LGE2024 TAMISEMI yasema CCM imefanikiwa kuweka Wagombea Mitaa yote, upinzani wameweka Wagombea 30,977 katika nafasi 80,430

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Yule ndo mwanaume na ndo Mpinzani haswa.. Hoja zake zilikuwa za msingi na Cdm wameingia Mazima kwenye mkenge ambao walitakiwa kutathimini kwanza
Lkn msimsauu yule mzee Sumu aiyonjwi. Sasa tuwaze namna ya kuonja sumu au mm ndio sijaelewa!!!!!
 
Siku ya hesabu ni mgumu sana wengi tunaangalia vyeo vya madaraka vya muda mchache wa dunia hii. Tupo tayari tusifiwe na binaadam wenzetu lkn tuziangamize nafsi zetu
 
Inashangaza serikali nayo inagombania nafasi za uongozi na wakati huohuo na wao serikali ndio marefarii wa uchaguzi huo!
 
Huyu ni waziri shetani na mwongo mkubwa.

Alistahili kusema kuwa yeye kwa ushetani wake amefanikiwa kuwaengua wagombea wote wa upinzani na kuwabakiza 30,000.
 
Mi nasubiri TU kuona wataojitokeza kupiga kura...
 
Alipoulizwa kuhusu Tume Kificho ya Watu wachache wa Frelimo ikifanyaje kufanya uchafuzi wa mchakato wa mzima wa matayarisho ya uchaguzi, uandikishaji na upigaji kura siku ya uchaguzi tarehe 9 Oktoba 2024 kigogo Fernado Mazanga alifunguka ...


SEMA UKWELI WA MUNGU MOHAMED MCHENGERWA", APIGWA MASWALI MAZITO NA WANAHABARI KUENGUA WAGOMBEA WA UPINZANI


View: https://m.youtube.com/watch?v=PAFT6Mfysx0
 
16 November 2024
Dodoma, Tanzania

NAIBU KATIBU MKUU CHADEMA, KIGAILA ANATANGAZA MAAMUZI MAZITO USIKU JUU DODOMA

View: https://m.youtube.com/watch?v=CoH_uLw9NzATumekwenda TAMISEMI kwenye ofisi za waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI maeneo ya Mtumba, tumegonga milango ya ofisi za TAMISEMI usiku huu siku ambayo ni ya mwisho kusikilizwa lakini tumeambiwa ana press mjini tukaondoka Mtumba hadi mjini kwenye press kumuona waziri Mohamed Mchengerwa...

Picha : waziri Mohamed Mchengerwa alipokuwa mjini Dodoma akiongea na press.

Huu ni uhuni mtupu na CCM ina kifua cha kujidai imeweza kusimamisha wagombea wengi na nafasi zote, huku wagombea wetu wakienda ofisi za serikali watu hawapo, ofisi zimefungwa au watumishi wanajificha ili wasisikilize matatizo ya wagombea wa CHADEMA katika ofisi zote za umma za TAMISEMI mikoani, wilayani na ofisi za maDED Halmashauri zote nchini

Picha: Jengo la makao makuu ya TAMISEMI Mtumba Dodoma.

Tukaambiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma kuja kuwasikiliza viongozi za CHADEMA ujumbe unaoongozwa na Benson Kigaila, akatusikiliza kisha akatuelekeza tumuone mkuu wa uratibu wa uchaguzi wa mkoa...

Mfano mgombea wetu wa mtaa wa Medeli mgombea wetu ameambiwa siyo mkazi wa pale na amemaliza uongozi wake mwezi Oktoba 2024... CHADEMA tukajibiwa kuwa mke wa mgombea wa mtaa kuwa mgombea wa CHADEMA halali Medeli ...vituko kweli kweli ..
 
mkoa wa Dodoma kuja kuwasikiliza viongozi za CHADEMA ujumbe unaoongozwa na Benson Kigaila,

CHADEMA waonana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule usiku huu 16.November 2024​


Picha maktaba : Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary S. Senyamule

Kesho pia CHADEMA wanaamkia ofisini kwa mkuu wa mkoa kufuatilia haki za wagombea wa CHADEMA mkoa wa Dodoma walioenguliwa ...
 
