Tamko la Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunnah Tanzania (BASUTA) kuhusu mkataba baina ya Tanzania na DP World

Tamko la Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunnah Tanzania (BASUTA) kuhusu mkataba baina ya Tanzania na DP World

Ahaaa!Kumbe vifua vyenu Ansaar Sunnah mmejaa chuki kwa sababu kuna mikataba ya TEC na Serikali mliyosubiri kuitumia ktk kuutetea huu wa DP World na mnatumika kumlinda wa dini yenu?Kwamba HUKO nyuma ilikuwepo mikataba mibovukuliko huu na huu mbovu uendelee ili iwe saresare maua?BAKWATA nao watakuwa na tamko kama hili la Waislamu?
 
Nchi hii ujinga ni wa kiwango cha juu, waliosema DPW wana mkataba mbovu wa IGA leo hii wapo kimya na pengine wanafaidika katika kupitishia mizigo yao pale TPA.

Oooh IGA hii mbaya na mbovu kabisa!, leo hii Adani yupo hapo hapo bandarini tena yeye ndio anayefanya biashara katika magati nyeti kuliko huyo DPW.

Maaskofu hawawezi kukwepa lawama za wao kutaka kumkwaza Rais SSH katika suala hili la uwekezaji pale bandarini.
 
Helo Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunna Tanzania (BASUTA) Wameshutumu Vikali kile wamepita Undumilakuwili na Ukosefu wa Uadilifu Kwa Wanaopinga mkataba wa Bandari kwa kile wameita kugumbia macho Mikataba ya hovyo iliyowahi ingiwa hapo kabla.
---

Tamko la Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunna Tanzania (BASUTA) likielezea kuhusu makubaliano ya uendeshaji na uendelezaji wa bandari."

BASUTA haturidhishwi na 'undumilakuwili' na ukosefu wa uadilifu wa wapingaji wa mkataba ambao walifumbia macho mikataba mingi ya hovyo huko nyuma katika sekta mbalimbali ikiwemo madini na hawakutaka ifutwe lakini wako tayari kwa gharama yoyote kuhakikisha mkataba huu unafutwa na unakufa".
---
TAMKO LA BARAZA KUU LA JUMUIYA ZA ANSAAR SUNNAH TANZANIA (BASUTA) KUHUSU MKATABA BAINA YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SERIKALI YA DUBAI KUHUSU USHIRIKIANO WA KIUCHUMI NA KIJAMII KWA AJILI YA UENDELEZAJI NA UBORESHAJI WA

UTENDAJI KAZI WA BANDARI TANZANIA

MJADALA WA MKATABA WA BANDARI USITAWALIWE NA UZUSHI NA CHUKI ZA KIDINI

Utangulizi
a) Kwa kuwa katiba ya nchi yetu ya mwaka 1977 toleo la 2000 ibara ya 18 (1) na 19 (1) zinatoa haki ya kila mtu kuwa na uhuru wa kuwa na maoni yake na kutoa nje mawazo yake;

b) Kwa kuwa katiba yetu inatoa haki sawa kwa raia wote pasina ubaguzi wowote kwa misingi ya dini, rangi, kabila, jinsia au vyovyote vile;

c) Kwa kuwa watu wengine wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, wanataaluma, wanahabari na wadau wengine wamekuwa wanatoa maoni yao kuhusu suala la Mkataba baina ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya Dubai kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji kazi wa Bandari Tanzania kupitia kampuni ya DP World inayomilikiwa na serikali ya nchi hiyo;

d) Kwa kuwa katika mijadala hiyo kumekuwa na upotoshaji mwingi wa makusudi wa matukio na taarifa kuhusu Mkataba huo wa bandari kwa chuki au kwa ajili ya kutetea maslahi binafsi ya kiuchumi, kisiasa au ya kidini ya makundi fulani

e) Na kwa kuwa na sisi, BASUTA, ni Watanzania, viongozi wa taasisi ya dini, kama ilivyo kwa viongozi madhehebu mengine yaliyotoa maoni.

