Tamko la Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) kumtaka Freeman Mbowe kuomba radhi

Ulimwengu wa Wanahabari na Watanzania kwa ujumla ulipigwa na butwaa pale Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Alkaeli Mbowe, alipoamrisha waandishi wa habari wa Televisheni ya Taifa (TBC) kuondoka katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za chama hicho, uliofanyika kwenye viwanja vya Mbagala Zackem jijini Dar es Salama kwa tuhuma za kwamba wanafikiri wao ni televisheni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika amri yake Mhe. Mbowe alitoa dakika 15. Kwa waandishi hao kuwa wamefunga vyombo vyao na kuondoka katika eneo la mkutano huo kwa madai kwamba TBC ilikuwa imesitisha matangazo ya mkutano huo ambayo awali yalikuwa yakirushwa mubashara.

Mbowe alisema wamechoka kuonewa na kufanywa wapumbavu hivyo aliwapa dakika 15 wawe wameondoka kwenye viwanja vya mkutano.

Kwa vipimo vyovyote vya kimaadili kitendo hicho kilikosa uungwana na hakikubeba misingi ya kiutu hata kama zilikuwepo dalili zozote za kukatishwa kwa matangazo hayo au huko kufanywa wapumbavu kama alivyosema Mhe. Mbowe.

Kitendo kile ambacho kilikosa busara na ukomavu wa kisiasa siyo tu kiliwadhalilisha na kuwafedhesha waandishi wale pamoja na taaluma yao isipokuwa zaidi kilihatarisha usalama wao na vifaa vyao kutokana na mazingira yaliyokuwepo.

Kutokana na hali hiyo ambayo haivumiliki hasa katika kipindi hiki cha kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 sisi DCPC ni klabu huru ya waandishi wa habari mkoa wa Dar es salaam, wakati tukiendelea kutafakari hatua sahihi za kuchukua kwa kushirikiana na wadau wengine wa habari mkoani humu, inachukua nafasi hii kukemea na kulaani kitendo kile pamoja na kumtaka Mhe. Mbowe kuomba radhi kwa waandishi wale, Televisheni ya taifa, tasnia ya habari, pamoja na Watanzania kwa ujumla.

Tasnia ya habari ni nyenzo muhimu katika upashanaji wa habari hasa nyakati hizi za kampeni za kisiasa na uchaguzi wananchi wanahitaji kujua sera, ilani na mipango ya vyama vya siasa kabla ya kupigakura. Na kwa vyovyote hakuna njia rahisi ya wananchi kuyapata yote hayo kama si kupitia vyombo vya habari ambavyo CHADEMA imeamua kuwadhalilisha.

DCPC inaungana na vyombo, taasisi na watu wote ambao wamekerwa na kitendo kile na inaviasa vyama vingine vyote kujiepusha na mihemuko inayoweza siyo tu kudhalilisha taaluma ya habari lakini pia kuwatia hatarini waandishi wa habari wanapokuwa kazini.

Mwenyekiti DCPC
Irene Mark
01.09.2020
Kama Mbowe amewakera si muende kuchukua picha na kuandika habari za mikutano ile inayojaa ng'ombe wanaosombwa na matrekta?? Kwani ni lazima muandike kuhusu Chadema??? Kaandikeni kuhusu kale ka kikundi ka CCM!
 
wacha kufukuzwa me ningesema wa chapwe bakora
 
We DCPC hivi unajua kuwa wananchi wengi wanafahamu kuwa chombo hiki kinatoa huduma zake kwa upendeleo? Hata Jana TBC yenu ilikata wakati Bwege akitoa yake ya moyoni huko Lindi.Kwani mtu akifanya makosa si sheria ichukue mkondo wake? TBC kama ni chombo cha umma kingelifanya haki kwa wote sio ilivyo ss kwanzia asubuhi had I usiku mnaonyesha stiglas tu.Hivi wakishinda hao mnaowachukia mtaweka wapi nyuso zenu. Nendeni na muda
 
kwa sentensi hii ni na mashaka kama hawa watu hawatakuwa wamenunuliwa na kutumika , nanukuu,

