LGE2024 TAMISEMI yasema CCM imefanikiwa kuweka Wagombea Mitaa yote, upinzani wameweka Wagombea 30,977 katika nafasi 80,430

LGE2024 TAMISEMI yasema CCM imefanikiwa kuweka Wagombea Mitaa yote, upinzani wameweka Wagombea 30,977 katika nafasi 80,430

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Huyu ni waziri shetani na mwongo mkubwa.

Alistahili kusema kuwa yeye kwa ushetani wake amefanikiwa kuwaengua wagombea wote wa upinzani na kuwabakiza 30,000.

Huyu ni waziri shetani na mwongo mkubwa.

Alistahili kusema kuwa yeye kwa ushetani wake amefanikiwa kuwaengua wagombea wote wa upinzani na kuwabakiza 30,000.
Huwezi kuaminika kirahisi wakati umeandaa mazingira ya kushinda uchaguzi kwa nguvu,kama kweli Demokrasia ni uwanja wa wote iweje ww uwe unajua kila kitu kuliko wenzako,unawatengenezea wenzako mazingira ya kipumbavu kabisa hayajaenda hata shule ukidhani watu ni wajinga.Hizo data ni za kupika tu kwa sababu mazingira yamejionyesha toka mwanzoni mwa zoezi hili.Wizara ina Mkwe ambaye hataki mama Mkwe wake ashindwe,sasa huyo ndio tutegemee atuambie ukweli while he is not serious.
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa amesema Chama cha Mapinduzi (CCM), kimefanikiwa kuweka wagombea katika nafasi zote za vijiji, vitongoji na mitaa huku upinzani ukiweka wagombea 30,977 sawa na asilimia 38 ya nafasi zote 80,430 zinazoshindaniwa.

Waziri huyo amesema hayo leo Jumamosi, Novemba 16, 2024 wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari jijini Dodoma akitoa tathmini ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Amesema nafasi zitakazogombewa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Jumatano ya Novemba 27, 2024 ni mwenyekiti wa kijiji nafasi 12,280, mwenyekiti wa mtaa nafasi 4,264 na mwenyekiti wa kitongoji nafasi 63,886, wajumbe wa serikali ya kijiji 230,834 na wajumbe wa kamati ya mtaa 21,320.

Amesema CCM kilifanikiwa kuweka wagombea katika nafasi zote zilizogombewa, huku vyama vingine vikiweka wagombea katika baadhi ya nafasi.

Nafasi za mwenyekiti wa kijiji zinazogombewa ni 12,280 ambapo vyama 18 vya siasa viliweka wagombea katika nafasi 6,060 sawa na asilimia 49.35 ya nafasi hizo.

Amesema nafasi za mwenyekiti wa mtaa zinazogombewa ni 4,264 ambapo vyama 18 vya siasa viliweweka wagombea katika nafasi 3,281 sawa na asilimia 76.94 ya nafasi hizo.

"Nafasi za mwenyekiti wa kitongoji zinazogombewa ni 63,886 ambapo vyama 18 vya siasa viliweka wagombea katika nafasi 21,636 sawa na asilimia 33.87 ya nafasi hizo," amesema.

Amesema nafasi zote zinazogombewa ni 80,430 (ukitoa nafasi za wajumbe wa serikali za vijiji na kamati za mitaa), ambazo zinajumuisha vijiji 12,280, mitaa 4,264 na vitongoji nafasi 63,886.

Ameongeza kuwa kati ya rufani 16309 ziizopokelewa baada ya muda wa nyongeza wa siku mbili nilizoongeza za rufaa takribani rufaa 5589 zimepokelewa na kukubaliwa hii ilizingatia kuwa dosari ambazo zilisababisha kuto teuliwa kwao hazikuwa kubwa na kuathiri kanuni.

TAMISEMI
Shetani hasemi ukweli hata siku moja.
 
16 November 2024
CHADEMA PWANI

Viongozi wagombea wanawake wa CHADEMA NOVEMBER 2024


View: https://m.youtube.com/watch?v=MBM9MwBqCIk
Sasa hivi Tanzania tuna viongozi wanawake kuanzia urais, spika, mawaziri, wakuu wa mikoa, maDC, maDED lakini mmeenguliwa kugombea serikali za mitaa 27 November 2024, ingekuwa nafasi hizo ni wanaume pekee tungesema ni mfumo dume ndiyo unakandamiza wanawake ... kule jimbo la Kibamba people's power imesababisha mkurugenzi kurejesha walioenguliwa....

15 November 2024
Jimbo la Kibamba Ubungo Dar es Salaam walivyopiga kambi usiku mbele ya Ofisi za Wilaya kuonana na Kamati ya Rufani ya Wilaya ...