Hivyo basi, sisi viongozi wa Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunnah Tanzania (BASUTA) kutoka sehemu mbalimbali nchini Tanzania, kwa kujali maslahi mapana ya taifa, tumeamua leo Agosti 23, 2023 kutoa tamko letu kuhusu mwenendo wa mjadala wa Mkataba huo wa bandari, kama ifuatavyo:

Maoni Yetu

1.0 Kuhusu maudhui ya Mkataba wenyewe

a) Kwa kuwa, tunaamini Serikali kupitia wataalamu wake imetoa ufafanuzi wa kutosha kwa wadau wanaokosoa baadhi ya vifungu vya Mkataba huo na hivyo kutaka yafanyike maboresho na kundi jingine (ambalo hatukubaliani nalo) linalopinga Mkataba wote;

b) Na kwa kuwa wanaopinga Mkataba wote na kutaka ufutwe, walifungua kesi Mahakama Kuu ya kuomba tafsiri ya kisheria ambayo, kama utawala sheria unavyotaka, ilisikilizwa kwa haki na uwazi; kisha hukumu kutolewa kwamba, licha ya kasoro ndogo ndogo Mkataba huu ni halali kwa mujibu wa sheria za nchi na unaweza ukaendelea.

c) Na kwa kuwa serikali sikivu ya awamu ya sita, inayoongozwa na Rais Dr Samia Suluhu Hassan imeahidi kusikiliza na kurekebsha kasoro zote zilizoainishwa kwa maslahi ya taifa.

Hivyo basi, sisi BASUTA tusingependa kujikita kwenye mjadala wa vipengele mahususi wa Mkataba wenyewe wa bandari tukiamini mchakato unaenda vizuri na maslahi mapana ya taifa yatafikiwa.

2.0 Katika mjadala wa Mkataba huu, BASUTA haturidhishwi na undumilakuwili na ukosefu wa uadilifu wa wapingaji wa Mkataba ambao walifumbia macho mikataba mingi na ya hovyo zaidi huko nyuma katika sekta mbalimbali, ikiwemo madini, na hawakutaka ifutwe; lakini wako tayari kwa gharama yoyote kuhakikisha Mkataba huu unafutwa na unakufa. Wanasahau kuwa huu si Mkataba wa kwanza wa ukodishaji wa uendeshaji bandarini, bali awali ilipewa jukumu hilo kampuni ya TICTS na kufanya kazi hiyo kwa miaka takriban 22. Hadi TICTS inaondoshwa, hakujawahi kuwa na mijadala ya hisia kama hii kupinga sera za uwekezaji na eti kutaka Watanzania wenyewe ndio waendeshe rasilimali zao, kama lilivyodai kanisa Katoliki na wadau wengine.

3.0 BASUTA tunatambua na kuheshimu haki ya makundi ya watu wakiwemo wanasiasa, madhehebu ya dini, wasomi na wanahabari, kuwa na maoni, lakini haturidhishwi na baadhi ya hoja za kibaguzi dhidi ya Uarabu, na hata Uislamu zinazotolewa na makundi yanayotaka Mkataba huu wa bandari ufutwe. Badala ya kauli kama vile “Hatuwezi kuwapa Waarabu bandari zetu”, tunadhani jambo bora na la busara ni kujikita kwenye vipengele vya Mkataba kuainisha maeneo yenye udhaifu ili serikali iangalie namna ya kuboresha.

4.0 Vilevile, BASUTA inashangazwa na kusikitishwa na upotoshaji wa makusudi wa baadhi ya mambo katika mjadala wa Mkataba huu wa bandari, licha ya ufafanuzi uliotolewa na serikali, ikiwemo madai kuwa bandari inauzwa, DP World wanapewa waendeshe bandari zote na mengineyo.

