Tume Haki Binadamu(THBUB)
Member
- Sep 17, 2024
- 27
- 28
Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani,THBUB yatoa tamko
Tamko la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei 1, 2025
Tarehe 1 Mei kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani. Maadhimisho haya yamelengwa katika kutambua mchango wa wafanyakazi duniani kote katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi kwa mwaka 2025 nchini yanaongozwa na kauli mbiu isemayo:
"Uchaguzi Mkuu 2025 Utuletee Viongozi Wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi, Sote Tushiriki"
Kauli mbiu hii inawahamasisha Wafanyakazi kujitokeza kushiriki katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka huu 2025 ili kuhakikisha kwamba pamoja na wananchi wengine wanawachagua viongozi wenye kuheshimu na kulinda haki za binadamu na kusimamia misingi ya utawala bora wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
THBUB inawakumbusha wafanyakazi kuwa upatikanaji wa viongozi waadilifu utapunguza malalamiko ya wafanyakazi hasa katika masuala yanayohusu maslahi yao binafsi.
Wakati maadhimisho haya yakifanyika, THBUB inatambua na kupongeza juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika...