Tamko la Balozi wa Tanzania nchini China kuhusu Mtanzania aliyehusishwa na Udhalilishaji wa mwanamke China

Tamko la Balozi wa Tanzania nchini China kuhusu Mtanzania aliyehusishwa na Udhalilishaji wa mwanamke China

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Kutokana na tukio lililosambaa mitandaoni ambapo Usalama wa Umma wa Xi'an uliripoti tukio la wanaume wa Kitanzania kuwanyanyasa wanawake, Ubalozi wa Tanzania nchini China umethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo umesema kuwa umeomba mamlaka kumlinda kijana huyo na uchunguzi kufanyika kupata ukweli wa tukio hilo SOMA: Mtanzania ashambuliwa na mwanamke wa Kichina, yasemekana kwa kosa la kudhalilisha wanawake.

Zaidi ya hayo, Ubalozi umeeleza kuendelea kufanya mawasiliano na Mamlaka Mjini Xian ili kuhakikisha haki inatendeka na kuutaka umma kuwa na subira wakati tukio hilo likifanyiwa kazi.

1663077629930.png

Picha: Sehemu ya Tweet iliyotolewa na Ubalozi wa Tanzania nchini China

balozi taarifa.jpg

Picha: Tamko la Ubalozi wa Tanzania nchini China
 
Tatizo wao wakija bongo tunawatetemekea sana na kujikomba, lakini ukweli halisi Blacks hatupendwi kabisa. Hata kama alishambuliwa yeye watasema alishambuliwa kwanza.
Tuipende nchi yetu, tupendane kwanza wenyewe kwa wenyewe.
 
Dah inauma sana...sijui sisi black tulimkosea nini mungu
 
Tujue kwanza kama ni kweli au la. Kama ni kweli kijana alikengeuka maadili ya wenyewe, basi tuna haja ya kumkemea. Kujihami nyuma ya ubaguzi hakusaidii,tabia mbaya inabidi ikomeshwe.

Aidha, wakati tunamkemea, bado haki zake zipo palepale. Tunaweza kumtetea kwa kupaza sauti kuzitaka mamlaka zimtendee haki. Sheria mkononi haifai.

Hata hivyo, tunapaswa kuchukua tahadhari tukiwa ugenini. Hapa kwetu bado uelewa na mifumo ya kuthibiti unyanyasaji wa kijinsia ipo chini. Nchi za wenzetu ni tofauti, unaweza ukapotea.
 
  • Nzuri
Reactions: Cyn
Tunao kibao hapa,kama vipi tuwachape tu ndio waone uchungu na wao, sema nini hapa ukimgusa tu basi unaswekwa ndani shenztaip
 
Ukienda nje fata kilichokutuma tu, ukitaka kuingia kwenye mambo mengine utajitafutia tu shida
My friend; huenda huyo kijana hakuhusika: infact, wachina wanasema kuwa waafrica wote wanafanana, nivihgumu kwa wao kutofautisha watu weusi, so, ukienda huko unatakiwa kuwa mwangalifu na kupunguza matembezi yasiyo ya lazima
 
Tujue kwanza kama ni kweli au la. Kama ni kweli kijana alikengeuka maadili ya wenyewe, basi tuna haja ya kumkemea. Kujihami nyuma ya ubaguzi hakusaidii,tabia mbaya inabidi ikomeshwe.
Ila najiuliza: haka katoto kanaweza kuhangaika na hichi ki ajuza?
 
Back
Top Bottom