Kipekee, tunasikitishwa sana na kauli isiyo na ushahidi wa kidodoso wa Kanisa Katoliki iliyodai eti wananchi wengi wanapinga Mkataba na wanataka ufutwe, ilihali hakuna utati kuhusu hilo uliofanyika.

BASUTA inashangazwa zaidi na makundi ya wapingaji kutotaka kusikiliza hoja zozote za ufafanuzi na kung’ang’ania misimamo.

Tunajiuliza, tatizo ni Mkataba tu au kuna waliyoyaficha vifuani mwao?

5.0 BASUTA tunasikitishwa na lugha za shinikizo na vitisho vya kuiangusha serikali kwa maandamano, fujo na vitendo vya jinai na uhaini. Iwapo kila kundi litataka matakwa yake yatimizwe kwa njia hizo, nchi inaweza kutumbukia katika machafuko makubwa.

Katiba inazungumzia haki ya kutoa maoni na kusikilizwa lakini haisemi lazima yafuatwe.

Utayari wa baadhi ya watu kuvuruga amani ili yao yatimie unazidi kutupa wasiwasi kuwa tatizo hasa sio Mkataba tu bali kuna chuki zilizojicha. Kwa kuliona hili, BASUTA tunatoa wito wa kuheshimiwa utawala wa sheria, hususan mfumo wa kukiwa maamuzi ya kiserikali katika uendeshaji wa nchi, kama yalivyoanishwa katika Katiba na Sheria za nchi kupitia vyombo rasmi kama Serikali, Bunge na Mahakama.

6.0 BASUTA imefurahishwa na kauli ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dr Samia Suluhu Hassan aliyoitoa Agosti 21, 2023 wakati akihutubia katika

sherehe za miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ya kuonesha

msimamo imara wa serikali na utayari wa kupambana na wanaotishia kuvuruga amani, pale aliposema: “Hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuligawa taifa hili…. wa kuivunja amani ya nchi yetu.”

7.0 Pamoja na kufurahishwa na msimamo wa Serikali, BASUTA tunaipa rai isikubali kuendeshwa kwa shinikizo la kundi lolote la kisiasa, kidini au kijamii na kufanya maamuzi kwa kutii matakwa ya kundi hilo kwani kwa kufanya hivyo itaendeleza mbegu mbaya iliyopandwa huko nyuma, ikamea na kuzaa tabaka la watu (wa aidha chama au dhehebu moja la dini) ambao ni raia zaidi kuliko wengine, na hivyo kuwa na kura ya

‘Veto’ katika maamuzi. Watu hao wasipolitaka jambo haliwi na wakilitaka huwa – tena kwa sababu ya maslahi yao binafsi.

8.0 Kwa msingi wa tuliyoyataja katika 4.0, kuhusu kauli za ubaguzi, tunawahimiza Watanzania wenzetu hususan viongozi wa dini, ambao kauli zao ndiyo hatari zaidi kwa sababu ya ushawishi mkubwa walionao, kujiepusha na matamko ambayo yanaweza kuipelekea nchi yetu katika laana ya uvunjifu wa amani kama ilivyotokea Rwanda 1994 na nchi nyingine.

Tunakumbusha kuwa katika baadhi ya nchi hizo, mambo yalianza hivi hivi kwa nyaraka namatamko ya kichungaji. BASUTA tusingependa kuyaona hayo yakitokea katika nchi yetu na tunatoa rai kwa serikali na vyombo vyake vya usalama viwe makini sasa kuliko wakati wowote ule.

9.0 BASUTA, kama tulivyotaja awali, tunaamini katika ukosoaji wenye afya wa kutaka maboresho ya baadhi ya vipengele vya Mkataba na sio upingaji wa jumlajumla wa kuukataa Mkataba wote.

Tunaamini aina ya pili ya upingaji unachangiwa zaidi na hisia kuliko hoja za msingi kwa ushahidi wa wazi wa kauli za chuki na ubaguzi dhidi ya Uarabu zinazotolewa na baadhi ya watu hususan mitandaoni na pia kwa ushahidi wa kampeni kubwa ya ‘kiimani’ ya Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) kupinga Mkataba huu kupitia kanisani.

