KERO Tandika - Chacha na Rahaleo (maarufu Mtaa wa Wahaya) wanaojiuza wanatuharibia Watoto

KERO Tandika - Chacha na Rahaleo (maarufu Mtaa wa Wahaya) wanaojiuza wanatuharibia Watoto

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
photo_2026-09-08_12-47-54.jpg

photo_2026-09-08_12-47-53.jpg
Nina kero kuhusu eneo la Tandika, maeneo ya Chacha na Rahaleo, maarufu kama Mtaa wa Wahaya Wilaya ya Temeke, Dar. Kuna watu wanaofanya biashara ya ngono katika vyumba vilivyopo katikati ya makazi ya wananchi.

Vyumba hivyo vipo ndani ya nyumba zetu za makazi, ikiwemo nyumba namba 115, na pia kuna pub iliyojengwa katikati ya makazi. Ndani ya pub hiyo kuna vyumba vinavyotumika kwa shughuli hizo, huku nje ya pub kukiwa na vyumba vidogo vyenye milango ya nje ambavyo pia vinatumika kwa shughuli hizo.

Tatizo kubwa tunalokutana nalo ni kwamba shughuli hizi zimekuwa zikifanyika waziwazi na kusababisha usumbufu kwa familia, hasa watoto. Wakati mwingine tunakuwa tumekaa ndani na familia zetu, lakini nje tunasikia kelele, muziki mkubwa, lugha chafu na mazungumzo ya kingono ambayo si sahihi watoto kuyasikia.

Hali hii inakuwa mbaya zaidi nyakati za usiku, ambapo watu wanaendelea kukaa kwenye vichochoro na maeneo ya karibu na nyumba za wananchi. Tunahofia athari zake kwa watoto wetu, kwa sababu wanakua wakisikia lugha na kuona vitendo ambavyo havilingani na maadili tunayojaribu kuwajengea.

Tunaiomba Serikali na mamlaka husika kulifuatilia suala hili, hasa matumizi ya nyumba za makazi kwa shughuli zinazoweza kuhatarisha amani na usalama wa familia. Tunaomba pia pub hiyo na vyumba vinavyotumika kwa shughuli hizo vikaguliwe na kuchukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

Tumekuwa tukivumilia kwa muda mrefu, lakini sasa tumechoka. Tunataka kuishi kwa amani na kuwalea watoto wetu katika mazingira yenye heshima. Tunaomba viongozi wa eneo hili walichukulie suala hili kwa uzito na watufikie kabla hali haijawa mbaya zaidi.
photo_2026-09-08_12-47-51.jpg

photo_2026-09-08_12-47-52.jpg
 
Jambo ni moja, wapangishie au wauzie hao nyumba yako ukajenge mahali palipostaarabika.
 
Poleni sana wakazi wa Tandika, inasikitisha sana ni matumaini mamlaka husika zitaona hili na kulishughulikia
 
aisee hilo eneo limedhihirisha maana halisi ya "consistency" --- poleni sana wakazi wa huko
 
Hivi usalama upo wapi kwa Mademu wa kuuza kwa maclub na mahotel na hawa kwa Wahaya?..
 
Back
Top Bottom