Wakuu habarii,
Kiukweli nianze kwa kukiri kuwa Mimi binafsi sio Mpenzi wa Tamthilia/Filamu za hapa nyumbani Almaarufu kwa Jina la Bongo Movie lakini Siku Moja Majira ya saa 1 usiku nilipokosa cha kufanya nikiwa Sebuleni nilikutana na Tamthilia tajwa hapo juu ikiwa inaonyweshwa kupitia Channel ya Sinema Zetu inayopatikana katika King'amuzi cha Azam.
Kiukweli baada kuiangalia nilivutiwa mno na Tamthilia hiyo huku nikivutiwa zaidi na Wahusika wake, Ubora wa Sauti na Picha sambamba na Mazingira waliyoigizia kwakweli hongera Director kwa kazi nzuri.
Mwisho nahitimisha kwa kusema kuna haja sasa kwa Waongozaji wa Tamthilia na Filamu hapa Nchini kuhakikisha wanaandaa Kazi katika viwango vya juu pamoja na kutunga Story zenye kuakisi Maisha ya Watanzania walio wengi ili ziweze kupata Netflix nk.
Nawasilisha
KUKUMSELA.