Kwa msingi huo, BASUTA tunatoa rai kwa TEC na makundi mengine kutafakari upya misimamo yao kwa maslahi ya taifa na waweke pembeni hisia. Wakifanya hivyo, watagundua kuwa huu siyo Mkataba wa kwanza wa aina hii duniani na hata hivyo ipo nafasi ya maboresho. Pia, nchi nyingi duniani za Wakristo tena Wakatoliki zinafanya kazi na DP World zikiwemo Angola kupitia bandari ya Lobito yenye urefu wa kilometa 7.2 wakati gati la Dar es Salaam linalokusudiwa lina urefu wa kilometa 2 tu.

Pia, zipo nchi kama Msumbiji kupitia bandari ya Beira, Brazil na Ufiilipino.

Hivyo, mikataba ya DP World na nchi hizi itoshe kuwahikikishia kuwa uwekezaji huu unahusu biashara yenye tija kwa taifa, na sio kitu kingine.

10.0 BASUTA, tunaungana na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, kutahadharisha dhidi ya tabia ya kutumia majukwaa ya dini kwa maslahi ya siasa au kinyume chake, kwani kufanya hivyo kunaweza kuleta uvunjifu wa amani na kuharibu utulivu wa taifa.

Katika suala hili, tumesikitishwa kuona TEC inaendesha kampeni kubwa za kanisani kupinga Mkataba.

Iwapo mamlaka za dini nyingine zikianza kampeni kutetea Mkataba katika nyumba zao za ibada, tuna wasiwasi suala hili la kiuchumi halitaamuliwa kwa uzito wa hoja bali ufuasi wa dini.

Mheshimiwa Kikwete alionya: “Siku ikika uanachama wa chama cha kisiasa au uumini thabiti wa dini ukawianishwa na chama cha kisiasa anachokifuata ndiyo mwisho wa nchi yetu…kutakuwa na chama cha siasa cha Wakristo, cha Waislamu vyama vya siasa vya Walokole.

Kuwafanya Watanzania kuyatazama masuala ya kisiasa, Serikali na utawala kwa mtazamo wa dini zetu ni jambo hatari.”

11.0 Kwa kuwa imeibuliwa hoja ya ukomo wa Mkataba wa bandari, BASUTA inatoa wito wa kufanywa mapitio ya mikataba mingine isiyo na ukomo, ikiwemo ule ulioingiwa mwaka 1992 kati ya Serikali na makanisa (Memorandum of Understanding) ambapo sehemu ya mabilioni ya walipakodi, hata wasio Wakristo, hutolewa na serikali kwa ajili ya hospitali na vyuo vikuu vya makanisa hayo. Pia, tunataka makubaliano yanayozungumzwa mara kwa mara kati ya serikali na kanisa ya kutojengwa hospitali za umma mahali zilipo hospitali za makanisa yafutwe kwa sababu wananchi wana Mkataba na Serikali kuwakishia huduma za jamii kwa gharama wanayoweza kuzimudu na sio kanisa.

12.0 Hata hivyo, kwa ujumla, BASUTA inaungana na msimamo wa Serikali, Bunge na Mahakama Kuu kwamba Mkataba huu siyo tu ni sahihi bali pia ni muhimu kwa maslahi ya nchi.

Uwekezaji wa kampuni kubwa yenye uwezo wa mkubwa wa kimitaji na kiteknolojia, na yenye uzoefu na weledi kama DP World ya Dubai utaleta ufanisi katika biashara ya bandari hasa katika mazingira ya sasa ya ushindani mkubwa uliopo, na hivyo kuliwezesha taifa kuvutia nchi nyingi kutumia bandari zetu kupitisha mizigo yao na kuliingizia taifa mapato makubwa.