View: https://m.youtube.com/watch?v=0i8jbcpPc68
 
Ofisi za Wilaya kuonana na Kamati ya Rufani ya Wilaya ...

Katibu Tawala Wilaya ya Ubungo Ndg Hassan Mohamed Mkwawa kiongozi wa kamati ya wilaya ya rufani shughulika na mapingamizi na rufaa za uchaguzi wa serikali za mitaa 2024

1731792140251.jpeg

Picha maktaba : Hassan Mohamed Mkwawa DAS wa wilaya ya Ubungo mkoa wa Dar es Salaam akiwa ktk shughuli zake za kawaida
 
Mzimamizi mkuu wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 aliye pia mteuzi wa maDED, DAS ambao ni wasimamizi wa chaguzi na rufani mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia S. Hassan

1731792634827.jpeg

Picha maktaba : Rais Samia Hassan akiwa kazini ikiwemo pia kuratibu na kutoa maagizo kwa waziri wa OR TAMISEMI wasimamizi wakuu wa uchaguzi wa 2024
 

MHE. MCHENGERWA: RUFAA 5,589 ZA WAGOMBEA ZIMEKUBALIWA​

1731817913124.jpeg

Imewekwa tar.: November 16th, 2024
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kati ya rufaa 16,309 za wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa zilipokelewa, rufaa 5,589 zimekubaliwa.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Novemba 16, 2024, Waziri Mchengerwa amesema rufaa hizo ni pamoja na zilizowasilishwa baada ya muda wa nyongeza wa siku mbili na uamuzi wake umezingatia dosari ambazo zilisababisha kutoteuliwa kwao awali hazikuwa kubwa zinazoathiri matokeo yaliyokusudiwa na kanuni.

Aidha, amesema katika nafasi zinazogombewa vyama 18 vya siasa vimeweka wagombea katika nafasi 30,977 kati ya nafasi 80,430 sawa na asilimia 38.51 huku Chama cha Mapinduzi (CCM) kikiweka wagombea katika nafasi zote.

Amesema katika nafasi za mwenyekiti wa kijiji zinazogombewa ni 12,280 ambapo vyama hivyo vimeweka wagombea katika nafasi 6,060 sawa na asilimia 49.35.

Pia, amesema nafasi za mwenyekiti wa mtaa zinazogombewa ni 4,264, vyama viliweka wagombea katika nafasi 3,281 sawa na asilimia 76.94 na nafasi za mwenyekiti wa kitongoji zinazogombewa ni 63,886 vyama vimeweka wagombea 21,636 sawa na asilimia 33.87.

Hata hivyo, ametaja baadhi ya sababu zilizosababisha wengine kutoteuliwa ni kukosa sifa ya uraia watanzania, kujidhamini wenyewe, kutojiandikisha kwenye daftari la wapigakura wa serikali za mitaa na wengine kuwa chini ya umri wa miaka 21.

Pamoja na hayo, amesema Ofisi ya Rais - TAMISEMI imefuatilia tuhuma zilizotolewa kwenye maeneo mbalimbali na kubaini hazikuwa na ukweli na zililenga kuleta taharuki na kuchafua mchakato wa uchaguzi unaoendelea vizuri

Source : OR TAMISEMI
 
16 November 2024
Mbeya, Tanzania

Utayari wa BAVICHA kama vijana Jimbo la Mbeya mjini 2024


View: https://m.youtube.com/watch?v=f3Ip9aD948Y
Mwenyekiti wa BAVICHA Jimbo la Mbeya mjini Hassan Mwamwembe, na katibu wa BAVICHA wakiongea kuhusu utayari wa vijana uchaguzi 2024

Jakaya Kikwete alifanya vizuri katika utawala wake ila mwendazake katika awamu yake aliharibu na sasa awamu ya sita imeamua kumuiga mwendazake wakidhani ndiyo utawala bora BARAZA la Vijana Mbeya mjini wakiangalia hali ya kisiasa iliyopo ...
 

MAENEO YA UTAWALA YATAKAYOFANYA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024​

1731821359863.jpeg


Imewekwa tar.: November 16th, 2024
Maeneo yatakayofanya uchaguzi tarehe 27 Novemba, 2024 kwa sasa ni vijiji 12,280 kutoka Vijiji 12,333 vilivyotangazwa hapo awali, mitaa 4,264 tofauti na mitaa 4,269 iliyotangazwa hapo awali na vitongoji 63,886 ukilinganisha na vitongiji 64,274 vilivyotangazwa kwenye gazeti la Serikali Tangazo Na.796 na 797 yote ya tarehe 06 Septemba, 2024.

