Wana chit chat habari... Nakuja kwa mwendo wa shoto-kulia (waliopitia jeshini enzi zetu wamenielewa hapo) kijeshi zaidi. Kwanza kabisa nimshukuru mwanasheria wangu
ruttashoborwa aliyeniletea barua ya kiofisi kuwa kuna kijiupepo kinavuma chit chat eti Mwenyekiti nipinduliwe. pia nawashukuru watendaji wangu wote katika ofisi yangu kwa kuonyesha msimamo thabiti na kutotetereka baada ya kusikia kelele za kile kinachoitwa mapinduzi, hii inadhihirisha jinsi walivyo makini na wanajiamini na kazi yao. Baada ya kupata taarifa hii nilikaa kimya kwanza ili niweze kusoma mawazo ya wanajamvi na uelewa wao juu ya nafasi yangu na msimamo wa kila mmoja katika jambo hili. Niliweza kubaini yafuatayo
i. Mwanzisha mada ameamua kuwachanganya watu kwani ametangaza mapinduzi ya kunivua uenyekiti ilhali hajui hata taasisi ya uenyekiti ikoje. matokeo yake kuna watu wameingia kwenye mtego wake pasi na kujua na muda si mrefu wataumbuka kama hawatajirudi.
ii. Wengi waliounga mkono mapinduzi haya hawajitambui na wengi ni bendera fuata upepo, ndo wale wakiahidiwa mabomba kutoa asali au kujengewa daraja toka posta hadi kariakoo wanashangilia pasipo kutafakari... wataishia pabaya.
iii.Wenye busara zao wametulia kwani wanaijua chit chat na taasisi ya uenyekiti na ndio maana wametulia and at some points wametoa ushauri kwa wakurupukaji.
TAMKO.
Kwa kuwa umma wa chit chat una imani na utendaji wa taasisi ya uenyekiti nasema mapinduzi aliyotangaza
Nivea ni batili na aombe radhi kwa wana chit chat kwa usumbufu aliowasababishia.Kinyume na hapo nitatoa masharti ambayo endapo atashindwa kutekeleza atajichagulia adhabu yeye mwenyewe.
ONYO
Kwa mnaopenda kushabikia mambo bila kuyapima be careful. Mwenyekiti hapinduliwi na wahuni na pick up na baiskeli zao. Tambueni hii sio mara ya kwanza mimi kutangaziwa mapinduzi, wako wapi wapinduaji...!?? Don't dance and me (usicheze na mimi) this is tall water.
Nawashukuru sana wale wote walioonyesha kuwa na imani nami. Tuanzie hapo kwanza....
c.c
Judgement ,
watu8,
ruttashoborwa
gfsonwin ,
The Boss Ruhazwe JR ,
Mamndenyi ,
Kipipi ,
Madame B and co. Ltd...
Chit chat mapendo
Baba V . The life chairperson of marriages and relationship affairs at chit chat..
Kuna swali..??????...