TANAPA: Kwanini hakuna "Mobile Zoos" kwa ajili ya kubebea wanyama pori wepesi kama ambavyo kuna Mobile Courts?

TANAPA: Kwanini hakuna "Mobile Zoos" kwa ajili ya kubebea wanyama pori wepesi kama ambavyo kuna Mobile Courts?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kwanini TANAPA hawana "Mobile Zoos" kwa ajili ya kubebea wanyama pori wepesi kwa ajili ya maonesho kama ambavyo kuna Mobile ATMs, Mobile Court pamoja na Mobile Hospitals?

images (11).jpg


MWEZI FEBRUARY MWAKA 2019: Rais John Magufuli wa Tanzania amezindua gari maalumu la mahakama inayotembea litakalosaidia kusikiliza kesi katika mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam. Uzinduzi wa gari hilo lenye teknolojia ya kisasa ndani yake na linalotumia umeme wa jua katika uendeshaji vifaa hivyo umefanyika leo katika maadhimisho ya Siku ya Sheria.

Gari hilo limegharimu kiasi cha Shilingi milioni 470.82. Gari hilo lenye television, kamera zenye uwezo wa kurekodi ushahidi wote kwa picha na sauti, kutoa msaada wa kuwabeba watu wenye ulemavu (lifti) na kipaza sauti kwa ajili ya kutangaza ratiba ya mahakama hiyo, linatazamiwa kusaidia uharakishaji wa kesi ambazo aghalabu zimekuwa zikirundikana katika mahakama za nchi hiyo.

Benki ya CRDB imeendelea na jitihada za kupanua wigo wake wa kuwahudumia wateja na kufikisha huduma za benki hiyo kwa Watanzania walio wengi kwa kuzindua tawi jipya na la kisasa linalotembea "Mobile branch" katika wilaya ya Mlele mkoani Katavi.

images (13).jpg


Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa mkoa wa Katavi, Mh. Juma Zubier Homea ameipongeza Benki ya CRDB kwa uzinduzi wa tawi hilo linalotembea katika wilaya ya Mlele huku akisema tawi hilo litasaidia kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi katika wilaya hiyo na wilaya za jirani.

Kwanini TANAPA hawana "Mobile Zoos semi trailer trucks" kwa ajili ya kubebea wanyama pori wepesi kwa ajili ya maonesho?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Back
Top Bottom