Mabadiliko haya yemetokana na Halmashauri za Wilaya za Kaliua, Nsimbo na Tanganyika kuwa na makazi ya Wakimbizi ya Ulyankulu, Katumba na Mishamo, na wananchi kuhama kwenye baadhi ya vitongoji kutokana na sababu mbalimbali.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa alipokua akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mchakato wa kuchukua, kurejesha, uteuzi pamoja na rufaa za wagombea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
 
Ni swala la kubali yaishe.

Lakini hakuna watanzania timamu kwa jinsi tunavyojuana huku vijijini A, B na C (walio chukua form za uchaguzi wapishane)!kwenye kujaza.

Jibu ni moja tu MaCCM ni majizi na dhulumati.
 
Wawatoe wapinzani wote wabaki wenyewe.maana hakuna jambo jipya watakaloyanya chini ya jua.Uwezo wakupata akili mpya hawana ndo maana wanaogopa ushindani.
 
Yaani kabla hata uchaguzi haujafanyika CCM imeshapora (kubaka) ushindi wa 68%.

Nawaambia tena bila Katiba mpya hii michezo ya kuigiza haitaisha, tujiandae mshangao mpya 2025.

Hata kama vyama vya upinzani vingetumia wiki 3 kufundishana namna ya kijaza zile form isingesaidia kitu, mkakati ulishasukwa mapemaa.
 
Kwa hiyo hata kabla ya kupiga kura CCM tumeshashinda kwa zaidi ya asilimia 60
Na ndiyo maana ya kuwaengua wapinzani kwani wangeachwa washindanishwe CCM ingeangukia pua,hawa nguruwe wa kijani ni waoga sana wa siasa za ushindani. Ila hii mbegu ya ukaburu wanayopanda ikija kustawi wao ndiyo watakuwa wahanga wakibwa. Watutsi waliwaonea sana Wahutu lakini ilipofika wakati wa kujibu mapigo Watutsi ndiyo walipata kipigo kitakatifu. Huu utaratibu wa kuwaona Wapinzani kama ni wahaini utakuja kuwaumiza sana CCM huko mbele ya safari.
 
kujua tu CCM imeweka wagombeya meeneo yote ya uchaguzi nchi nzima, wkt upinzani wameweka wagombeya wachache inatosha kukupa picha yawazi waz!!!!i Wapinzani wapo kimjini mjin wanaitumia siasa kama mchezo wa Kubet wanamkekawao wanachagua pakuweka ela!!!! Mfukoni wanamkeka na Media zao
Walipoweka pesa wakiona mizinguo Media inafanyakazi kulalamikia ujuma. Daaaa Sasa kweli CCM kuna siku itashindwa kweli tuache utani kama kushindwa kupitia Media umu lkn CCM MILELE imejipanga kinomanoma upinzani nikama wamekata tamaaa lkn ukiwasikia umu jamiiiF utazan kweli wamejipanga kuna mwaka tuliambiwa mwaka huu CCM isaau kupita bila kupingwa lkn wapi hii 2024 bado wapinzani wanaBET aibu yenu chaguzi za 2030 to 35 mjipange mapema mjivue aibu CCM aiyondoki kwa kumkebei rais aliemadarakan bali kujipanga kuweka wagombeya nch nzima chama kimekuwa chamatukio kinasubili jengo lianguke kipitishe fitna ndio CCM itaanguka kama lile jengo,, mmesaza mapemaa.
 
19 November 2024
Makao makuu ya CHADEMA
Mikocheni
Dar es Salaam, Tanzania

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Aikaeli Mbowe ameeleza takwimu za wagombea wa chama hiko katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

View: https://m.youtube.com/watch?v=Wasl5cbRSqc
 
19 November 2024
Makao makuu ya CHADEMA
Mikocheni
Dar es Salaam, Tanzania

Mbowe Awa Mbogo, "Safari Hii Hatujitoi Uchaguzi Serikali za Mitaa, Tuatenda Nao Ulalo Ulao"


View: https://m.youtube.com/watch?v=NqbnGGqin-U
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Aikaeli Mbowe amesema kuwa chama chake hakina mpango wa kujitoa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024, licha ya wagombea wao wengi kuenguliwa katika mchakato wa uteuzi.

Akisisitiza kuwa ilikuwa ni Azimio la Kamati Kuu ya chama hiko kushiriki kwenye chaguzi zote pamoja na mapungufu yote.Mbowe ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya CHADEMA yaliyopo Mikocheni Dar es Salaam.
 
19 November 2024
Makao makuu ya CHADEMA
Mikocheni
Dar es Salaam, Tanzania


View: https://m.youtube.com/watch?v=_gqVTR-jwQs
Katibu mkuu wa CHADEMA kamanda John John Mnyika akijibu na kufafanua kauli za waziri OR TAMISEMI ndugu Mohamed Mchengerwa alizotoa mbele ya press conference ya juzi mjini Dodoma ...
 
Back
Top Bottom