayari tumefanya uhakiki kubaini kuwa hii ilitokana na waombaji kukosea kuandika taarifa zao, wengi wao waliandika miaka waliyomaliza kidato cha nne na mwaka waliopata shahada yao basi… lakini ukweli ni kwamba hakuna mhitimu wa mwaka 2019, 2018 wala 2017 aliyechaguliwa kwenye ajira hizi,” alifafanua Nyamhanga.

Alisema kwa mujibu wa vielelezo walivyovipitia, kwa waliochaguliwa kupata nafasi hizo ualimu wengi wao ni wahitimu wa kidato cha nne kuanzia mwaka 2010 hadi 2014.
Vile vile, Katibu Mkuu huyo alisema wanaendelea na uhakiki wa majina yote ili kujiridhisha kama ni watu wanaostahili na kuondoa dosali zote.

“Uhakiki huu utaanza leo (jana) na tunatarajia ukamilike ndani ya siku mbili ili watakaostahili waripoti katika maeneo yao na kupatiwa stahiki zao kama ambavyo taarifa ya awali ilivyokuwa inabainisha,” alieleza.

Katibu Mkuu Utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro, alisema wao ndio wenye mamlaka ya kutoa vibali vya ajira na katika mwaka huu wa fedha, jumla ya walimu 13,000 watapatiwa ajira.
Alisema katika ajira hizo 13,000, walimu 8,000 ndiyo ambao majina yao yametolewa kwenye mtandao na wengine 5,000 watatangazwa baadaye.

Akizungumza kuhusu uhakiki, Dk. Ndumbaro alisema walimu ambao watabainika kuwa wamepata nafasi hizo kwa udanganyifu wataondolewa, na nafasi zao kupatiwa mtu mwingine mwenye sifa.

“Mfumo huu uliotumika kuomba ajira kuna baadhi ya walimu ambao walikuwa ni wa Historia, lakini wamejaza na somo la Hisabati ili mfumo uwatambue,” alisema na kuongeza:

“Sasa niseme tu kwa yeyote atakayebainika amepata ajira kwa somo ambalo hajalisomea, ataondolea na kumzuia asipate tena ajira serikalini.”

Chanzo: NIPASHE
PhD 2
Eng 1
Mnasahihishwa na mitandao ya KIJAMII.kwanini msipitie mambo yenu kabla hamjarusha?
 
Back
Top Bottom