Pre GE2025 Tamko zito la vijana CCM wa vyuo vikuu waunga mkono Rais Samia na Dkt.Mwinyi kugombea urais 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Umaskini mbaya Sana, Wacha wawe machawa tu,
Eti wasomi! Palestina kapigwa na kuuliwa, kila Leo, hatujaona tamko Lao, Vita ya ukraine, hatujaona tamko Lao, uchaguzi, wa, USA, hatujaona uchambuzi wao, ila tu wameamka waliposikia ccm/samia, ni mwendo wa kutembea na nyota!
Unakuwa chawa leo wa samia, akitoka kesho, unasahaulika, so stupid
 
Dodoma, Tanzania

Vijana na Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mohammed Kawaida na Katibu Mkuu Jokate Mwegelo wamesema wako tayari kuhakikisha Wagombea wa nafasi ya Urais waliopitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM 2025, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, wanashinda kwa kishindo.

Mwenyekiti wa UVCCM Mohammed Kawaida amesema hayo baada ya Vijana kufanya matembezi ya hisani katika Jiji la Dodoma ikiwa ni kuunga mkono maamuzi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu uliofanyika January 18 na 19,2025 na kuwapitisha Dkt.Samia na Dkt. Mwinyi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa UVCCM Jokate Mwegelo amesema matembezi hayo ni ahadi walioiweka ili kuunga mkono maamuzi ya Wajumbe na hivyo wako tayari kuhakikisha adhima ya kuhakikisha Chama kinaendelea kushika Dola ipo mikononi mwa Vijana kwani Mgombea mwenza wa Urais kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Emmanuel John Nchimbi ni zao la UVCCM.

Zaidi ya Vijana 1000 wakiwemo Wanafunzi wa Vyuo na Vyuo Vikuu, baadhi ya Wenyeviti wa Mikoa na Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Vijana Ng’wasi Kamani wameingia barabarani na kupitia Mitaa mbalimbali ya jiji la Dodoma kufanya matembezi hayo
 
UVCCM WAJIFUNZE KUTOKA CHADEMA NA NCHI ZINGINE VIJANA KUCHUKUA NAFASI ZA MAAMUZI

KUTOKA MAKTABA:

VIJANA NA MABADILIKO, WAKATI HUU 2024 / 2025 NI SAHIHI KUINGIA KTK NAFASI ZA MAAMUZI IKIWEMO URAIS


Duniani ni vijana wa vyuo vikuu ndiyo wanaoongoza kuchagiza mageuzi, Vijana ni taifa la leo, watoto ndiyo viongozi wa kesho. Kauli za kilaghai kuwa vijana ni kwa ajili ya taifa la kesho siyo sahihi.

Vijana msihofu msuguano na wazee waliopo mamlakani, kusubiri kupewa ni kukubali kuwa tumejumuishwa na watoto chipukizi. Ni wakati wa vijana kuchagiza kwa mbinyo wa hoja kuwa uongozi wa nchi ni kwa ajili ya vijana.

Historia inaonesha mara baada ya uhuru wa kwanza kupatikana ktk mtaifa mbalimbalii iwe kwa mtutu wa bunduki au maandamano ya kuondoa wakoloni, baadaye kulifuatia msuguano wa wananchi wenyewe kwa wenyewe kwa kutoridhishwa na wale waliochukua utawala toka kwa wakoloni.

Sababu mbalimbali zilizua msuguano ktk nchi huru kama udiktekta, tawala kamdamizi ya chama kimoja kongwe, utawala mbovu, ubaguzi wa kielimu mfano mtoto aliyesoma shule za kata / st. Kayumba anadanganywa kuwa akihitimu chuo kikuu atakuwa na nafasi sawa na mwenzake aliyesoma St. Mary's akamaliza elimu ya chuo kikuu pia anayekimanya kiingereza vizuri zaidi na wajomba wake wapo ktk nafasi za kiutawala n.k

Hapo ndipo Wanafunzi waliopo ktk nchi kama Sudan, Chile, Cuba, Afrika ya Kusini, Kenya walishiriki kudai mageuzi ili kuondokana na tawala zilizomgoa mkoloni.

Tanzania vijana hawajishughulishi kuhoji mambo yasiyowaridhisha wananchi kama bandari kuchukuliwa kuwa vituo vya nchi ngeni, matumizi mabaya ya kodi za wananchi, tozo zilizokifu wananchi, demokrasia kubinywa, katiba kandamizi n.k

Huko Chile marekani ya kusini nchi iliyo viongozi wa vyama vya wanafunzi wenye kushiriki kikamilifu katika siasa pia maandamano imewezesha kiongozi kijana wa wanafunzi Gabriel Boric ambaye ndiye rais kijana kabisa wa kuchaguliwa amezaliwa 11 February 1986 ambaye alichukua madaraka ya urais tarehe 11 March 2022 baada ya kushinda uchaguzi mkuu nchini Chile tarehe 19 December 2021 kwa kupata asilimia 60% ktk uchaguzi wa urais.

Gabriel Boric on the Chilean student movement 14 June 2017
Mwanafunzi wa chuo kikuu Tanzania toka familia masikini anazama ktk mkondo wa madeni ya fedha za mkopo wa elimu ya juu huku akiwa anaimani na matumaini potofu ya Ilani ya CCM imeandika ahadi ya mambo ya uongo ya kupata ajira, mazingira ruhani kuwa wataweza kupata vyeo vya ulaji vya kisiasa UVCCM, kuwa MNEC Halmashauri Kuu ya CCM, mbunge wa CCM n.k au kuwepo mazingira (hewa) ya kujiajiri.

