TANAPA: Kwanini hakuna "Mobile Zoos" kwa ajili ya kubebea wanyama pori wepesi kama ambavyo kuna Mobile Courts?

TANAPA: Kwanini hakuna "Mobile Zoos" kwa ajili ya kubebea wanyama pori wepesi kama ambavyo kuna Mobile Courts?

Unajua kuna watu serikalini wanamaliza 5 years bila kuja na any constructive advice au solution to our many problems facing our country.
Mkuu, mimi binafsi ninaamini ya kwamba Mungu hakufanya makosa mtu yeyote kuzaliwa Tanzania na kuendelea kuwa hai mpaka muda huu. Ninaona kwamba nina wajibu wa kuona jamii ninamoishi inasonga mbele na kuwa bora zaidi ya jana.
 
Ikumbukwe kwamba huwezi kumkamata simba au fisi au chui aliyepo mbugani na kumbeba au kumleta kwenye maonesho, anaweza kuleta madhara makubwa kwani hajazoea kuangaliwa na watu closely. Hawa unaowaona saba saba au nane nane huwa wametolewa kwenye Zoo au bustani za wanyama, mostly ziko Arusha.
Arusha kuna snake park niliwahi kwenda...
 
Yaani kwenye sikukuu mbalimbali badala ya kuona trips za watu from Morogoro kwenda Mikumi NP au Mpanda town kwenda Katavi NP etc utakuta watu wamejazana kwenye Bar na kumbi za starehe wapiga bia...
Lengo langu mimi ni kuwalenga zaidi wanafunzi mkuu.
 
Kiuhalisia Tanapa jukumu lao ni kusimamia, kulinda na kuendeleza maeneo yote yenye hadhi ya hifadhi za taifa.

Zoos (Zoological parks) hizi zimeachwa kwaajili ya wawekezaji binafsi ( japo zipo na za serikali pia) ambavyo hata wewe kama utakua na mtaji wa kutosha pamoja na kukidhi vigezo na matakwa unaweza kuanzisha.

Kingine ni kuwa wanyama pori unaowaona katika Zoos, Ranches pamoja na wildlife farms huwa wanapatikana kutoka katika mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) .

Nadhani utakua umepata mwanga kidogo.
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kwanini TANAPA hawana "Mobile Zoos" kwa ajili ya kubebea wanyama pori wepesi kwa ajili ya maonesho kama ambavyo kuna Mobile ATMs, Mobile Court pamoja na Mobile Hospitals?

View attachment 1627675

MWEZI FEBRUARY MWAKA 2019: Rais John Magufuli wa Tanzania amezindua gari maalumu la mahakama inayotembea litakalosaidia kusikiliza kesi katika mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam. Uzinduzi wa gari hilo lenye teknolojia ya kisasa ndani yake na linalotumia umeme wa jua katika uendeshaji vifaa hivyo umefanyika leo katika maadhimisho ya Siku ya Sheria.

Gari hilo limegharimu kiasi cha Shilingi milioni 470.82. Gari hilo lenye television, kamera zenye uwezo wa kurekodi ushahidi wote kwa picha na sauti, kutoa msaada wa kuwabeba watu wenye ulemavu (lifti) na kipaza sauti kwa ajili ya kutangaza ratiba ya mahakama hiyo, linatazamiwa kusaidia uharakishaji wa kesi ambazo aghalabu zimekuwa zikirundikana katika mahakama za nchi hiyo.

Benki ya CRDB imeendelea na jitihada za kupanua wigo wake wa kuwahudumia wateja na kufikisha huduma za benki hiyo kwa Watanzania walio wengi kwa kuzindua tawi jipya na la kisasa linalotembea "Mobile branch" katika wilaya ya Mlele mkoani Katavi.

View attachment 1627676

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa mkoa wa Katavi, Mh. Juma Zubier Homea ameipongeza Benki ya CRDB kwa uzinduzi wa tawi hilo linalotembea katika wilaya ya Mlele huku akisema tawi hilo litasaidia kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi katika wilaya hiyo na wilaya za jirani.

Kwanini TANAPA hawana "Mobile Zoos semi trailer trucks" kwa ajili ya kubebea wanyama pori wepesi kwa ajili ya maonesho?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Kweli aisee!,wakiweka hiyo mobile zoo,mimi.sitaenda hifadhini kutalii.
 
Zoos (Zoological parks) hizi zimeachwa kwaajili ya wawekezaji binafsi ( japo zipo na za serikali pia) ambavyo hata wewe kama utakua na mtaji wa kutosha pamoja na kukidhi vigezo na matakwa unaweza kuanzisha.
Okay...
 
Kingine ni kuwa wanyama pori unaowaona katika Zoos, Ranches pamoja na wildlife farms huwa wanapatikana kutoka katika mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) .
Sasa mkuu, kwani hizo "Zoos" za serikali haziwezi kuwa na "Mobile Facilities"?...
 
Back
Top Bottom