Hata ukiwauliza wapinzani walete ushahidi wa kuibiwa hawana zaidi watakuletea karatasi za kupigia kura fake!
Kumbuka kuna ushahidi wa mazingira na kuna ushahidi wa vielelezo!
Vielelezo tayari wapinzani wanavyo hadi vya picha na video, sema tu havijarushwa hapa sababu ya shinda ya mitandao! Au hukumuona mgombea wa CHADEMA akionyesha moja ya karatasi origional ilotumika kupigia kura ambayo walikamata katika moja ya majimbo hapa bongo?
Ushahidi wa mazingira nao ni mwingi tu:-
1.Rejea mgombea wa CUF jimbo la Temeke ambaye alipata kura 0 (SIFURI) kwenye kituo kwenye kituo ambacho alipiga kura yeye mwenyewe na wanafamilia 7, Na hapakuwa kura hata moja iliyoaharibika, Je hizi kura zote 8 zilienda wapi?
3.Hata riport za baadhi mashirika kama CIP zinaonyesha kwamba wananchi waliojitokeza kupiga kura mwaka huu walikuwa wachache sana,! Je kura milioni 15 zilitoka wapi???
3.Tangu tuanze mfumo wa vyama vingi CCM Zanzbar haikuwahi kushinda kwa Zaidi ya asilimia 69% inapochuana na Maalim Seif Au Seif hakuwahi kupata chini ya asilimia 40, Je kwa kuzingatia hali halisi ilivyokuwa wakati wa kampeni Je wewe unaona yale matokeo ni fair and just?
4.Kwa kuzingatia hali halisi ya kampeni zilivyokuwa na historia halisi ya mikoa kama Dasm, Mbeya,Kilimanjaro, Arusha, Lindi, Mtwara, Iringa,Njombe na Songwe, Je ni Wapinzani wanaweza kukosa jimbo hata moja kwenye mikoa hiyo???
........... Hapa hata bila miwani mbona kila kitu kinaonekana wazi? Tuweni na hofu ya Mungu, ni bora kukaa kimya kuliko kusuport kitu ambacho unajua kabisa si kweli!!!