''''' Kutokana na hali hiyo ambayo haivumiliki hasa katika kipindi hiki cha kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu''' .

kwenu haivumiliki , TBC aidha inavumilika , hamjui siasa ina makorokoro mengi ya hila . Mmoja wapo kaona hila na yeye kachukua hatua . ili wasikwazane . Tangu lini shetani akalipeleka kanisa la yesu mbinguni na hata kusema nililichunga vyema , haipo hiyo . shetani hubaki ni shetani tu .
Hao ni vibaraka wa CCM.Huyo Irene Mark aliyesema tamko anafanya kazi ofisi ya CCM.Ni marapeli wa habari
 
Ni lini Tbc wameandika mema ya Chadema? Kuna faida gani ya wao kuwepo kwenye mikutano ya Chadema kama haitaandika na kuripoti mema yao? Chadema haina chochote cha kupoteza zaidi ya kutoa onyo na fundisho kwa hao wanafiki. Tbc jirekebisheni kama chombo cha umma, kinachoendeshwa kwa kodi za waTz wote bila kujali itikadi zao.

Anyway, nimesoma mahali kuwa huyo dada alietoka hilo tamko la klabu ya waandishi ni kada mtiifu wa ccm, hivyo anatumika tu.
 
Ulimwengu wa Wanahabari na Watanzania kwa ujumla ulipigwa na butwaa pale Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Alkaeli Mbowe, alipoamrisha waandishi wa habari wa Televisheni ya Taifa (TBC) kuondoka katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za chama hicho, uliofanyika kwenye viwanja vya Mbagala Zackem jijini Dar es Salama kwa tuhuma za kwamba wanafikiri wao ni televisheni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika amri yake Mhe. Mbowe alitoa dakika 15. Kwa waandishi hao kuwa wamefunga vyombo vyao na kuondoka katika eneo la mkutano huo kwa madai kwamba TBC ilikuwa imesitisha matangazo ya mkutano huo ambayo awali yalikuwa yakirushwa mubashara.

Mbowe alisema wamechoka kuonewa na kufanywa wapumbavu hivyo aliwapa dakika 15 wawe wameondoka kwenye viwanja vya mkutano.

Kwa vipimo vyovyote vya kimaadili kitendo hicho kilikosa uungwana na hakikubeba misingi ya kiutu hata kama zilikuwepo dalili zozote za kukatishwa kwa matangazo hayo au huko kufanywa wapumbavu kama alivyosema Mhe. Mbowe.

Kitendo kile ambacho kilikosa busara na ukomavu wa kisiasa siyo tu kiliwadhalilisha na kuwafedhesha waandishi wale pamoja na taaluma yao isipokuwa zaidi kilihatarisha usalama wao na vifaa vyao kutokana na mazingira yaliyokuwepo.

Kutokana na hali hiyo ambayo haivumiliki hasa katika kipindi hiki cha kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 sisi DCPC ni klabu huru ya waandishi wa habari mkoa wa Dar es salaam, wakati tukiendelea kutafakari hatua sahihi za kuchukua kwa kushirikiana na wadau wengine wa habari mkoani humu, inachukua nafasi hii kukemea na kulaani kitendo kile pamoja na kumtaka Mhe. Mbowe kuomba radhi kwa waandishi wale, Televisheni ya taifa, tasnia ya habari, pamoja na Watanzania kwa ujumla.

Tasnia ya habari ni nyenzo muhimu katika upashanaji wa habari hasa nyakati hizi za kampeni za kisiasa na uchaguzi wananchi wanahitaji kujua sera, ilani na mipango ya vyama vya siasa kabla ya kupigakura. Na kwa vyovyote hakuna njia rahisi ya wananchi kuyapata yote hayo kama si kupitia vyombo vya habari ambavyo CHADEMA imeamua kuwadhalilisha.

DCPC inaungana na vyombo, taasisi na watu wote ambao wamekerwa na kitendo kile na inaviasa vyama vingine vyote kujiepusha na mihemuko inayoweza siyo tu kudhalilisha taaluma ya habari lakini pia kuwatia hatarini waandishi wa habari wanapokuwa kazini.