Angalizo:
Kuhusu vipengele vya mkataba wa bandari, majadiliano mengi yamefanyika huko nyuma na serikali Imeshatoa ufafanuzi dhidi y aupotoshaji unaofanywa hivyo BASUTA haikujikita katika mawanda hayo.

Hitimisho
Kwa maslahi ya umoja, mshikamano, utulivu na ustawi wa nchi yetu, tumetoa tamko letu hili kwa nia njema kabisa kwa maslahi ya nchi yetu na Watanzania wote pasina kujali dini, rangi, kabila, jinsia wala tofauti zao za kisiasa.

Tanzania ni kubwa kuliko sisi sote na wala baadhi yetu wasijitwishe ukiranja wa kuwasemea wengine ilhali wako hai na wanazo haki za kiraia kama walizo nazo wao.

Mungu Ibariki Tanzania.


My Take
TEC wamechokonoa vingi.
Leo hii adani yupo hapo bandarini na kampuni yoyote ya kitanzania haijazuiwa kuwekeza muda wowote ule katika bandari yoyote iliyopo ndani ya JMT.

Hiyo IGA tuliyodanganywa na wasomi kwamba inakwenda kuimiliki bandari nzima haina mabavu ya kumuondoa Adani na haitakuwa na mabavu ya kumuondoa muwekezaji mwingine yoyote atakayetaka kuwekeza kule Kigoma, kule Nyasa, kule Mtwara na Lindi.
 
Nchi hii ujinga ni wa kiwango cha juu, waliosema DPW wana mkataba mbovu wa IGA leo hii wapo kimya na pengine wanafaidika katika kupitishia mizigo yao pale TPA.

Oooh IGA hii mbaya na mbovu kabisa!, leo hii Adani yupo hapo hapo bandarini tena yeye ndio anayefanya biashara katika magati nyeti kuliko huyo DPW.

Maaskofu hawawezi kukwepa lawama za wao kutaka kumkwaza Rais SSH katika suala hili la uwekezaji pale bandarini.
Mkuu. Je ukisema chakula hiki sio kitamu na bado ukawa unakula basi ni shida ? Hwana jinsi na ni haki yao kutumia hiyo bandari
 
Mkuu. Je ukisema chakula hiki sio kitamu na bado ukawa unakula basi ni shida ? Hwana jinsi na ni haki yao kutumia hiyo bandari
Kusema haina maana kama huna uwezo wa kuthibitisha kwamba ni kichungu.

Maaskofu waliingizwa mkenge na watu ambao hawana utaalamu na masuala ya sheria za kimataifa. Pengine ni suala la dini ya hao wamiliki wa DPW kuwa ndio ile ile ya SSH.
 
Watetezi wa mkataba wa Bandari, wanaotaka masai waondolewe na wanaochekelea wakosoaji wa rais wakitekwa, kuteswa na kuuuwa ni watu wanaofanana. Ukiangalia hata wasimamizi wa huu uharamia wote wanafanana...
 
Kusema haina maana kama huna uwezo wa kuthibitisha kwamba ni kichungu.

Maaskofu waliingizwa mkenge na watu ambao hawana utaalamu na masuala ya sheria za kimataifa. Pengine ni suala la dini ya hao wamiliki wa DPW kuwa ndio ile ile ya SSH.
Walioingizwa mkenge ni wewe na unaofana nao ....TLS na wanasherio wote magwiji walisema ni mkataba wa kipumbavu. Hata hukumu ya ile kesi waliofungua akina mwabukusi kuna sehemu inaonyesha mapungufu ya ule mkataba sema walijifaya hawawezi kuingilia mhimilii mwingine. Unafikiri kwanini rufaa ya ile kesi inapigwa danadana?
 