VIJANA NI WAKATI WA KUACHA KUTEGEMEA CHAMA DOLA KONGWE


Picha maktaba : Vijana chawa wa Vyuo vya elimu ya juu Tanzania.

Vijana vyuo vikuu na mijini pia vijijini badala ya kumezwa na ukiritimba wa UVCCM na ahadi kuwa ni viongozi wa kesho huku watoto wa vigogo wa CCM wanapewa nafasi sasa na siyo kesho wanatakiwa kuunda chombo chao kipya cha kutambulika kama mdau muhimu anayehitaji kuonekana katika majukwaa ya siasa pia ktk vituo vya redio, televisheni na mitandao ya kijamii kuchagiza mabadiliko na mageuzi ikiwemo pia kupewa nafasi nje ya mfumo wa vyama ili wagombee nafasi za kuchaguliwa na wananchi.

VIJANA KULE CHILE BARA LA LATINO AMERIKA WAMEWEZA

Gabriel Boric - The 100 Most Influential People of 2022 - TIME

time.com › collection › gabriel-boric


23 May 2022 Ā· He is making Chile the social, economic, and political laboratory of the world once again. Stiglitz is a Nobel Prize–winning economist
 
Kama wasomi ndio wanaandika hivi basi tutakuja kupata viongozi wasiojua hata lugha yetu ya Kiswahili.

Vv

Ndiyo wenzetu hao wa UVCCM wa chama dola kongwe wanaoongoza nchi, kutunga sera ya elimu, uchumi n.k
 
Wanakwenda na upepo, ukienda kulia wamo, kushoto wamo, kaskazini wamo, kusini wamo.
Kuna wengine wanaimba nyimbo huko sijui za birthday km hawana akili nzuri.
Unafiki ni janga kubwa sana Balopee Tanzanie.
 
Kudadeki, Tanzania kuna wajinga wengi sana, hata lugha yako tu huijui alafu unaanzisha mada
 
Hawa jamaa wanatumika vibaya sana
 
Hawa jamaa wanatumika vibaya sana
UVCCM na wakubwa wao CCM na jumuiya zake WAZAZI, UWT, BAKWATA, mabaraza ya maaskofu n.k zinatumika kuharibu bongo za vijana wasiwe na uwezo wa kujitambua wala kusoma muekeleo wa nchi ili wasijiulize.

Kama taifa je linakwenda uelekeo sahihi au la, vijana wa CCM hawawezi kuhoji / ku- challenge wazee wao kifikra kama vijana wanaojitambua waliopo BAVICHA CHADEMA.
 
Kuna muda unajiuliza Hawa watu huwa wanapewa Nini Hadi kinawabadili uwezo wao wa kufikiri?
 
Vijana wasomi wa UVCCM jimbo la Ubungo Dar es Salaam watetea fomu moja kwa mheshimiwa rais Dr. Samia Suluhu Hassan


View: https://m.youtube.com/watch?v=NH4Se4sWQ3sUbungo leo vijana wa Chuo cha Maji, UDSM mlimani na Chuo Kikuu cha Ardhi walio wanaUVCCM wamesisitiza kujitosa kugombea nafasi zote ngazi za udiwani, ubunge na ndani ya CCM, ila nafasi ya Urais ni nafasi ya Mwenyekiti Samia Suluhu Hassan ...

wasomi wa UVCCM jimbo la Ubungo Dar es Salaam wameongeza maridhiano ni baina ya CCM na watanzania wote.

Na kusisitiza kuwa masuala ya maridhiano siyo kwa ajili ya kungumza na Tundu Lissu, John Heche hilo chama cha CHADEMA inapaswa kulifahamu, na kuwa maridhiano yahawezi kutekwa nyara na viongozi hao wa juu wa CHADEMA waliotangaza :No Reforms No Elections " ...
 
... msiwalaumu hao Watoto, siku hizi vyuo havilei 'RADICALS' kama enzi na Mwalimu!
... hata enzi za Mwalimu ukiingia kichwakichwa ilikuwa inakula kwako!
 
Eti awa ndo think tank wa taifa la kesho, twendako taifa litakua na vilaza wengi sana
 

KIJANA MZALENDO AIVAA CCM "HIKI NI KITUKO WAMEVUNJA KATIBA CCM KAMA WANAMPENDA SAMIA HARAKA YA NINI"


View: https://m.youtube.com/watch?v=9Vdp5kcgCt4
Mashaka N'kindikwa asema katiba ya chama cha CCM na kanuni zake zimevunjwa.


Kijana maarufu wa UVCCM anayejitambulisha kuwa ni mtanzania mzalendo ndugu Mashaka N'kindikwa asema katiba ya chama cha CCM na kanuni zake zimevunjwa, huku akifanya rejea ya vitabu viwili kimoja cha katiba na cha pili kitabu cha kanuni za CCM


Mashaka N'kindikwa alisema hiki ni kituko cha karne walichofanya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa tarehe 18 January 2025 Dodoma , Tanzania. Na maana yake hakuna uhalali wa uteuzi uliopitishwa kinyume cha katiba na kanuni za chama.

Pia kada huyu wa UVCCM akaongeza tulimuona rais mstaafu Jakaya Kikwete alistuka na kuhoji wajumbe wa mkutano mkuu kama mnajua hiki mnacho shangilia ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…