Mwenyekiti DCPC
Irene Mark
01.09.2020

chadema wanayo haki ya kufanya walivyofanya. media ya Tz inaogopa dola na serikali inawakaba mno wasitoe habari za upinzani. Inaudhi kweli na kwa dhati kaabisa hongerezeni sana chadema kwa kuwafukuza TBC wajinga wakubwa.
 
Taaluma ya Wana habari ushauri unaeza kupokea au usipokee sababu ya kudharaulika katika jamii ni mambo Kama haya waacheni wanasiasa na siasa zao nyie simamieni misingi ya haki sawa, misingi ya taaluma zenu katika kuwasilisha taarifa mbele ya jamii...hizi chokochoko zitaenda zaidi y chedema zaidi y Mh Mbowe bakieni kwenye njia yenu mengine ziwe story tuu
 
Ulimwengu wa Wanahabari na Watanzania kwa ujumla ulipigwa na butwaa pale Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Alkaeli Mbowe, alipoamrisha waandishi wa habari wa Televisheni ya Taifa (TBC) kuondoka katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za chama hicho, uliofanyika kwenye viwanja vya Mbagala Zackem jijini Dar es Salama kwa tuhuma za kwamba wanafikiri wao ni televisheni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika amri yake Mhe. Mbowe alitoa dakika 15. Kwa waandishi hao kuwa wamefunga vyombo vyao na kuondoka katika eneo la mkutano huo kwa madai kwamba TBC ilikuwa imesitisha matangazo ya mkutano huo ambayo awali yalikuwa yakirushwa mubashara.

Mbowe alisema wamechoka kuonewa na kufanywa wapumbavu hivyo aliwapa dakika 15 wawe wameondoka kwenye viwanja vya mkutano.

Kwa vipimo vyovyote vya kimaadili kitendo hicho kilikosa uungwana na hakikubeba misingi ya kiutu hata kama zilikuwepo dalili zozote za kukatishwa kwa matangazo hayo au huko kufanywa wapumbavu kama alivyosema Mhe. Mbowe.

Kitendo kile ambacho kilikosa busara na ukomavu wa kisiasa siyo tu kiliwadhalilisha na kuwafedhesha waandishi wale pamoja na taaluma yao isipokuwa zaidi kilihatarisha usalama wao na vifaa vyao kutokana na mazingira yaliyokuwepo.

Kutokana na hali hiyo ambayo haivumiliki hasa katika kipindi hiki cha kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 sisi DCPC ni klabu huru ya waandishi wa habari mkoa wa Dar es salaam, wakati tukiendelea kutafakari hatua sahihi za kuchukua kwa kushirikiana na wadau wengine wa habari mkoani humu, inachukua nafasi hii kukemea na kulaani kitendo kile pamoja na kumtaka Mhe. Mbowe kuomba radhi kwa waandishi wale, Televisheni ya taifa, tasnia ya habari, pamoja na Watanzania kwa ujumla.

Tasnia ya habari ni nyenzo muhimu katika upashanaji wa habari hasa nyakati hizi za kampeni za kisiasa na uchaguzi wananchi wanahitaji kujua sera, ilani na mipango ya vyama vya siasa kabla ya kupigakura. Na kwa vyovyote hakuna njia rahisi ya wananchi kuyapata yote hayo kama si kupitia vyombo vya habari ambavyo CHADEMA imeamua kuwadhalilisha.

DCPC inaungana na vyombo, taasisi na watu wote ambao wamekerwa na kitendo kile na inaviasa vyama vingine vyote kujiepusha na mihemuko inayoweza siyo tu kudhalilisha taaluma ya habari lakini pia kuwatia hatarini waandishi wa habari wanapokuwa kazini.

Mwenyekiti DCPC
Irene Mark
01.09.2020
Waandishi wanatumika vibaya
 
Dah...bado nasisitiza ....CDM watafute sababu yoyote ... Wajitoe au wavuruge uchaguzi...hata kama ni ya kipuuzi [emoji2960]
 
Back
Top Bottom