Walioingizwa mkenge ni wewe na unaofana nao ....TLS na wanasherio wote magwiji walisema ni mkataba wa kipumbavu. Hata hukumu ya ile kesi waliofungua akina mwabukusi kuna sehemu inaonyesha mapungufu ya ule mkataba sema walijifaya hawawezi kuingilia mhimilii mwingine. Unafikiri kwanini rufaa ya ile kesi inapigwa danadana?
Uelewa wa sheria umepimwa kwa namna walivyoshindwa kuutafsiri huo mkataba, Hao TLS wasikutishe kwa jina lao kubwa walishindwa kuitafsiri IGA wakawapotosha mpaka maaskofu.

IGA haiwezi kuibana bandari eti isitafute mwendeshaji mwingine, pale bandarini kuna Adani, mhindi huyu kaja mwaka mmoja baada ya DPW na kwa sasa wanafanya kazi pamoja hapo hapo bandarini, hiyo IGA ingekuwa inatufunga kama kina Mwabukusi walivyodanganya umma hao Adani wangeweza vipi kuingia mkataba na Bandari wa kufanya shughuli za kiuendeshaji?.

Watu wangu wanateketea kwa kukosa maarifa. Hiyo rufaa haisikilizwi na haiwezi kusikilizwa kwa sababu ni upuuzi mtupu. Huyo Mwabukusi ni mweupe sana kwenye masuala ya kisheria na nia aibu kuiongoza taasisi kubwa ya TLS.
 
Uelewa wa sheria umepimwa kwa namna walivyoshindwa kuutafsiri huo mkataba, Hao TLS wasikutishe kwa jina lao kubwa walishindwa kuitafsiri IGA wakawapotosha mpaka maaskofu.

IGA haiwezi kuibana bandari eti isitafute mwendeshaji mwingine, pale bandarini kuna Adani, mhindi huyu kaja mwaka mmoja baada ya DPW na kwa sasa wanafanya kazi pamoja hapo hapo bandarini, hiyo IGA ingekuwa inatufunga kama kina Mwabukusi walivyodanganya umma hao Adani wangeweza vipi kuingia mkataba na Bandari wa kufanya shughuli za kiuendeshaji?.

Watu wangu wanateketea kwa kukosa maarifa. Hiyo rufaa haisikilizwi na haiwezi kusikilizwa kwa sababu ni upuuzi mtupu. Huyo Mwabukusi ni mweupe sana kwenye masuala ya kisheria na nia aibu kuiongoza taasisi kubwa ya TLS.
Kwani nchi hii kunq kufuata sheria...kwa sababu hao wengine wamekuja bandarini ndiyo umeona akina Issa Shivji na magwiji wengine wamekosea? Wenyewe wameutafsiri mkatabata kama ulivyo na ni rubbish hata kwa mtu asiye jua jua sheria.
 
Kwani nchi hii kunq kufuata sheria...kwa sababu hao wengine wamekuja bandarini ndiyo umeona akina Issa Shivji na magwiji wengine wamekosea? Wenyewe wameutafsiri mkatabata kama ulivyo na ni rubbish hata kwa mtu asiye jua jua sheria.
Wamewaingiza chaka kina nyinyi msioelewa chochote. Huwezi kuutafsiri mkataba kwa kutazama kifungu kimoja tu, Ule ulikuwa na vifungu 24 vinatafsiriwa vyote kwa pamoja.

IGA haiizui serikali yetu kuwa na mwendeshaji mwingine kwenye bandari zetu na pia pale pale bandarini TPA.

DPW anaaendesha magati namba 4 mpaka 8 pekee. Adani anaendesha magati namba 9 mpaka 11. Na TPA kama mwenyeji anaendesha magati namba 0 mpaka namba 3 pekee.

Mfano, wewe na mimi tunaweza kuwa tunaifahamu kampuni nyingine yenye uwezo wa kuendesha bandari tukaenda wizara ya mawasiliano na uchukuzi tukaiomba kuendesha bandari ya Mtwara au ya Tanga na tutapewa tenda ya kuendesha ikiwa lipo tangazo la wizara lenye kuita waendeshaji kwa ajili ya bandari hizo na hiyo IGA ya DP World haina nguvu ya kutufanya lolote.
 
Back
Top Bottom