Ukisoma hiyo document utajua kuwa Balozi wa Marekani wa sasa hivi upeo wake ni mdogo au anatatizo lingine.
Kwanza
Balozi anaanza na Uchaguzi ulikua wa amani na watanzania waliruhusiwa kupiga kura nchi nzima kwa uhuru.Kauli hii inapingana na kauli ya dhana ambayo anaonekana kuiamini na kuipa msisitizo.Ni wazi kuwa kama asinge anza na kauli ya hapo juu kuwa Uchaguzi ulikua huru hakuna Mtanzania yeyote hata wale wa vyama vya upinzani ambao wangemuamini kwani kila mtanzania aliongea na kuthibitisha mazingira mazuri ya upigaji kura ikiwa ni pamoja na ulinzi na taratibu zingine.
Pili
Anasema waandamanaji walishikwa,alitaka waandamanaji waachiwe ili itokee fujo!.Kwenye kuzuia machafuko best practice ni kuzuia dalili za machafuko.Upuuzi anaooongea Balozi ni kudhihirisha nia yake ya kuona damu inamwagika katika uchaguzi huu.
Tatu
Uchochezi wa Balozi wa marekani unaendelea kwa kudanganya umma wa Watanzania kuwa zipo kura zilizopigwa mara mbili,zipo kura zilizopigwa kumpigia mgombea kabla ya siku ya kura na wapo mawakala walinyimwa au kuondolewa vituoni.Madai haya ni ya kutengeneza kwa lengo lile lile la kuhatarisha amani ya nchi
Nne.
Balozi wa Marekani kwa kutumia mbinu za kijinga anataka suala la uchaguzi liendelee,kwa kuruhusu maandamano.Nchi hii ni huru na uchaguzi umeisha.Hivyo uhuni wa Balozi kutaka kuwashughulisha Watanzania na maaandamano ni jambo lisilokubalika.Tuna mengi ya kufanya,watu wanapaswa kuwa kazini.