Tamthilia ya Zahanati Kijijini

Tamthilia ya Zahanati Kijijini

Leo tena kwa Tausi
Makubwa Yarabii
Mtoto una ngendebwe wewe[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Akija mama yako anamtaka Mbiki
Wewe ukija unamtaka Tausi
Sisi wengine tukalale majumbani kwetu?

Odama nae sura ambavyo huwa anaiweka lo ananikeraa
 

Attachments

  • BE227CA3-298E-497F-8740-AA70CAB4EF06.jpeg
    BE227CA3-298E-497F-8740-AA70CAB4EF06.jpeg
    648 KB · Views: 8
  • 698648EA-E7A2-40F9-8775-E6D6BE5109A2.jpeg
    698648EA-E7A2-40F9-8775-E6D6BE5109A2.jpeg
    509.5 KB · Views: 10
  • 447191F2-C8C0-464C-8953-98D01C960FB7.jpeg
    447191F2-C8C0-464C-8953-98D01C960FB7.jpeg
    747.1 KB · Views: 8
Wakuu habarii,

Kiukweli nianze kwa kukiri kuwa Mimi binafsi sio Mpenzi wa Tamthilia/Filamu za hapa nyumbani Almaarufu kwa Jina la Bongo Movie lakini Siku Moja Majira ya saa 1 usiku nilipokosa cha kufanya nikiwa Sebuleni nilikutana na Tamthilia tajwa hapo juu ikiwa inaonyweshwa kupitia Channel ya Sinema Zetu inayopatikana katika King'amuzi cha Azam.

Kiukweli baada kuiangalia nilivutiwa mno na Tamthilia hiyo huku nikivutiwa zaidi na Wahusika wake, Ubora wa Sauti na Picha sambamba na Mazingira waliyoigizia kwakweli hongera Director kwa kazi nzuri.

Mwisho nahitimisha kwa kusema kuna haja sasa kwa Waongozaji wa Tamthilia na Filamu hapa Nchini kuhakikisha wanaandaa Kazi katika viwango vya juu pamoja na kutunga Story zenye kuakisi Maisha ya Watanzania walio wengi ili ziweze kupata Netflix nk.

Nawasilisha
KUKUMSELA.
Ni vizuri kuona kuwa unapenda tamthilia na filamu za hapa Tanzania na unatambua ubora wa kazi zinazofanywa na wasanii wetu. Ni kweli kuwa kuna haja ya kuwa na viwango vya juu na kuzingatia ubora wa sauti, picha, mazingira, na hadithi zinazoigizwa ili kuvutia watazamaji na kuwafanya wawe na hamu ya kuangalia tena na tena.

Kuhusu kutunga hadithi ambazo zinaakisi maisha ya watu wa Tanzania, hii ni muhimu sana kwa sababu itawawezesha watazamaji kutambua na kuhusiana na hadithi hizo. Ni muhimu kwa waongozaji kuzingatia hadithi ambazo zinahusisha mambo ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni ambayo ni muhimu kwa Watanzania na pia kuzingatia tofauti za tamaduni kwa Tanzania nzima.

Kuhusu kutangaza kazi zetu kimataifa, kuna fursa nyingi zinazopatikana kwa njia ya majukwaa kama vile Netflix, Amazon Prime, na nyinginezo. Ni muhimu kwa waongozaji kuhakikisha kuwa wanatuma kazi zao kwa majukwaa haya ili kuongeza usambazaji na kupata watazamaji kimataifa.
 
Back
Top Bottom