Shida yao hao vilaza huwa wanatuona wananchi wote hatuna akili. Mimi ndiyo maana sijishughulishi tena na huo upuuzi wao wa kupiga kura.
Hakuna kinacho kukera ndio maana hupigi kura.Ukitaka kufanya mabadiliko yoyote wajibika,shiriki uchaguzi piga kura kijana,ukipiga kura utaitetea kura yako na MUNGU wa mbinguni atayasikia maombi yako.Tunatakiwa tuhamasishane kwende kupiga kura,ww usihofu kwamba wataiba kura shiriki na amini hawataiba siku zote,wakati wa MUNGU ukifika nakuhakikishia hakuna mtu ataiba kura na siku ipo ambayo wezi wote na wahuni watarudi shimoni na nakuhakikishia hilo.Twendeni tukapige kura kwa furaha na tumtangulize MUNGU.
 
Huwezi kuaminika kirahisi wakati umeandaa mazingira ya kushinda uchaguzi kwa nguvu,kama kweli Demokrasia ni uwanja wa wote iweje ww uwe unajua kila kitu kuliko wenzako,unawatengenezea wenzako mazingira ya kipumbavu kabisa hayajaenda hata shule ukidhani watu ni wajinga.Hizo data ni za kupika tu kwa sababu mazingira yamejionyesha toka mwanzoni mwa zoezi hili.Wizara ina Mkwe ambaye hataki mama Mkwe wake ashindwe,sasa huyo ndio tutegemee atuambie ukweli while he is not serious.
 
16 November 2024
Tarime, Tanzania

Katibu wa CHADEMA jimbo la Tarime vijijini anaongea na waandishi wa habari kuhusu :

CHADEMA YAFANYIWA HUJUMA TENA MAAMUZI YA RUFAA HAYAKUFUTA KANUNI ZA UCHAGUZI

View: https://m.youtube.com/watch?v=8KOwzcm5zK8Katibu wa CHADEMA jimbo la Tarime vijini kamanda Mrimi Zabron awa mbogo maamuzi ya DAS wilaya ya Tarime Vijijini...

Waweka hujuma zilizofanywa na DAS na Kamati yake ya rufani ya wilaya ya Tarime vijijini na kufikia maamuzi kwa kutumia kanuni zisizokuwepo ...

Mgombea wa CCM ndugu Mugaya Lyoba Kisire kesi ya mauaji criminal case 66 2021 vs Jamhuri kifungo cha mwaka mmoja jela lakini hajaenguliwa katika kugombea na amepitishwa kugombea

Mgombea mwingine wa CHADEMA kutoka kijiji cha Mpakani Sirari amevaa joho la udiwani kwa miaka mingi ameengulwa kuwa siyo raia huu ni uhuni Kamati ya Rufani wa Wilaya waka edit kitambulisho cha uraia wa Kenya ili kisomeke cha mgombea wetu wa CHADEMA ...

TOKA MAKTABA:
KATIBU TAWALA mkoa wa Mara asisitiza ushirikiano na wadau yaani 4R za kauli mbiu ya awamu ya sita iliyopo madarakani

Posted on: November 15th, 2024
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Gerald Musabila Kusaya leo ameongoza kikao tathmini na mipango ya utekelezaji wa mradi wa Kizazi Hodari Mkoa wa Mara killichofanyika katika ukumbi wa uwekezaji na kuzitaka Halmashauri kutoa ushirikiano kwa taasisi zinazotekeleza mradi huo.
 
Vetting ya "uwazuri" bongo ni ya hovyo sana aisee! Tunasafari ndefu sana bongo hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…